Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Weka banda la chips,halafu niajiri mimi kukuchomea chips za kiwango cha macdonald
 
*Kuwa Tajiri kwa Mtaji wa Laki 3 tu, Kupitia Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji*

*LEO TUANGALIE MCHANGANUO WA TSHS 300,000/= (LAKI TATU) KWA KUANZISHA MRADI WA UFUGAJI KUKU WA KIENYEJI.*

[emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239][emoji239]

_Hapa tuta hitaji kuku 11 tu wakubwa wanao taga yani majike 10 na Jogoo 1 tu. Kwa kutumia kuku hao 11 baada ya miezi mitatu unaweza ukawa na kuku mia Tatu 300 au na zaidi kama unataka._

*Nunua kuku wako katika chanzo cha kuaminika kuepuka magonjwa usinunue kuku sehemu za masokoni au kwenye mabanda ya njiani au kuku wanao safirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.*

_Unapo nunua kuku wakubwa kwanza unapo wafikisha wape chanjo ya mdondo (Newcastle vaccine) ili kuweka rekodi yako ya chanjo maana chanjo hii hurudiwa kila baada ya miezi 3. Ukumbuke tarehe uliyo wachanja na tarehe utakayo wachanja tena baadae._

*Usinunue kuku kabla hujaandaa banda na Chakula.*
Katika sh. 300,000 toa sh.69,500 ambayo utanunua Chakula cha kuku, kuku hawa hawana formula ya Chakula hivyo unaweza kununua material ukachanganya Chakula mwenyewe ampapo utaokoa pesa nyingi pia.

*Mchanganuo Wa 69,500 ni:-*
Pumba gunia 1. Shs.20,000 gunia la pumba lina kilo 70.

Paraza kilo 25 = 700x25 =17,500. Paraza ni mahindi yaliyo vunjwa vunjwa kwaajili ya Chakula cha kuku.
Mashudu ya alizeti kilo 15. 700x15=10,500
layer's consetraite

Kilo 25 kifuko. = 21,500.

Ukijumlisha utakuwa umepata kilo 135 kwa shs 69,500. Ambapo kila kilo moja ya Chakula utakuwa umenunua kwa shiling 514.8.

Chakula hicho kichanganye kwa kutumia chepe kichanganye vizuri kichanganyike pumba lazima iwe kavu kabisa ikaushe usiwape kuku pumba mbichi.

*Kumbuka kuku anayetaga anakula Gram 130 kwa siku*
Hivyo kuku 10 watakula kilo *1.3 kwa siku ambayo ni gram 1300.*
Hivyo tutaweza kuona Chakula chetu kitatupeleka zaidi ya siku 100 ya zaidi ya miezi mitatu.

*TOA SHS 170,000 AMBAYO UTANUNULIA KUKU.*
Mchanganuo wake Kwa kila kuku mzuri ambaye ajazeeka anayetaga utampata kwa shilingi 15,000 na Jogoo nzuri utampata kwa shilingi 20,000.

Jogoo 1 = 20,000
Majike 10 x15,000= 150,000 jumla 170,000.
Itakuwa imebaki shs. 60,500

-Hii pesa iliyobaki ni kwa ajili ya kununu material ya bei nafuu na kutengeneza banda la kuku 10 hadi 20. Kuku hawa hawaitaji banda Kubwa kwasababu hawashindi ndani wataingia ndani wakati Wa kulala jiaoni na mchana wakati wakutaga Kuku wachiwe eneo la kutosha na lenye mchanga watakao itumia kuoga kuondoa wadudu km papasi na utitiri sehemu wanayopenda kuoga nyunyizia Dawa ya utitiri.

