Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

dah ! bussiness idea for elfu tano? Tsh au US$

kama ni Tsh basi wewe ni sangoma
 
Acheni utapeli na kuwadanganya watu mnapotosha jamii kama hali ya maisha imekuwa ngumu sana tumia hizo business idea zako kujiimarisha kwanza wewe@jenseny
 
Mibongo bwana! Mnajifanya kujua jua mno! Kazi kufanya biashara za boda boda tu...........!
 
kama jibu ni ndio ni PM number yako nitakupgia nitakushauri utanilipa elf 5 tu baada ya kufanikiwa au nipgie.0658825141

Mkuu pengine nia yako ni nzuri sana kwenya bandiko,Ila hujatoa utambulisho wa kutosha kuusu hiyo Idea yako,wajasiliamali hatuko ivyo mkuu(umesahau kiti kinachoitwa Customer satisfaction),ujajenga confidence kwa mteja wako.
 
jieleze kwanza na utoe ufafanuzi ili tukuamini.
Hivi ulivyokuja umekaa kitapeli zaidi.
 
Jamaa anamaanisha kuwa mwenye shida aende kwake(call him) na aleze anashida gani, kiasi cha peas a/d then,jamaa anakupa ushauri ni biashala ipi unayoweza kufanya kulingana na mtaji wako
Just think outside the box, how many of,us can come up with viable idea which has possibility of geting us out of the financial rat race????? Just keep on doing till someone make it na wegine watakuja
 
Mbona Fee ndogo sana mkuu ongeza Fee kwanza ili tukuamini kwamba upo serious.
 
habari wana jf mimi n kijana ambae nafanya kaz kwa m2 inayoningizia elfu 5 au 4 kwa siku ila nataka nianze kivyangu nikiwa na sh lak 3 msaada please
 
Jibu haya maswali halafu nitarudi badae

1. Elimu yako
2. Ujuzi au/ uzoefu wako wa kazi yoyote .
3. Una penda nn?
 
habari wana jf mimi n kijana ambae nafanya kaz kwa m2 inayoningizia elfu 5 au 4 kwa siku ila nataka nianze kivyangu nikiwa na sh lak 3 msaada please

Fanya ufigaji huria kwa kuku kienyeji mwaka mmoja ukipita ww sio kijana tena
 
Njoo hapa nikuambie. Jaribu hii:

kufuga kuku wa kienyeji;

mchanganuo:
-Tsh.60k kwaajili ya kujenga/kuandaa banda, chakula na virutubisho vya kuku.
-Tsh.50k kwaajili ya kuku wa kuanzia. Usinunue kuku wakubwa, ni ghali sana na wanakua used/wametumika sana, nunua kuku wadogowadogo waliotoka tengana na mama yao sio muda. Kwa huku (ir) bei ni tsh.5,000 so hapo utanunua kama 10 hivi. Ila make sure una mix, majogoo mawili ni tosha kabisa, vongine vijike (tetea).
-najua vitu kama maji, mtu wa kuhudumia huna haja ya kuajili mtu. Wewe mwenyewe husika maana bado ndio unaanza.
-Hadi hapo unakua umetumia Tsh.110k tu. Nyimgine iliobaki weka kwaajili ya backup ya madawa, chakula, pesa ya kumlipa docta (hii muhimu sana, usiwe bahili kuwalipa wale jamaa, ata kama kuku zako ziko poa kiafya, muite azicheki tu, sio gharama, akija mara moja unaweza mtoa buku 3 hivi fresh)
-Kuku (hao madogo ulionunua ambao umri wao ni kama miezi 4 hivi) watachukua tena kama miezi 2 ili waanze kutaga au ata kuuza. Hapo pesa itaanza kuzunguka.

Baada ya hii stage, hujamaiza:

-unaweza anza na kufuga kuku wa mayai, wale ambao hawaatamii mayai. Hapa utaanza pata mayai na kuyauza. Hivyo utakua unapiga pesa kwenye mayai na kuku.
-Unaweza pia ukanunua na zile mashine za kutotoleshea vifaranga(bei zake ni kama 80k hivi, ila lazima kuwe na umeme unapokaa).

Hitimisho;
-ukianza leo najua baada ya muda kama wa miezi 8 unaanza kupiga hela ya mayai na nyama.

Pesa ulionayo sasa (laki 3) usijidanganye ukaanzisha duka, genge, au biashara za uchuuzi wa mazao au vitu toka mjini upeleke kijijini. Hizo waachie wenye pesa ndefu, ambao ata shoti (hasara) ya laki 5 ikitokea hawayumbi. Wewe hapo ukipoteza/ukipata hasara ya laki 1 tu, kuirudisha daah itachukua muda.

Thanks.

Ila ukitoka kaka nikumbuke, mwenyewe hali mbaya hapa.
 
Mimi nakushauri kaka funguwa genge lina faida sana na utakuja kuniyambia
 
Back
Top Bottom