Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

mtaji mdogo sana na inabidi uwe mvumilivu sana kwenye swala zima la kupata faida nzuri, kama sio muuza sura nenda boma sokoni wanapouza mitumba wanaanza kufungua sa10 usiku wahi mashati ya kiume jinzi model then uanze kutembeza kwa madenti vyuoni ata kwa watu binafsi, pale uwa wanauza bei rahisi sana kuliko watu wanavyopigwa mtaani,waweza nunua labda shati kwa elfu tatu ukalipiga mpaka elfu kumi...try ilo

That good
 
jf tuache matani, mimi ninalo eneo fresh katikati ya mji wa morogoro, naendesha biashara ya mgahawa lakini haiendelei, wanga wengi, chuma ulete sijui inakuaje, nikiuza pesa sioni na uuzaji wenyewe kwa siku naweza kupka mchele kg 1 na unga kg1 yaani inaumaa!! eneo nalilipia, kuliachia naona uchungu nataraji labda watoto wakimaliza masomo na uhaba huu wa ajira panaweza kuja kuwafaa, lakini nateseka sana. naomba ushauri wenu zaidi
Hiyo biashara ya chakula ni nzuri sana, ila nakushauri umuombe Mungu
 
Upo wapi.. Una penda kufanya biashara gani toka moyoni mwako na isiwe ni stori umesikia biashara flani inalipa basi nawe ume ingia ila kiuhalisia hauipendi na mwisho wa siku wengi wao huwa wana shindwa na kufunga biashara.. Kitu cha kwanza jiulize wewe una penda fanya biashara gani na kwann hiyo na sio nyingine..je umefanya juhudi gani za kutosha za kuji funza kwa watu wanao ifanya hy bzness..ili ujue changamoto zake na faida zake..je hiyo biashara kwa eneo ulilopo baada ya mda flani ina weza leta faida na kuanza kuji endesha yenyewe... Mm naweza kukushauri uza mahindi ya kuchoma ina lipa..kumbe eneo ulilopo n kijijini kila mtu ana shamba lake au nika kwambia uza bible hapo ulipo kumbe jirani ulipo wewe kuna msikiti au uza quran kumbe jirani yako kuna kanisa hapo lazima biashara iwe mbaya... So wewe sema nipo sehemu flani mazingira niliyopo kuna hichi na hichi so kupitia hayo mazingira wewe binafsi unaonelea ukifanya biashara hii itakuwa sawa..je wadau mna nishauri nn so watu wana anzia hapo.. Yangu n hayo kama nime kukwanza samahani
Kwa kuangalia biashara mtu unayopenda mie naapenda biashara za kupimp magari, kama TTR AUTO UPGRADES toka niko mdogo, sasa ukiangalia ile ni biashara ya pesa ndefu unafikiri ntawezaje kwa mtaji wa chini ya milioni? Nafikiri ishu sio biashara unayopenda, ishu ni biashara ilio ndani ya budget yako na management skills, hata kama huipendi ila ikupe mtaji wa kuja kufanya business unayoipenda baadae
 
Habari zenu wadau

Naombeni ushauri

Kwa mtaji wa laki mbili naweza fanya biashara gani maeneo ya chuo na ikanilipaa???

Nimewaza nyingi ila nipeni uzoefu

#Ni maeneo ya Moja ya chuo kilichopo Dodoma
 
Nunua Rim uuze moja moja, Rim moja inakaa karatasi Nadhani ni buku, Ukiuza kila karatasi moja kwa 100 Aaghh uongo, Hakikisha kila mtu anajua kuwa unauza Rim moja moja. Utanikumbuka
 
Nunua Rim uuze moja moja, Rim moja inakaa karatasi Nadhani ni buku, Ukiuza kila karatasi moja kwa 100 Aaghh uongo, Hakikisha kila mtu anajua kuwa unauza Rim moja moja. Utanikumbuka
Hii hapana
 
Habari zenu wadau

Naombeni ushauri

Kwa mtaji wa laki mbili naweza fanya biashara gani maeneo ya chuo na ikanilipaa???

Nimewaza nyingi ila nipeni uzoefu

#Ni maeneo ya Moja ya chuo kilichopo Dodoma
Fungua genge la matunda linalipa
 
Natamani kufanya biashara za online, nitengeneze website ambayo nitafanya booking za mabus ya mkoani so nilikuwa nataka kujua changamoto zake kama mtu ana experience yeyote ya hiyo biashara?
 
Back
Top Bottom