Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Heshima yako mkuu HMS thats th best advice ever!
Mkuu umempa jamaa shyref bonge la ushauri akizingatia hayo atakuwa bonge la tajiri
Habari. Mtaji sio tatizo ila ni fikra ndo kikwazo kikubwa, na madhali umekuja kuomba hizo fikra basi fanya moja kati ya fuatayo.
Tafuta madogo wawili waaminifu wa mtaani wasio kua na ajira. Nunua maji ya jumla uwape wazungushe wauze, waweza kupiga elfu 5 kila cku faida kwa kila mmoja, kwa mwezi una laki 3 mara 3 ya mtaji wako, mambo yakienda vizuri unachukua goli unauza.
Unaweza ukawapa birika la kahawa wakazunguka mtaani wakauza, unapiga bao. mtaji ukiwa mkubwa unaanzisha genge la kahawa, unamuweka mdada mmoja anapika maandazi, vitumbua, kashata, anapika kahawa, chai ya tangawizi mwengine kijana anauza na kusimamia mapato.
Unaweza kuzama karume ukatafuta pamba za ukweli za kike (ndio wanunuzi) na simple kali, ukazama chuo chochote hostel ukawaonesha. (japo sishauri sn maana unatakiwa uwe na taste nzuri ya mavazi).
Anzisha kibanda cha kuuza fruits, tafuta dogo mmoja, awe ana katakata anauza, na dumu moja atengeze fruits ile wanaoweka kwenye glasi, mtaji unatosha.
Tengeneza askirimu za mifuko, mpe dogo akatembeze kwenye shule, kule ndo target customers wako.
Mawazo yapo mengi, ukiona zote zimekushinda, chukua hiyo hela yote nenda kwa bim kubwa, mwambie mama, nimehangaika kitaa siku kadhaa nime make jiwe moja, lkn nimeangalia matumizi yake au nan wa kumpa sijaona mwingne zaidi yako, naomba upokee pesa hii najua sio kubwa ila ongezea ongezea kwenye shughuli zako, mbusu miguu hlf sepa zako. Yaan ndani ya siku chache sn utaona opportunity za kazi zinavokuja mwenyewe utashangaa. Badala ya kuipigia misele au kuhongea au kupiga maji (meongelea kiujumla) ni bora ufanye jambo moja la heri litakalo badilisha taswira ya maisha yako, n by da way dats the ryt ting 2 do, she derves it 2 b kissed in da legs every day, morning n nyt, take it 4m me, da pain of deliverin u in labor z mch az same az dying in a car crash, o drownin in water o smashed by a train in2 2 halfs, n dats js givin birth, didn't tok abt avn u in her belly 4 9 month suffern with frequently puking n mch more, cleann ur dyper, feedin u, mch more worst wen u cried n cnt tok coz ur very tiny 4 dat n she z tryin 2 make u mute n smile coz she's feeln grieve inside seein u her only angel rolling ur tears out from ur beautiful eyes, n carry u here n der, tickling ur cheeks n tok un understandle words (lyk abububuu, papapaaa, yalobby, ashunu shunuu, bababaaa, jst 2 make u smile n singing u songs 2 make u sleep) do u know how mch terrible dat job is?, mch more feeding u, takn u 2 school, iron ur dress, washn ur pants, taking gud care of u though she z so poor 4 dat bt still struggln n neva give up, wen u grow up u sayn shitty stuffs 2 her bt neva kicked u out of her home rather dan js keepn u in heart n olwys prayn gud 4 u. ur nat dat dumb js nat 2 kiss her, nat even 1nc. man u cnt repay ur mum, u telln me u cnt even kiss her feet? dat wl b a shame n disgrace 2 God, n wl olwys feel difficulty here n hereafter. Go kiss ur mum, n u wl c da relief.
Kila la heri.
Siku hizi hamna uaminifu wameshaondoka nao walio tangulia. unaibiwa na mdogo wako mwenyewe ktk biashara
Ukiwa na mawazo hayo biashara hautafanya. Utabaki kajiriwa wenzio wanapiga bao.
