Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?


Rudi jukwaa la utambulisho,ukakaguliwe
 
Uzi ishaingiwa Kirusi!! Vigumu kupata msaada wa kueleweka kwa sasa.

Hata hivyo uko wapi?

Jaribu kupitia nyuzi za Wadau wengine humu ndani waliowahi kuomba msaada ka wewe hata kama kianzio wanakuzidi. Ninaamini utaokota mawili-matatu! Pole Mkuu!
 
Pole mkuu,uzi umeingia doa Jifunzi kuwa mpole hata ukikejeliwa.
 

jaribu kufanya kilimo cha umwagiliaji
 
Siku ingine ukitaka ushauri usigusie itikadi au imani za watu utaukosa ushauri.
Japokuwa umesema huna eneo/site hapo napata ugumu kukushauri sababu ka sungura hako kadogo sana.
Lakini ungekuwa na eneo na una kilo mbili ningekushauri ufanye kilimo cha fasta kama utakuwa karib na chanzo cha maji.
Panda vitunguu swaumu ni mradi mzuri.
Anzisha bustani ya nyanya kwa wingi.
Hizo ni biashara zakukupa return ndani ya miezi mitatu.
 
Mkuu fuga kuku tu ila watengenezee mazingira mazuri kuondokana na maradhi na usiwe bahili kwenye dawa halafu uwe mstahmilivu!
 

Samahani mkuu kama kuna niliowakwaza.
Kuhusu huu mradi nimesema sina eneo kwa maana ya mabanda ya kufugia kuku maana niliona ndio mradi rahisi kuufanya.
 
Kama ni kuku kuna uzi jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji,pitia utapata namna ya kuanza.
Kuku kama unaweza pata kuanzia mita square kumi na kuendelea utafuga tuu. Ukipata eneo ukianza na jogoo watano tetea 10 au 15,ukawatibu wanaweza anza taga ndani ya wiki kadhaa.
Zingatia chanjo na chakula
 

Vizuri kaka"""
 

Samahani mkuu kama kuna niliowakwaza.
Kuhusu huu mradi nimesema sina eneo kwa maana ya mabanda ya kufugia kuku maana niliona ndio mradi rahisi kuufanya.


kumbe ni wale wale wenye I.D mbili tatu, ndio maana unaanzisha thread na kuitia madoa wewe mwenyewe! Kwa mtindo huo sidhani kama utapata ushauri sawia hapa!
 
kumbe ni wale wale wenye I.D mbili tatu, ndio maana unaanzisha thread na kuitia madoa wewe mwenyewe! Kwa mtindo huo sidhani kama utapata ushauri sawia hapa!

Sasa wewe ushauri wako ni nini?
 

ushauri mzuri sana tena pengine bora kuliko ushauri nyingine
 
kama jibu ni ndio ni PM number yako nitakupgia nitakushauri utanilipa elf 5 tu baada ya kufanikiwa au nipgie.0658825141
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…