Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kazi zinakwisha wakati wowote. Hata ukiwa mwadilifu mwenzio anaweza kuharibu mkakumbwa wote. Mwajiri pia anaweza kutokuwa na hali nzuri kibiashara ikala kwako. Tafuta biashara inayoweza kuanza na kukua taratibu unayoweza kuisimamia kulingana na muda huru ulionao hata kama utaweka msaidizi. Biashara ziko nyingi ila Tafuta biashara yenye wateja.
 
Fungua mama ntilie ya nguvu ajiri Wa mama pawe pasafi
 
fungua ntakuja na King'asti kununua vitop na skin tight. nguo biashara nzuri ila inabidi ujipange chalii
 
Last edited by a moderator:
biashara inahitaji utayari na hari ya kuifanya biashara husika.kuajiriwa isiwe kikwazo kwa wewe kujitanua vilevile utapaswa kuwa mwangalifu ili biashara yako isiwe kikwazo cha kazi yako.
 
Fungua mama ntilie ya nguvu ajiri Wa mama pawe pasafi
Yani wewe umenikumbusha wakati jamaa yangu mmoja alipofungua mgahawa wake Manzese na idea ya usafi wateja wakawa wana pita tu, waakaoogopa kukaa mle. Si kila sehemu kunahitajika usafi,
 
We jamaa piga biashara, kwa uzoefu wangu ukishauriwa n wasomi biashara utaiona ngumu, wanacomplecate mno. wewe fanya tu maisha hayana kanuni kwamba ukipita njia hii ndo utafika. Ingia mzigoni na ufanye kwa malengo.
 
Fungua chips stall! Tafuta sehemu nzuri itakupa good experience
 
Za mihangaiko wakuu wa jukwaa hili,ninaomba mawazo yenu kwenye hili,kwa mtaji wa laki mbili mtu anaweza fanya biashara apa mjin daslaam?na biashara isimbane sana sababu yupo chuo anasoma.
 
Fuga kuku wa kienyeji anza na Jogoo 2 na kuku majike 3 Kuku hawa wafuge kienyeji waache watembee wenyewe kutafuta chakula kila kuku atawanunua kwa sh. 10,00o jumla sh. 50,0000 pesa zitakazobaki atanunua madawa na kuwatunza. Hesabu ya ongezeko kila mwezi kuku 3 watataga mayai 30x6 anaweza kuwa na vifaranga 180 pamoja na kuku wakubwa watakuwa 185. Baada ya miezi 6 wale vifaranga watakuwa wakubwa nao wataanza kutaga nao ambapo hali itakuwa hivi nusu ya wale vifaranga inaweza kuwa majike baada ya mwaka 1 utapata kuku 95x mayai 10x6= utakuwa na kuku 5700. ukijumlisha na hao wa mwanzo utakuwa na kuku 5700 +185= 5885 ukiwauza utapata 5885 x bei ya 10,000= sh. 58,850,000.00. Faida ya kuku wa kienyeji ni wavumilivu wa magonjwa hawana ghrama kubwa kuwatunza wanajitafutia chakula. Unaweza kuuza mayai na nyama hasa majogoo kwa kuwa yanakua haraka.
 
Za mihangaiko wakuu wa jukwaa hili,ninaomba mawazo yenu kwenye hili,kwa mtaji wa laki mbili mtu anaweza fanya biashara apa mjin daslaam?na biashara isimbane sana sababu yupo chuo anasoma.

me pia nipo chuo!! Kuna biashara nafanya nadhan hata yeye aweza fanya kwan mtaji huo watosha kabisa!! Yuko chuo gan??
 
Baba Ilhaam ungeweka biashara unayofanya ili iwe faida kwa wengine.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…