Sasa hivi niko kwenye biashara na napiga baooooo
Kama unaifanya mwenyewe sawa, lakini statement yako ulioitoa ni kama vile unamaanisha biashara zote ufanye mwenyewe haiwezekani, kuna watu wengine wameajiriwa na wanataka kufanya biashara, hakuna jinsi zaidi ya kumtafuta mtu mwaminifu ukamuamini akakusimamia biashara yako we ukawa ni mfatiliaji, ukianza kusema watu siku hizi sio waaminifu hauwezi kufanya biashara.
Laki 8 ni nyingi sana kama unajicho pevu la tatu la kuziona fursa,binafsi nishaanzaga na mtaji wa Tsh40000(elfu arubain tu) right now nina ROI ya 7m kama faida every two weeks ni ngumu kuamini but thats it..anyway nisikuchoshe
Tafuta washing machine with dry cleaning system, used atleast ichukue kwa 400000 Huna haja ya kununu liquid soap you can make it by your own at your home.
Huna haja ya kukodi frem..tafuts eneo lavwazo hapo nyumbani kwako au chumba cha wazi
Tafuta hosteli na vyuo vyenye mkusanyiko wa watu wengi maeneo ya karibu yako..bandika ads kwamba unafua na kupasi nguo za wanafunzi na watu wengine kwa bei nafuu na ofa maalumu plus nguo za aina yoyote..lets say unafua na kupasi T-shirt na jeans kwa 2500 each@1250 plus ofa ya kufua boxer na vest/sidiria na chupi bure kwa mhusika mmoja..
400000 ivunje kama ifuatavyo: toa 50000 nunua baiskeli toa 100000 ingia mkataba wa miezi mitano kwanza na kijana mdogo kutoka uswekeni ambaye hana ajira wa kumlipa 20000 kila mwezi plus allowance ya 500 kwa kila complete order anayoileta(ya 2500)..mpe baiskel kwaajili ya kuchukua na kurudisha order za watu.huyu kijana usisahau kumpa motisha za malazi chakula na matibabu.
Imebaki 250000:Ivunje kama ifuatavyo
Toa 50000 nunua pasi na perfumes mbili moja ya kike na moja ya kiume(perfume ni mbwembwe tu kwa wateja wako)
Toa 30000 nunua enga za bei rahisi au tafuta muuza mitumba akuelekeze material ya kununua kwa ajili kutengeneza enga za gharama nafuu..hizi enga zitumike kutudukia na kudeliver nguo za watu..ila zisibaki kwa wateja.
Toa 30000 tengeneza kijikabti au sanduku nyuma ya ile baiskeli kwaajili ya kucollect na kudeliver order za watu.
Imebaki 140000 toa 50000 ingia mkataba na muuza maji wa karibu yako kuchukua dumu tatu kwa hesabu ya 750 kila siku za kazi kwa muda wa miez miwili..NB:Kama una'access na maji ya bure hii ni salama yako
Imebaki 90000 toa 40000 kwaajili ya kununua liquid soap materials pamoja na jiki material ya kutengeneza jiki nyumbani..
Imebaki 50000 toa 35000 iweke iwe pesa ya kulipia gharama za umeme kwa kipindi cha atleast mwezi mmoja na nusu..na 15000 kwaajili ya yale mabandiko ya printed white paper kama matangazo NB:inabidi wewe na yule kijana muwe nembo muhimu ya kuitangaza biashara yenu msitegemee mabandiko tu.
Kilichobaki ni kuanza kazi na kusubiri mvua ya wateja itakayo kuwa ikimiminika hapo ulipo..
Zingatia huduma nzuri kwa wateja wako.Na pia zingatia ulichowekeza na utakachokuwa ukikipata kama faida...pia zingatia ghatama nafuu kwakila huduma ya kuzisafisha nguo za wateja wao..lengo ni kuwa'outstand major dry cleaning franchises na kuprovide huduma kama yao ila kwa bei nafuu..Zaidi ya hapo SEE YOU AT THE TOP..WISHING YOU ALL THE BEST 😉
1. Chuuza samaki kuleta mikoani
2. Mafuta ya kupikia - alizeti peleka Dar
3. Nunua mazao - hifadhi hadi bei ipande ndio uuze
Yoyote kati ya hizo au zote utatoka