Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Habari za mida hii wana JF,
Naomba kuuliza, kwa mtaji wa Tsh 200, 000 naweza kuanzisha biashara gani hapa Dar itakayoniwezesha kutengeneza faida ya Tsh 20, 000 kwa siku!!
Msaada wenu tafadhari!!
Mtafute somebody CONTROLA soma nyuzi zake
 
Skin Jeans za kike tunaenda Tandika na Kariakoo tunanunua kwa Tsh. 3000/= kwa kila PC 1.

Hiyo laki mbili yako unapata hizo skin jeans 50,baada ya hapo unazifanyia modification kwa Tsh1000/= kwa kila skin jeans na laki mbili yako inakuwa imeisha na unakuwa umetumia 4000/= kwa kila jeans

Huku kwetu Mbagala kila jeans unauza Tsh 10000/=,hii ina maana umepata faida ya Tsh 6000/= kwa kila jeans na ili upate faida ya Tsh 20,000/= inabidi uuze PC 4 za skin jeans na lengo lako linakuwa limetimia ila huwa tunauza hadi PC 5-8 kwa siku.

Wengi watadharau ila wengine ndio tuanishi mjini kwa style hizo

Wanangu wa Tudo watakuwa wanaelewa nilichokiandika hapa
 
Mimi machinga wa kutengeneza wadada kucha na rangi,mtaji wangu ni elfu20,siku mbaya napata15 ikiwa nzuri 20 au 25.
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]
Mkuu, tushirikishane idea tafadhari!!
Hii funny huwa inafundishwa wapi? Au unajifunza mwenyewe?
Vipi kwa Dar, naweza kujifunzia wapi?? Na yenyewe unaifanya kwa kutembea au uko na ofisi?
Ni faida nzuri unayoipata!
Msaada wako mkuu!
 
Bro kujifunza ni rahisi Sana hata week humalizi kama upo serious,mtafte jamaa anaezunguka akufundishe maana wenye ofisi wanacharge hela ndefu,utaskia laki4 miezi miwili,we jufunze kupaka na kuweka kucha kawaida,halafu unavyoendelea kufanya kazi ndio ujifunze rangi za gell na za unga,pia kuweka nyusi na kuchor a henna ukipenda,ukijua hivi hukosi50 perday
 
Safii
 
Mkuu maisha ni rahisi ukiamua kuyafanya yawe rahisi.Faida anayotaka ni faida ya 20,000 ambayo ni sawa na 10%.So anatakiwa tu ajue ni bidhaa agani ambayo anaweza akauza moja na akapata faida ya 10% on the spot.

Sasa kuhusu consistency hapo inategemea na bidii yake ila kwa uzoefu wangu katika biashara najua kwamba inawezekana kuwekeza 200,000 kwa siku na kutengeneza faida ya 20,000.Kama unakataa kwa sababu huna imani au huwezi hapo ni sawa ila haimaanishi kwamba haiwezekani.Inawezekana.

SWALI lake ni JE ni Biashara gani hiyo?JIBU langu ni Biashara ya kuuza TAARIFA.
 
Mbona umedharau walimu best mwalimu gani ambae hana mshahara wa laki sita.
 
Noted.
 
Biashara sio kiasi kikubwa cha mtaji, biashara ni MANUNUZI.

Jitahidi upate chimbo ambalo utanunu bidhaa kwa bei ya chini kabisa na ukaziuze kwa bei ya juu kidogo ili utengeneze pesa.

Kusema kwamba huwezi kuingiza 20K kwa mtaji wa 200K ni kukosa akili maani ni 10% ya mtaji.

Kutumia mamilioni ya hela ili uingize 20K nao ni ujinga uliokithiri.
 
Nikajua million mia mbili kumbe ni laki mbili
 
Acha uongo😜😜🤣
 
Habari za mida hii wana JF,
Naomba kuuliza, kwa mtaji wa Tsh 200, 000 naweza kuanzisha biashara gani hapa Dar itakayoniwezesha kutengeneza faida ya Tsh 20, 000 kwa siku!!
Msaada wenu tafadhari!!
Kuuza mayai
 
Bado hujajua mbinu zote za biashara kas bench la nyuma ujifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…