Banda tengeneza la kuhamisha la futi 4x8x4 yani urefu kwenda juu futi 4 upana futi 8 kipenyo futi 4. Tumia materio yaliyo karibu nawe kama mirunda, mabanzi, Mabati reject au yaliyochakaa chicken wire au wire mesh, fito mbao 2x2 au 4x2 n.k. Kama ni sehemu za mjini litakugharimu kama Tsh 50,000-60,000.Vijijini au nje ya mji ambapo miti ni mingi litakugharimu Tsh 25,000 hadi 35,000.
Haya jinsi ya kuwaendeleza hao kuku ili kupata kuku wengi hadi utakao wataka. Hapa itabidi ukubali kupeleka Mayai sehemu ambapo wanatotolesha ambapo trey 1 ni shilingi 10,000.

Hapa kuku hawa 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku ambapo kwa mwezi ni Mayai 240. Kila baada ya siku 7 peleka Mayai kwenye Mashine yakutotolea (incubator). Hivyo kwa mwezi utapeleka Mayai 240 utapata wastani Wa Vifaranga 200. Hivyo baada ya mwezi nakushauri usitotoleshe tena hao Vifaranga 200 ni wengi sana kwa kuanzia kwa kuwa tayari tunenunua Chakula cha kuku cha kutupeleka miezi mitatu basi Mayai utakayo endelea kuokota utayauza kwaajili ya kupata hela ya Chakula cha Vifaranga watakao toka hao zaidi ya 200. Hivyo mradi huu utakuwa unajiendesha wenyewe.

Nikiwa na maana kama kuku 10 watakupa wastani Wa Mayai 8 kwa siku na Mayai 240 kwa mwezi ni wazi kwamba kuku hao wanakuingizia 120000 kwa mwezi ambaya sasa hela Hii itatumika kununua Chakula cha kulea hao Vifaranga ambapo Mayai ya mwezi tu yataweza kununua Chakula ambacho Vifaranga 200 watakula mwezi pamoja na chanjo na Dawa zote.

Hivyo baada ya miezi mitatu utakuwa na Vifaranga wakubwa Wa miezi miwili na Chakula cha kuku wakubwa ndo kitakuwa kinaishia hapa utachanganya Chakula cha aina moja tu wale Vifaranga watakuwa wameshakuwa kiasi cha kula Chakula chochote.


PITIA HAPA MKUU UFANYE KAZI ...UKIHITAJI HUDUMA YA CHANJO NA TIBA USISITE KUULIZA.
Nimeelewa
 
mimi nikushauri kwanza nikupongeze kwa kuwa na wazo la uwekezaji katika biashara.

Niukweli usiopingika kwamba ukitaka kuwa tajiri na kuwa huru katika eneo la kifedha basi biashara ndiyo suluhisho.

Kwa mtaji wa laki 3 kwetu sisi wafanyabiashara ni pesa nyingi sana kama ukiweza kuwekeza kwenye fursa zinazokuzunguka na zisizo hitaji mtaji mkubwa.

Siku zote biashara zenye fedha nyingi ni biashara ndogo ndogo.

Ukiweza kununua Mayai kama trei 10 za kuku wa kisasa na ukazunguka kwenye vioski vya kukaanga chips na kuuza kwa jumla ndani ya muda mchache utakuwa umekuza mtaji wako.

Mfano ukanunua trei 1 kwa sh 6500 ukauza elf 7000 kwenye trei 10 utapata elf 10

ukipata wateja 10 kila siku wote wakachukua Trei 10 kila m1 utakuta unatengeneza laki moja kwa siku faida. Hapo hujatoka?

Tatizo la watu wengi hawataki kuanzia chini ndiyo maana wanadharau fedha na kubaki maskini.
Nimependa mchanganuo huu jaribu kuutumia mkuu
 
Mimi nabeba laki 5 pikipiki nalipa elf 25 narudi na mzigo wa uhakika unapotafuta kiki hata kama co mkinga inabidi uwe mgumu kwenye matumizi ya kizembe
 
umachinga unalipa sana unakuta una mtaji mdogo unaingza pesa kede
 
Kwa mtaji huo bidhaa au Huduma iwe akili yako, nguvu zako
Ili hiyo laki inunulie vitendea kaz vyake hapo lazima unakuwa millionaire
 
Back
Top Bottom