Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

muombe mtu anaejua kukaanga karanga kwa kiwango kizuri akuelekeze kisha nunua uzinunue nunua karanga kwa jumla anza kukaanga na zifungashe vizuri kisha tafuta vijiwe maeneo ya stand,mashuleni,na sehemu zote zenye mkusanyiko wa watu,,kwa mtaji uo unatosha sana usione haya we fanya pia zingatia usafi na ww muda wote uwe smart,,,,ujasema uko wapi mimi niko arusha nauza karanga na mchele kwa bei ya jumla unaweza ukaniPM
Kilo ya karanga imefika ngapi mkuu? Juzi naambiwa 3200 nikabaki na mshangao..inapanda kika siku.
 
niachiemimi,
huu ushauri mzuri ila una mapungufu especially hapo unaposema anunue matunda yanayokaribia kuharibika! katika vitu mjasiriamali anatakiwa kuepuka no kufanya biashara za ujanja ujanja na kuuza fake au substandard products! mfano hspo kwenye juice unadhani MTU akiumwa tumbo baada ya kunywa juice mbovu kesho atarudi tens?
 
Pole na majukumu.
Kwa pesa uliokua nayo unaweza kuanza na biashara ndogo ndogo kwa lengo la kukuza mtaji ili uweze kuhamia kwenye biashara kubwa. Sijui upo maeneo gani ila popote ulipo naamini kuna watu hivyo basi unaweza kufanya haya. Tengeneza uji wa lishe (ulezi), Kahawa chai na Tangawizi na uwe unauza kijiweni kwako pia unaweza kuweka na magazeti hapo kwa wale watakaopenda kujisomea wakati wanaendelea kuburudika kwa vivywaji tajwa hapo juu.

Pia unaweza kuwa unatengeneza barafu nzuri za maziwa au ukwaju na unawapa vijana wadogo dogo walio mitaani wanaenda kuzungusha na wakimaliza wanakuletea hesabu, kumbuka utamlipa kulingana na alivyo uza hivyo itampa changamoto na yeye ya kuuza sana ili malipo yake yawe mazuri.

Pia unaweza Kununua (used) toroli (guta) la kusukuma na ukalikodisha kwa wale vijana wanaobeba mizigo mjini. Labda niishie hapo kwa sasa.
 
Huku kwetu kijijini lita inauzwa tsh 300. na ikifika mjini inauzwa tsh700. ukibeba lita 100 una faida ya kutosha
Mmmh huko kunakouzwa Lita 300 panafikika? Samahani lakini mi nanunua Lita moja 2000
 
Wasikukatishe tama mkuu,biashara yeyote unayoanza na mtaji mdogo huwa inafanikiwa sana,
cha msingi tulia angalia mazingira uliyopo unaweza kufanya nini kwa hiyo laki?
nafasi yako ya kusimamia hiyo biashara,kama ukiona muda wako ni mdogo tafuta biashara yanye risk ndogo.
wote unaoona wamefanikiwa walianza na kidogo. kila la kheri mkuu.
 
Unaweza kufanya biashara yoyote kwa mtaji huo sababu mtaji mkubwa siku zote huwa no akili zako na uwezo wa kupangilia.

Jipange na tengeneza mpango vizuri usifanye biashara mpya na mazingira yako ya kuipata hiyo laki kama ni chips basi anza kwanza kwa kufikiria kuiweka kwenye ndizi maana MTU akikosa chips atakula ndizi.(Sio lazima iwe hiyo ila mfano wa hivyo).Kisha Italia kidogo kidogo hadi mtaji mkubwa utakuwa umeshapata wazo la kusimamia maisha yako yote...
 
Kuna hii biashara ya maboksi ya kufungia mzigo
Kama upo kariakoo hii biashara inaweza kukuingizia hadi Elfu 20 kwa siku kwa kutumia mtaji wako wa laki moja

Cha msingi usiwe na SONI tu kwenye kazi yako...Mungu atakusimamia na utafanikiwa
 
***
Tatizo la sisi watanzania MTU akishapaa juu tu, huona kila kitu hakifai au hujenga dharau na vijimajigambo! even "50000/-" is a enough capital for certain business!/
Sahihi mkuu,nakumbuka kipindi fulani niliwahi kusikia mazungumzo ya vijana fulani,mmoja wao alikuwa na shida yamtaji wa 50000 tuu,na alikuwa anazungumza kwa hamasa huku dalili zote za mtu aliepaniia kufanya kitu zikijibainisha wazi usoni mwake.
 
Kwa mtu anayetafuta maisha na hanaga aibu wala shobo kwenye kutafuta pesa hata elf 10 ni mtaji.. Kwa hii laki moja waweza anza kununua peni kwa bei ya jumla 100 na kuziuza 200 maeneo ya chuo.

pia unaweza kununua rim kwa 6,000 yenye karatasi 500 na kubana karatasi 4 za rim na kuziuza kwa 200 hivyo kupata mauzo jumla ya 25,000 rim ikiisha.

ofisi yako ni begi lako na sehem nzuri we zuga maeneo ya vyuoni, hii biashara nlishawai kuifanya pale Arusha tech college japo nliiacha maana ilikuwa ni jaribio tu na kiukweli ina faida
 
niachiemimi,
Ushauri wako ni mzuri lakini sio mzuri hata kidogo...matunda ambayo umesema hayafai yatatumikaje kutengeneza juice? Sio sahihi.... juice inatakiwa matunda fresh mazuri ambayo hayajatoboko. Kutumia yasiyofaa ni kuwalisha wateja uchafu.

Nilishawahi kuuza juice, matunda mazuri tu ya kawaida yanafaaa na inalipa sana. Usafi ni muhimu sana kwenye kutengeneza juice..ukikosea kidogo tu watu wanaharisha!
 
Thank you kk, umenipa bonge la idea. Nitaifanyia kazi. Japo sio mm niliyeomba ushauri
 
Back
Top Bottom