Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

mkuu bei ya lita moja mafuta huko middle east ni chini kuliko lita moja ya maji ya kunywa.
 
Tuliaminishwa gesi hapo ntwara ikianza kuvunwa mambo yatakuwa supa. Kilichotokea kila mtu anashuhudia vipofu wanaona
 
Hivi hiyo mashine ya betting inauzwaje
Kama wakiume chukua mashine ya, betting weka laki 2 ilobaki tafuta kiti weka sehem iliyochangamka fanya biashara,, kwa weak hukosi laki moja kama faida!!
 
Huko maisha safi,

Habari za kuulizana "Ulaji wake wa Mafuta Ukoje" hamna.
 
Thamani ya pesa ya Irani ikoje ukilinganisha na pesa yetu?
 
Habari za asubuh wakuu naomba kujuzwa juu ya bei ya jumla ya viti vile vya Cello vyenye miguh ya chuma pamoja na Meza nataka nifanye biashara ya Natural Juice Bar.
 
Wadau wa JF poleni na majukumu pamoja na maandalizi ya kumaliza mwaka.

Niende kwenye mada tajwa , hivi kwa hapa Dar hasa Tabata kwa mtaji wa 500,000 ninaweza kufanya biashara gani? Najua humu JF kuna nyuzi nyingi zimeliongelea hili sijazitumia kwakuwa ni za miaka y'a nyuma sana na mambo yamebadilika tofauti na sasa.

Karibuni wadau
 
Bustani ya mboga mboga,
Anza na mazao yasiyohitaji madawa mfno matembele, mchicha, maboga etc, (achana na spinach)
Kukodi eneo 20000 la kuweza kuwa na matuta 10+
Mbegu 40000
Mbolea 25000 ya kuku kiroba wanafanya 2000-2500
Iliyobaki vitendea kazi jembe + ndoo mbili za maji.
Mapato:-
Tuta moja la mita 2 kwa 4 huuzwa kwa 15k na kuendelea kutegemeana na kujaza kwake.
Uvunaji hufanyika kila baada ya week 2, mfano matembele ukishayapanda utaendelea kuweka mbolea tu kila baada ya kuvunwa, hadi miezi 6.

Mwanzo mgumu kila la heri.
(Nina experience na hiyo shughuli, nilishafanyaga huko nyuma)
 
1.Biashara ya Karanga za kukaanga/mbichi
2.biashara ya mama ntilie
3.biashara ya miwa
4.unaweza nunua baiskeli ukakodisha kijijini
5.unaweza chonga mkokoteni ukakodisha kwa saa 1,000/=.
6.unaweza nunua nguo ama viatu vya mtumba ukaenda kuuza mtaani kwa kutembeza
7.ukafungua genge simple lenye mazaga yote mtaani
8.unaweza tumia kama ada ya kujifunza skills flani,gereji,kushona viatu,computer
9.unaweza itumia kununua na kujenga banda la kuku,kanga kwa ajili ya ufugaji
10.unaweza limia heka mbili za ardhi ifakara kwa ajiri ya kilimo cha mpunga
11.unaweza agiza vitu online vya USD 0.5 ukaja kuviuza kwa USD 2.5
Acha wengine nao wajazie
NOTE:kuweza kufanya kitu hiyo pesa na utayari wa mfanyaji ni vitu viwili tofauti.
Hiyo laki 1 unaweza lipia lodge na huyo malaya asije au unaweza walipia pombe rafiki zako na nyumbani bado wakalala njaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…