Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Wazee toeni somo vizuri bas kuhusu hii chia seeds na wengi tunaweza kuwa interested na kufanya hii biashara
 
Mikoa ya Dar,Moro, Mwanza,Mbeya,Arusha na Moshi kote huko lishaanza kusambaa kwa kasi sana.Unasaga kwa blender au mashine yeyote halimradi huwe unga pata vijiko 2 vya chakula kutwa kwa kuchanganya na juice,chai,mchuzi au chakula plus matunda utapata matokeo ndani ya masaa 48.
isije ikawa kama zile mambo za mayai ya kware....
 
Option 1
Huu ni wakati wa likizo na vijana wengi wapo mtaani, tumia nafasi hii kuwavuta kwako. Unaweza kwenda kununua Toys za mtumba laki tatu, kwenye laki inayobakia nunulia box za kufungia zawadi na gift papers. Hakikisha unabakiza hela ya kutosha kununua betri na kumlipa fundi wa kurepair zilizoharibika. Hizi ukiuza hukosi milioni mbili, sema utatumia miezi miwili kuuza na biashara itasimama tena January na Feb
Opt 2
Tumia hiyo hela kulipia uwanja wa shule hapo mtaani kwenu, tafuta wadada wawili na wakaka wawili wenye njaa ya mafanikio kama wewe. Nifuate DM tuangalie uwezekano wa kuweka vifaa vya watoto kuchezea kwenye huo uwanja, tuna vitu vya kisasa kuanzia jumping castles, swings, merry ground, climbers, hadi inflatable pools. Hapa unaweza kufanya kwa muda mfupi tena hutokuwa na mamlaka maana ni biashara yetu wewe utakuwa na asilimia zako kadhaa kwa kutupatia eneo na wasaidizi.
 
Wazee toeni somo vizuri bas kuhusu hii chia seeds na wengi tunaweza kuwa interested na kufanya hii biashara
Kitu hakifahamiki lkn unaambiwa kina faida kubwa.. Hao wateja utawapataje?
 
Uza glass ptotecta na makava ya simu
Tena uzitembeze mwenyewe hadi ukue
1. Glass za kawaida 800 utauza 3000 adi 5000
2. Glass za 3d na 5d 4000 utauza 10000 na 15000
3. Makava ya kike na kiume clasic 4000 utauza 10000 na 15000

Nina Tsh 400,000/= (laki nne) nahitaji ushauri nifanye biashara gani ambayo inaendana na pesa hii ili nipate faida nzuri. Sio lazima iwe biashara, inaweza ikawa kitu kingine chochote kile cha kunipatia pesa (faida).
Nipo Ubungo Msewe, Dar Es Salaam
 
Mimi ni mwanachuo wa UDOM kinachopatikana Dodoma. Mimi pia ni mtoto wa mkulima hivyo namshukuru Mungu nimepata mkopo. Sasa wakuu kwa pesa ya mkopo ndani ya miezi miwili Mimi nimepiga tathmini naona laki 2 inanitosha kwa matumizi sasa nilikuwa nawaza January nikipata ile pesa ya chakula nianzishe mradi wa kuniingizia kipato ampapo ntakuwa na laki 3, ila nin a laki nyingine hivo jumla ntakuwa na mtaji wa laki NNE. Jee ni biashara gani ndogo ambayo kwa huo mtaji naweza anzisha na kumuweka mtu angalau kunizalishia hata 5000-10000 per day. Ushauri wenu unahitajika kusudi nikimaliza chuo niwe na pakuanzia wakuu. Natanguliza shukrani kwenu wote.
 
Tuwasiliane whatsap nikupe mchongo 0622 296251
 
300,000
Gunia la viazi vitamu shambani ni 60000
Mabibo sokoni 100000
Nunua gunia 4 kwa 240000
Nauli mpaka shambani ni 20000
Inabaki 40000 ya nauli ya mzigo mpaka sokoni.
Ukiuza utapata 400000 toa mtaji wako 300000 unabaki na 100000.
Kutokea hapo unaweza kujiongezaa ndugu.
Shambani wapi Mkuu
 
Back
Top Bottom