Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

jamani kwa washing mashine sampuli hii itanifaa kwa kazi kweli?
Ina KG 8 ni manual
nimeikuta dukani inauzwa ila sina elimu ya kujua uwezo wake kikazi
 
kama vp tuwasiliane mie niko dar agiza dagaa mie niuze nitaongezea hapo mtaji sawa na wako kinachopatikana tunagawana sawasawa
 
bado najaribu kutafuta market kuhusu iyo kitu
Aisee unaweza kusupply samaki sato fresh mikoani... Mimi nahitaji mtu wa kuniletea hiyo makitu kila wiki, kwa kuanzia laki moja itatosha. Hutahitaji kusafiri..mzigo utaupost kwenye basi, nakulipa kwa simu-pesa. Unalipwa ukimkabidhi mzigo konda... Haina longolongo.
 
hata mi nataka nijue maana kashauriwa kuzileta Dar
labda apeleke SUDAN

Dar labda aongee na watengezaji wa chakula cha mifugo. btw mapanki wanakula wenye hali ya chini, kuna jamaa yangu alikuwa anapeleka singida anabadlishana na mazao alikuwa anauza sana. kawaida wanachofanya kiwandani wanachuna ngozi na kuondoa mnofu wa juu tu usio na mifupa.

Kuna minofu huwa inabaki ukiangalia kwenye picha niliyoweka hapo juu utaona kuna minofu ya kutosha tu, hayo yanakaangwa ndiyo yanaenda kuuzwa watu wenye kipato cha chini wanakula.

Badala ya hiyo mi ningemshauri kama anataka biahsara ya samaki alete dagaa au fillet za samaki apeleke mahotelini.
 
oh! Ahsante
sasa ikitolewa minofu
zitanunuliwa kwa matumizi gani mengine wakati inabaki mifupa?

kwa ajiri ya kula, kuna mabaki ya minofu na wanao kula ni wale wa hali ya chini
 
1. Chuuza samaki kuleta mikoani
2. Mafuta ya kupikia - alizeti peleka Dar
3. Nunua mazao - hifadhi hadi bei ipande ndio uuze

Yoyote kati ya hizo au zote utatoka

Biashara za procuce ambazo huharibika baada ya muda ni risk. Unaweza kushtukia mtaji umepukutika. Sikukatishi tamaa, ila hakikisha umeandaa soko usije haribikiwa na bidhaa zako kabla hazijapata mteja.
 

unapatikana wapi mkuu?
 
Biashara za procuce ambazo huharibika baada ya muda ni risk. Unaweza kushtukia mtaji umepukutika. Sikukatishi tamaa, ila hakikisha umeandaa soko usije haribikiwa na bidhaa zako kabla hazijapata mteja.
la maana ilo mkuu ndo maana natafuta soko la uhakika
 
unapatikana wapi mkuu?


Huo ndipo mpango mzima wa mtiririko wa biashara bila khofu, lakini usidanganyike na ya kutembeza mitaaani utapukutisha mtaji. Mtafute huyo ndio biashara, ila jambo la kwanza nenda kaonane naye mfanye mipango kamili. Usije ukatuma mzigo halafu pesa haiingiii kwenye account yako.
 

asante ushauri mzurii huu
 
Nunua samaki peleka mahoteli makubwa, nenda mwenyewe kwa wavuvi...

Nunua dagaa peleka minadani, nunua kwa wavuvi moja kwa moja...

Au nunua dagaa peleka Dar...

hilo suala la samaki awe makini kweli sis,

siku moja niliamua kwenda Igombe kufanya utafiti juu ya uuzwaji wa samaki, kukweli watu wa pale wengi si wakweli, wengi wanaongea mambo ambayo ukiyasikiliza ni kama wanalinda soko lao binafsi...

Biashara ya samaki ni nzuri, ila kama kawaida ya biashara, lazima apambane na risks mbali mbali.
 

kweli yahitaji umakini wa hali ya juu
 
njoo gold crest jumapili kuanzia SAA 9 kuna semina ya kibiashara unaweza pata elimu itakayokusaidia. nicheki kwa hiz namba kwa maelezo zaidi 0759797874
 
Nimepata kitu kikubwa sana hapa aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…