Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

HMS bravooooooo
umetoa mawazo mengi sana mazuri kwa watu wenye mitaji midogo. Like like like
 
Last edited by a moderator:
Reactions: HMS
Siku hizi hamna uaminifu wameshaondoka nao walio tangulia. unaibiwa na mdogo wako mwenyewe ktk biashara
 
inategemea uko wapi,km unaweza kwenda pembeni mwa mji unaoishi kanunue kuku wa kienyeji (hawatafika 10) ukauze mjini, au nunua beli la mtumba tembea nalo minada ya vjijini. Hatua kwa hatua uta gain momentum,usiogope kauli za watu wa humu jf, wako so impersonated,hata mbuyu ulianza kama mchicha ndg yangu
 
Reactions: HMS
Kaka haina shida nafikiri nimekosea nikakuandika wewe nilikuwa namtaka yeye.Maana kuna watu wanaomba ushauri huku wana misismamo yao kichwani kuwa ni lazima afanye kitu fulani che heshima machoni pa watu wakati hana uwezo huo.

Mimi nilishangaa sana kumwona jamaa alimaliza chuo hana kazi muda mrefu anaogopa kuuza duka la vifaa vya ujenzi kisa watu watamwonaje.

Mwenyewe ni graduate lakini ukikutana na mimi kwenye kona utashangaa kazi ninazofanya mradi hela iingie haijalishi ni kazi gani ili mradi iwe halali
Tuache hulka tufanye kazi na kwa hali hii tutaacha kulalamika kila siku serikali serikali.
 
Siku hizi hamna uaminifu wameshaondoka nao walio tangulia. unaibiwa na mdogo wako mwenyewe ktk biashara

Ukiwa na mawazo hayo biashara hautafanya. Utabaki kajiriwa wenzio wanapiga bao.
 
Sasa hivi niko kwenye biashara na napiga baooooo

Kama unaifanya mwenyewe sawa, lakini statement yako ulioitoa ni kama vile unamaanisha biashara zote ufanye mwenyewe haiwezekani, kuna watu wengine wameajiriwa na wanataka kufanya biashara, hakuna jinsi zaidi ya kumtafuta mtu mwaminifu ukamuamini akakusimamia biashara yako we ukawa ni mfatiliaji, ukianza kusema watu siku hizi sio waaminifu hauwezi kufanya biashara.
 
Very Good keep it up
 
Wanajamvi nahitaji mawazo yenu ilikujikwamua kimaisha.

 
1. Chuuza samaki kuleta mikoani
2. Mafuta ya kupikia - alizeti peleka Dar
3. Nunua mazao - hifadhi hadi bei ipande ndio uuze

Yoyote kati ya hizo au zote utatoka
 
1. Chuuza samaki kuleta mikoani
2. Mafuta ya kupikia - alizeti peleka Dar
3. Nunua mazao - hifadhi hadi bei ipande ndio uuze

Yoyote kati ya hizo au zote utatoka

asante kwa ushauri tafanyia kazi
 
Watu wachoyo sana kumchangia mwenzao mawazo tu atoke ila umbea watafanya hadi kukuche. Ushenzi sana huu ndio maana Tanzania kuendelea itakuwa ngumu na ufisadi utkuwa kwenye, kwani ufisadi ni shortcut ya kufikiri.

Kwa maana hii Tanzania ni kama imelaaniwa. Taabu sana hata ukiangalia hapa jamvini mambo mengine yanayojadiliwa ni ya kipuuzi na yale ya maana watu hawajadili kwa inavyopasa.

Hii ni challenge kwenu wanajamvi. Sasa tuone watakavyosutuka. Utapata miradi ya kutosha kambi7. Ingekuwa unaandika kuhusu mme au mke ametoroka nyumbani ungeona hata PM ungepata. Tusubiri sasa kambi7!
 
Nunua samaki peleka mahoteli makubwa, nenda mwenyewe kwa wavuvi...

Nunua dagaa peleka minadani, nunua kwa wavuvi moja kwa moja...

Au nunua dagaa peleka Dar...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…