Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Nimekusoma umetisha mkuu, nimeanza vutiwa na jambo moja la kigeni katika taifa letu.... Kuagiza vitu kwa bei nafuu mtandaoni na kuuza.

Mi nina mil.2 sijui nianzishe biashara gani hapa Dar. Nishauri plz
 
Kama una chochote cha kukupatia kula. Million Moja weka Fixed account katika bank kubwa mfano mimi ningeshauri NMB (Babalao kwa sasa, inapigwa push na pia ina support maeneo mengi kitaifa)
Fixed account pesa yako haina makato na inakua salama ,unaweza kuanzia miez 6, mwaka au miaka miwili mpaka mitano...(source NMB).

Utabak na Milliona Moja ya soko linalokua ni la utalii tafuta leseni ya Travel services/Air ticketing (ila usichukue ya TALA iko juu USD 2000, Hii waweza chukua badae biashara yako ikikua ukasajili na utalii) kama utafanya ivo nione nipo soko ilo miaka mitatu sasa.
 
lazima uende mbinguni.
Bustani ya mboga mboga,
Anza na mazao yasiyohitaji madawa mfno matembele, mchicha, maboga etc, (achana na spinach)
Kukodi eneo 20000 la kuweza kuwa na matuta 10+
Mbegu 40000
Mbolea 25000 ya kuku kiroba wanafanya 2000-2500
Iliyobaki vitendea kazi jembe + ndoo mbili za maji.
Mapato:-
Tuta moja la mita 2 kwa 4 huuzwa kwa 15k na kuendelea kutegemeana na kujaza kwake.
Uvunaji hufanyika kila baada ya week 2, mfano matembele ukishayapanda utaendelea kuweka mbolea tu kila baada ya kuvunwa, hadi miezi 6.

Mwanzo mgumu kila la heri.
(Nina experience na hiyo shughuli, nilishafanyaga huko nyuma)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unahudumia jioni, mboga unauza saa ngap sasa?
ndio mkuu ni kila week mbili unavuna.
Matembele ukishapanda ndio imetoka utaendelea kuvuna mpaka miezi 6. Muhimu kila yakivunwa ni kuweka mbolea tu na kung'olea magugu.
Mchicha ukivunwa unakwatua tuta then unapanda tena. Kilo moja ya mbegu nafikiri unaweza kupanda tuta 3-4

Shamba unahudumia asubuhi na jioni.

Me nilikuwa nasoma so, shamba langu nilikuwa nahudumia jioni tu. Na mambo yalikuwa yanaenda vyema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bustani ya mboga mboga,
Anza na mazao yasiyohitaji madawa mfno matembele, mchicha, maboga etc, (achana na spinach)
Kukodi eneo 20000 la kuweza kuwa na matuta 10+
Mbegu 40000
Mbolea 25000 ya kuku kiroba wanafanya 2000-2500
Iliyobaki vitendea kazi jembe + ndoo mbili za maji.
Mapato:-
Tuta moja la mita 2 kwa 4 huuzwa kwa 15k na kuendelea kutegemeana na kujaza kwake.
Uvunaji hufanyika kila baada ya week 2, mfano matembele ukishayapanda utaendelea kuweka mbolea tu kila baada ya kuvunwa, hadi miezi 6.

Mwanzo mgumu kila la heri.
(Nina experience na hiyo shughuli, nilishafanyaga huko nyuma)
Dah aisee Respect Mr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama una chochote cha kukupatia kula. Million Moja weka Fixed account katika bank kubwa mfano mimi ningeshauri NMB (Babalao kwa sasa, inapigwa push na pia ina support maeneo mengi kitaifa)
Fixed account pesa yako haina makato na inakua salama ,unaweza kuanzia miez 6, mwaka au miaka miwili mpaka mitano...(source NMB).

Utabak na Milliona Moja ya soko linalokua ni la utalii tafuta leseni ya Travel services/Air ticketing (ila usichukue ya TALA iko juu USD 2000, Hii waweza chukua badae biashara yako ikikua ukasajili na utalii) kama utafanya ivo nione nipo soko ilo miaka mitatu sasa.

Mkuu naomba uelezee hii bzness ikoje I mean nini unatakiwa kua nacho, kufanya, jinsi gani ya kutafuta wateja, na jinsi gani unaweza kipata mapato. Nipo ktk mazingira yanayonishawishi kufanya hii kitu lkn nakosa ABC zake. Kama hutojali tuwasiliane hapa 0652494919
 
Harabi Zenu Wadau Wa JF Naamini Humu ni Sehemu Nzuri Hasa Katika Kubadilishana Mawazo na Kupeana Ushauri Katika Masuala Mbalimbali Nilikua Nataka Mnishauri Kuhusu Jambo Moja Mm ni Kijana Mkazi wa Dar Nina Mtaji wa Sh Laki Tatu (300000) Nataka kufanya Biashara Naomba Ushauri Nifanye Biaehara Gani??
Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari members!!!
Nina laki mbilia je nianzishe biashara gani?
Nipo dar es salaam mbagala.
Ushauri,maoni.
Ahsanteni.
 
Nenda manzese kuna viatu vile kama vya kimasai vya aina tofauti chukua pair tofauti
Jumla ni 4,000 per each kwahiyo hapo unaweza kununua pair30 ni 120,000
Inatagemea na wateja utakaopata ila unaanza kuuza 10 hadi 7,000 faida ni kwenye 180,000 hadi 90,000

80,000 uliyobaki nayo mwanzo
Unanunua ubuyu magomeni kwa Babu issa wa jumla
60,000 wa aina tofauti wa maziwa, wa zanzibar (wenye pili pili na ambao hauna) wenye majimaji ule nimesahau jina lake
10,000 unanunua vikombe kkoo vya kupakia ubuyu
Bila kusahau vipakiti ni kwenye 2,000/3,000

Kwahiyo unatembeza viatu huku na ubuyu wako, una smart unaweza ukawa unapost status anaehitaji unampelekea bila kusahau majirani, chuo cha karibu na ulipo
Bei weka affordable kulingana na aina ya watu wanaokuzunguka bila kusahau hali ya uchumi ilivyo
 
Viatu vya kimasai 4000?????

Jamani kuweni wakweli pale hakuna hiyo bei ... Tuweni realistic

Sent using Jamii Forums mobile app

IMG_8061.JPG

Usibishe kama hujui kuuliza sio ujinga ungeuliza ukaelekezwa

Alafu ukisoma comment kua makini tafadhari kabla hujaquote

Nimesema viatu kama vya kimasai
Naponunua mm vipo hadi 3,000 ni mtaji wako tu kuna kiwango unanunua kwa 4,000 na 3,000

Huyo wa juu yeye anauza 4,500

View attachment 1322197
 
Back
Top Bottom