Mura....
amang'ana ghao weito?
Sikiliza nikwambie vizuri kitu. Mimi ni mwenyeji wa mwanza, japo kwa sasa naishi mkoa mwingine.
Kuna mjasiriamali mmoja hapo mwanza ambaye aliongoza Nchi nzima katika mid size growing industries, anashughulika na uzalishaji na usambaji wa unga, nadhani kampuni yake iko Ilemela, inaitwa KIPIPA MILLERS.
Hii kampuni tata ilianza na mtaji wa Tshs milioni moja na nusu miaka zaidi ya 14 iliyopita.
.................................
Sasa tata, huyu kama alianza na mtaji wa 1.5m na sasa anamiliki zaidi ya Tshs bilioni 5, wewe unashindwa nini?
Mimi naye nina wazo hili hili na mengine mengi tu. Nakushauri, anza kwanza kukuza mtaji angalau ufikie milioni 2 hivi kwa sababu moja, hiyo laki nne ni sawa na gharama za kusaka mashine ya kufungia mifuko, kutengeneza lebo, kulipa vibarua wachache utakaokuwa nao, umeme, usafirishaji na mengine kem kem!!!
................
Mdau
Conq'ueror, bila shaka atakuwa anazijua ofisi za Makusanya pale Mwaloni Kirumba, hawa nao nimewaona toka mwaka 2004 wakifanya shughuli za usagaji na upakiaji wa nafaka mbali mbali kama mahindi na mpunga, mtafute tu kwa wema atakusaidia, ila kuwa makini usiingie gharama za ziada.
.....
Sasa tata, usiwe mvivu wa kuingia google kujitafutia malighafi za kusoma. Hii ni historia ya huyo kipipa, ilishanivutia kwa kweli...
âNilianza na Sh1.5 milioni sasa napata Sh5 bilioniâ - Makala