Makini Buz
Member
- Jan 13, 2015
- 21
- 9
Eid Mubarak ndugu zangu waislamu.
Kuuliza ni moj ya njia ya kufahamu. Nina kiasi cha laki150 sitaki niharibu je, biashara gani naweza kufanya iwe kama kianzio?Nipo mkoa wa Kilimanjaro nimehitimu chuo mwaka jana lkn sina issue yeyote. Pls wanajamvi ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.
LAKI MIA MOJA NA HAMSINI???? pesa nyingi sana hiyo afu umesema umehitimu chuo? ulisoma nini hapo chuo eleza ili tuanzie humo kwenye ujuzi wako
Mkuu nimesoma uhasibu ngazi ya cheti n sales& marketing ila hakuna ajira ya maana
Nunua mayai ya kware uanze kuyauza,Teh teh teh?!
Mhhhh! kumbe tuko wengi hata mie nimeshahangaika sana, huwezi amin nimefanya kazi za ndani kwa wados kama houseboy kwa mda mrefu sana mpaka sasa nina akiba ya sh laki 2 so najiuliza nifanye biashara gan mi ni mpishi najua kupika kila aina ya chakula.
mdogo wangu kama huna ubishoo hiyo hela ni nyingi sana.. Nenda maeneo ya mwika, rombo nunua parachichi lete mjini..@6 month utarudi hapa JF kuwashauri wengine
Nenda kanunue baro ya mtumba nguo za watoto. Tafta minada ilipo panga chini, uza, tembezea watu maofisini hasa mashuleni ukimaliza bila shaka hiyokosa faida ya kuanzia elf 60-80, rudia mzigo tena na tena, mahtaji ya watu yatakupa uwanda mpana wa kuongeza mzigo.
Kama upo moshi mjini nenda memorial chagua nguo kwa bei nafuu, fua piga pasi tembezea watu.
Kwanini usianzishe genge la chakula mjini? Anza kutafuta maeneo yenye watu wengi pika msosi na utauza tu