Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,599
Mura....
amang'ana ghao weito?
Sikiliza nikwambie vizuri kitu. Mimi ni mwenyeji wa mwanza, japo kwa sasa naishi mkoa mwingine.
Kuna mjasiriamali mmoja hapo mwanza ambaye aliongoza Nchi nzima katika mid size growing industries, anashughulika na uzalishaji na usambaji wa unga, nadhani kampuni yake iko Ilemela, inaitwa KIPIPA MILLERS.
Hii kampuni tata ilianza na mtaji wa Tshs milioni moja na nusu miaka zaidi ya 14 iliyopita.
.................................
Sasa tata, huyu kama alianza na mtaji wa 1.5m na sasa anamiliki zaidi ya Tshs bilioni 5, wewe unashindwa nini?
Mimi naye nina wazo hili hili na mengine mengi tu. Nakushauri, anza kwanza kukuza mtaji angalau ufikie milioni 2 hivi kwa sababu moja, hiyo laki nne ni sawa na gharama za kusaka mashine ya kufungia mifuko, kutengeneza lebo, kulipa vibarua wachache utakaokuwa nao, umeme, usafirishaji na mengine kem kem!!!
................
Mdau Conq'ueror, bila shaka atakuwa anazijua ofisi za Makusanya pale Mwaloni Kirumba, hawa nao nimewaona toka mwaka 2004 wakifanya shughuli za usagaji na upakiaji wa nafaka mbali mbali kama mahindi na mpunga, mtafute tu kwa wema atakusaidia, ila kuwa makini usiingie gharama za ziada.
.....
Sasa tata, usiwe mvivu wa kuingia google kujitafutia malighafi za kusoma. Hii ni historia ya huyo kipipa, ilishanivutia kwa kweli...
âNilianza na Sh1.5 milioni sasa napata Sh5 bilioniâ - Makala
Tata vipi kwa kununua unga ulosagwa tayari na kufungasha kisha kusambaza kwa hiyo hela haitatosha kuanzia.
Tata!
Ngoja nikupe wazo zuri tata. Unajua tata haya mambo yanahitaji sana maandiko! Maandiko ninayoyazungumzia hapa ni pamoja na ukusanyaji wa taarifa juu ya watakaokuwa wateja wako wakubwa, competitors wako tata unatakiwa uwajue ili uendane nao, bei za soko na mabadiliko yake unatakiwa uzijue vile vile ili usije ukaenda kinyume na ukapata hasara tata.
Tatat katika mambo ya biashara na uchumi, kuna vitu ambavyo ni lazima uingie gharama kwa mfano, gharama ya usafirishaji na usambazaji, gharama za manunuzi ya vifaa vya kupakizia na mengineyo chungu nzima.
Sasa tata kwa mujibu wa mtaji ulionao, fanya kwanza mambo yafuatayo bila gharama kwanza:
Tata, hakuna biashara isiyo kuwa na MPANGO WA BIASHARA DUNIANI. HAIPO NAKWAMBIA! mpango wa biashara ndiyo ufunguo pekee unaokuonesha mtaji wako tarajio utakuwa ni kiasi gani.
- Fanya utafiti juu ya upatikanaji wa bidhaa yenyewe...
- Fanya utafiti juu ya soko unalotegemea kuhudumia hapo baadae
- Fanya utafiti juu ya gharama za mwanzo utakazoingia kama umeamua kuanza kununua na kusambaza mwenyewe
- Fanya utafiti juu ya mabadiliko ya bei zao hili unalotaka kuliingilia katika biashara.
Mpango wa biashara (Business Plan) tata una faida kuu tatu:
Kuwa makini tata, biashara za sasa sio zile za kusema eti hizi ni za wachaga wala wakinga pekee, hapana. Business is the matter of following principles, Unafanikiwa!
- Kwanza unakuonesha mtaji (Expected capital) wako utakuwa ni kiasi gani bila hata wewe mwenyewe kuumiza sana kichwa.
- Pia business plan itakuonesha Makadirio ya mapato (Revenue generation) katika kipindi chote utakachokuwa katika uzalishaji wako
- Business Plan itakuonesha pia Return on investment itakuwa ni kiasi gani kutokana na mtaji ulioingiza katika biashara yako.
nakupa ushauri ndg, unapotaka mafanikio ni lazma upambane sana tu. ww unaonekana kuwa unataka kufanya biashara nzuri lakn vitu vingi unauliza bila kufight mwenyewe. kwa huo mtaji wako huwez kufuata mahindi vijijini kwa kukodisha gari, labda upate washirika muwe pamoja. tafuta sehemu wanapoingiza mzigo kwa semi ununue hapo gunia nne ambazo zitakugharimu kama laki mbili then nenda sehemu za uswahilini zenye wakaz wengi ukaanze kusaga sembe na kuuza kwa bei ya punguzo hata la sh 500 kwa kiroba huku ukiboresha quality utapata wateja wengi tu. vidole vinauma kutaipu
Tata vipi kwa kununua unga ulosagwa tayari na kufungasha kisha kusambaza kwa hiyo hela haitatosha kuanzia.
nakupa ushauri ndg, unapotaka mafanikio ni lazma upambane sana tu. ww unaonekana kuwa unataka kufanya biashara nzuri lakn vitu vingi unauliza bila kufight mwenyewe. kwa huo mtaji wako huwez kufuata mahindi vijijini kwa kukodisha gari, labda upate washirika muwe pamoja. tafuta sehemu wanapoingiza mzigo kwa semi ununue hapo gunia nne ambazo zitakugharimu kama laki mbili then nenda sehemu za uswahilini zenye wakaz wengi ukaanze kusaga sembe na kuuza kwa bei ya punguzo hata la sh 500 kwa kiroba huku ukiboresha quality utapata wateja wengi tu. vidole vinauma kutaipu
Namba 6,7 na 9 tuwasiliane kwa namba 0765999539 niko Kirumba,nitatoa uzoefu na ujuzi wangu!
Mdau Conq'ueror, bila shaka atakuwa anazijua ofisi za Makusanya pale Mwa
Sokoro waito na mura mwomba ushauri,
1.(i)Pale mwaloni baadhi ya mashine wana gharama kubwa na ukoboaji wao na kusaga ni wa kulipua(afanye utafiti).(ii)Achague sample ya unga unaopendwa sokoni ili alenge kuzalisha unalingana au kuzidi.
2.Kuhusu parking ni bora ajue kwanza ni wepi watakuwa wateja wake wa kwanza(zinaweza kutofautiana kulingana na wateja walengwa).
3.Soko🙁a)Wakati anaanza kuuza atembelee maduka ya rejareja. (b)Alenge kuuza jina kwanza,bidhaa itafuata. (c)Wateja wawe kama ndg,ikiwezekana hata nje ya biashara k.m msiba n.k(d)Awe mwepesi kupatikana kwa wateja wake muda wote. (d)Afuatilie bidhaa aliyouza tayari kama anavyofuatilia mchumba mpya. (e)Mabadiliko ya bidhaa mbovu dukani yafanywe.(f)Ajifunze lugha nzuri,mwepesi wa kujenga urafiki na kuepuka hisia za siasa,dini wakati wa kazi ili kutokwaza wateja.
HIYO NI KWA UFUPI:
KUMB:UNAWEZA KUUZA ICECREAM ICE LAND.UAMUZI UNAO MWENYEWE. MKORERE BHUYA
Inategemea na mahali penyewe aweza kuuza nyanya au mgahawa