Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Vijana wote tungekuwa na werevu kama hyu mkuu tungekuwa mbali sana.
 
Ki ukweli mi nakushauri kwa mitaa uliopo kama unaweza anzisha genge, au uza chakula, biashara za chakula huta anguka kiraisi ksb huta lazimika kununua chakula kwa ajili yako au familia"
Kama una eneo unaweza ukafuga na kuku wa kienyeji hata 5 tu vile mabaki ya chakula unaweza kuwalisha kwa malengo, hope utafanikwa"
 
Mimi nafanya biashara ya Mult level Marketing nilianza na mtaji wa laki 280 inanilipa nanaendelea vizuri kwa sasa. Nakushauri na wewe karibu laki tatu inaweza kuwa mtaji mkubwa sana kwa biashara hii. 0763797853 whatsap na live calls
Ipoje mkuu
 
Mimi nafanya biashara ya Mult level Marketing nilianza na mtaji wa laki 280 inanilipa nanaendelea vizuri kwa sasa. Nakushauri na wewe karibu laki tatu inaweza kuwa mtaji mkubwa sana kwa biashara hii. 0763797853 whatsap na live calls

Naomba na mimi nichukue namba yako plza
 

langi tatu= rangi tatu

kigori=kigoli

ulembo=urembo

iriyo= iliyo

kwa niaba ya FaizaFoxy
 
Habari zenu team! Tuungane kunishauri ni biashara gani naweza kuanzisha kwa sh laki tatu 300,000/= na ikanilipa ndani ya muda mfupi... Ushauri ndugu zanguni..Ahsanteni
*Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji*

*LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.*

[emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239]

_Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka._

*Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.*

_Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae._

*Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.*
Katika sh. 300,000 toa sh.69,500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

*Mchanganuo Wa 69,500 ni:-*
Pumba gunia 1. Shs.20,000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17,500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10,500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21,500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69,500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

*Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku*
Hivyo kuku 10 watakula kilo *1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.*
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

*TOA SHS 170,000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.*
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15,000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20,000.

Jogoo 1 = 20,000
Majike 10 x15,000= 150,000 jumla 170,000.
Itakuwa imebaki shs. 60,500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10,000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.


PITIA HAPA MKUU UFANYE KAZI ...UKIHITAJI HUDUMA YA CHANJO NA TIBA USISITE KUULIZA.
 
Je unaweza kunipa changamoto kubwa inayowakuta ukiwa unafanya mradi huu.
 
Kwanza kabisa unaweza kufanya biashara ya kuuza mayai....either mayai ya kisasa au ya kienyeji. Kwa upande wa mayai unaweza kufanya kautafiti kidogo tu ili uweze kujua maeneo ambayo unaweza kupata mayai kwa bei nafuu zaidi.... Kwa ufahamu wangu, tray moja ya mayai ya kisasa unaweza kupata kwa bei ya jumla ya hadi 6000/= kutoka shambani.....ukiwa na 300000/= unaweza kupata jumla ya tray 50 ambazo ukisambaza kwa bei ya 7500/= kwa tray moja utakuwa na faida ya takribani 75000/= kwa mkupuo mmoja. The same applies kwa mayai ya kienyeji japo yenyewe upatikanaji wake unaweza kuwa mgumu kiasi (Bei ya manunuzi kwa tray inaweza ku-range kati ya 9000 hadi 12000 kulingana na namna utakavyoweza kutafuta source nzuri huko mashambani). Kwa kuanzia, soko lako linaweza kuwa kwa wauza chipsi, mama ntilie na maeneo mengine ambako kuna uhitaji mkubwa.

Biashara nyingine unayoweza kuiwaza ni biashara ya kujumua ubuyu kutoka Zanzibar.....Kwa ufahamu wangu mdogo, unaweza kupata ubuyu kwa bei ya jumla ya shilingi 500/= ambao ukija kuu-repack unaweza kuuza kwa bei ya rejareja ya kati ya 1000/= na 1500/=. Gharama ambazo zitahitajika hapa ni za kununua vifungashio (Bei hutegemeana na ubora wake i.e. plastic or Nailon lkn bei yake pia sio kubwa kiivyo), labelling (mara nyingi ina-range kati ya 100/= na 150/= kwa kila package).....kwa hiyo kwa 300000/= unaweza kununua packet 500 halafu iyo 50000/= inayobaki unaweza kujazilishia na ukatumia kwa logistics zingine e.g. repacking, labelling n.k.....Kwa hizo packet 500 ukisambaza kwa bei ya rejareja 1500/=, unapata faida ya shilingi 500000/= (Hii ni kama utaamua kuuza mwenyewe kwa walaji). Ukiuza kwa bei ya 1000/= kwa maduka, supermarkets, na retailers wengine utatengeneza faida ya shilingi 250000/=. Ni chaguo lako mwenyewe kwamba utatumia mfumo upi kuuza bidhaa zako kulingana na mazingira yanayokuzunguka. Huwa "nasikia" ubuyu mzuri sana unapatikana kwa Babu Issa wa Mji Mkongwe Zanzibar (Unaweza kudadisi pia kwa wajuzi wa haya mambo...sifahamu sana).
NB: Hayo yote yaliyoorodheshwa hapo juu ni mawazo ghafi yanayohitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua mazingira halisi ya biashara husika e.g. usumbufu wa kodi hasa unapovusha ubuyu kutoka Zenji, ubora na aina ya ubuyu uliopo sokoni kwa sasa na mahitaji halisi ya soko e.t.c.

Naamini kwamba ziko biashara nyingine nyingi tu ambazo hazihitaji uwe na mtaji mkubwa sana, ila zinahitaji uwe highly calculated na uwe na nidhamu ya fedha ili uweze kudunduliza na kukuza mtaji wako mapema.
Usivunjike moyo reimah..YOTE YANAWEZEKANA.
 
Je unaweza kunipa changamoto kubwa inayowakuta ukiwa unafanya mradi huu.
1.soko-kama ukishindwa kutafuta mapema baada ya kuku wako kufikia muda wa kuuza ..feed consumption itakuwa kubwa kupelekea kupunguza faida.
2.magonjwa kutokana na kushindwa kufatilia chanjo tangu siku ya kwanza ya kuanza shughuli.

ukihitaji mtiririko wa chanjo na tiba za magonjwa yanayokabili mradi huu uni-pm ili tusikele watu
 
Mkuu tunaomba utuwekee mtiririko wa chanjo na tiba za magonjwa ili wote tujifunze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…