Ngoja nimsaidie huyo ndugu....
Belo zimepanda bei sahizi belo za nguo zunategemeana na quality ila kuanzia 250,000 kupanda unaoata belo la nguo nzuri kwa kg100.....
Kuna watu walisema zinapatikana mnazi mmoja, na kuna wengine walisema kariakoo kwa wachina wanabelo nzuri
Ila biashara hii sikuhizi, imekuwa na ushindani, so ili uwin soko uwe na nguo quality sana na uangalie walengwa wako ni watu gani na wanapenda nguo gani....
Skin jeans, brouse kali, koti jeans , korean koti [kwamikoa ya baridi], gauni kali za party [party dress] shati na suluari za officin
Hapo nimepanga kwa kufuatisha bidhaa zinazotoka sana age iwe kubwa kiasi, size za wanachuo kuliko wanafunzi wa sec ambao wengi hawawezi afford.
Ila angalizo; kununua belo kunaweza kukupa hasara kwani ni 50% 50% unaweza pata mzigo mzuri sana au mbaya sana, ila kuna wazoefu wanaangalia label [lebo] zinazowekwa kwa mabelo nje kila rangi ya label ya belo huwa inaakisi quality yake......maana kuna watu wanajulikana kwa uzuri wa kuwa na nguo nzuri pia unaweza tu toa tip kwa wanaokuuzia kuwa wakutafutie belo zuri
Ila kama huwezi pata mzoefu au mtu wa tip basi ji heri uchague nguo 1 1 sehemu za minada mikubwa dar ilala boma na kulikuwa na karume kuanzia saa 12 asubuh mabelo yanakatwa unachagua nguo nzuri kwa bei ndogo kwa laki 3 unaweza pata nguo hata 100+ kutegemea na uhitaji na nguo gani