Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Eid Mubarak ndugu zangu waislamu.
Kuuliza ni moj ya njia ya kufahamu. Nina kiasi cha laki150 sitaki niharibu je, biashara gani naweza kufanya iwe kama kianzio?Nipo mkoa wa Kilimanjaro nimehitimu chuo mwaka jana lkn sina issue yeyote. Pls wanajamvi ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.
 
Dah! Hapo kuna ugumu wa kuanzisha biashara ila nisikukatishe tamaa unaweza kuanza. Lkn je unania au wazo la biashara? utajituma? Fanya bishara ya mayai y kuku wa kienyeji nunua kijijini safarisha maeneo ya moshi mjini amini usiamini ndani ya miezi6 utakuwa umefika mbali zaidi and then fanya biashara nyingine tayari utakuwa una mtaji au kama vp uniPM namba zako nikuambie jambo itakusaidia mdogo wngu
 
Nenda kanunue baro ya mtumba nguo za watoto. Tafta minada ilipo panga chini, uza, tembezea watu maofisini hasa mashuleni ukimaliza bila shaka hiyokosa faida ya kuanzia elf 60-80, rudia mzigo tena na tena, mahtaji ya watu yatakupa uwanda mpana wa kuongeza mzigo.

Kama upo moshi mjini nenda memorial chagua nguo kwa bei nafuu, fua piga pasi tembezea watu.
 
Eid Mubarak ndugu zangu waislamu.
Kuuliza ni moj ya njia ya kufahamu. Nina kiasi cha laki150 sitaki niharibu je, biashara gani naweza kufanya iwe kama kianzio?Nipo mkoa wa Kilimanjaro nimehitimu chuo mwaka jana lkn sina issue yeyote. Pls wanajamvi ushauri wenu ni muhimu sana kwangu.

LAKI MIA MOJA NA HAMSINI???? pesa nyingi sana hiyo afu umesema umehitimu chuo? ulisoma nini hapo chuo eleza ili tuanzie humo kwenye ujuzi wako
 
Mkuu nimesoma uhasibu ngazi ya cheti n sales& marketing ila hakuna ajira ya maana
 
mdogo wangu kama huna ubishoo hiyo hela ni nyingi sana.. Nenda maeneo ya mwika, rombo nunua parachichi lete mjini..@6 month utarudi hapa JF kuwashauri wengine
 
Mkuu nimesoma uhasibu ngazi ya cheti n sales& marketing ila hakuna ajira ya maana

ni matumaini yangu kuwa unaweza kufanya biashara yoyote ndogo na ikakutoa sehem moja mpaka ingine, napata matumaini hayo kutokana na elimu yako.kabla hujaanza chochote kwanza anza na kufanya utafiti hapo ulipo uone jamii inayokuzungukaa utagundua kero zao kupitia kero unaweza kuzigeuza kuwa fursa MFANO watu wana kero ya maji,kumbe unaweza kuangalia namna ya kuwaondolea hiyo kero ya maji kwa kuwapelekea kwa kuwauzia maji kwa bei nafuu
 
Mhhhh! kumbe tuko wengi hata mie nimeshahangaika sana, huwezi amin nimefanya kazi za ndani kwa wados kama houseboy kwa mda mrefu sana mpaka sasa nina akiba ya sh laki 2 so najiuliza nifanye biashara gan mi ni mpishi najua kupika kila aina ya chakula.
 
Kweli ajira ngumu tujiajili vijana, serikali ishasema ajira hamna jiajirini
 
Mhhhh! kumbe tuko wengi hata mie nimeshahangaika sana, huwezi amin nimefanya kazi za ndani kwa wados kama houseboy kwa mda mrefu sana mpaka sasa nina akiba ya sh laki 2 so najiuliza nifanye biashara gan mi ni mpishi najua kupika kila aina ya chakula.

Kwanini usianzishe genge la chakula mjini? Anza kutafuta maeneo yenye watu wengi pika msosi na utauza tu
 
Mkuu kuna baro la tsh150,000/= ? niliwah uliza bei inasimamia laki3 au laki6, kulingana na ukubwa. naomba ufaham zaidi

Nenda kanunue baro ya mtumba nguo za watoto. Tafta minada ilipo panga chini, uza, tembezea watu maofisini hasa mashuleni ukimaliza bila shaka hiyokosa faida ya kuanzia elf 60-80, rudia mzigo tena na tena, mahtaji ya watu yatakupa uwanda mpana wa kuongeza mzigo.

Kama upo moshi mjini nenda memorial chagua nguo kwa bei nafuu, fua piga pasi tembezea watu.
 
Kwanini usianzishe genge la chakula mjini? Anza kutafuta maeneo yenye watu wengi pika msosi na utauza tu

Napata wakati mgum kwani hiyo hela naona kama haitoshi kuanza maisha kwani mpaka sasa naishi kwa hawa mabos wangu.
 
Umeshauriwa vizuri sana dogo....Ila ukianza biashara uwe mvumilivu..
 
Back
Top Bottom