Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mtaji ukiwa mdogo na biashara itakuwa ya kitoto kama kuuza maji,juice, mama ntilie nk! Endelea kuzichanga ili uanze biashara kwa mtaji mkubwa!!
 
Habar waungwana ningependa mnishauri niko tayar kufanya biashara ya aina yeyote mana nikitu napenda kukifanya mda mrefu ila nna mtaji wa 750k nasijui nifanye biashara gani ushauri wenu kwangu ni jambo jema tafadhali....
 
Tafuta eneo lenye watu wengi , uza mitungi ya gesi Anza kuuza mitung midogo ya kilo6 , mtaji ukikua utauza na mitung mikubwa, onana na mawakala wakuu wa kampuni za gesi km oryx na mihan watakupa ushauri zaidi kuhusu hii biashara, kwa mtaji ulionao unatosha kabisa kuanza hii biashara
Asante mkuu je kwa mtaji wa laki 7 na 50 utatosha kulipia frame nakununua hizo bidhaa
 
Sema upo mkoa gani..umeoa/kuolewa Then tukupe chochote kitu maana kuna ushauri wa kumpa bachelor na mtu mwenye familia.
 
Sijajua eneo unalotaka kufungua biashara frame zinakodishwa kwa shilling ngap, , lakini unaweza kuanza na mitung 15 midogo ya kilo6, ambayo utanunua shilling 45,000/ complete pamoja na vifaa vyake kwa wakala mkuu , we utauza kwa Bei yoyote utakayoitaka inategemea na sehemu uliyopo, ukichukua 45,000/= ukizidisha kwa 15 (idad ya mitung) itakucost 675,000/=
Unaweza ukaanza kwa kuuza mitung ya kampuni mbili tofaut mfano mihani ukanunua mitungi 7 na oryx ukanunua mitungi 8 , unaanza biashara, ,
Shukran mkuu asante sana ntalishughulikia
 
Habar
Namba kusaidiwa wazo la biashara!
Walau niishi kwa uafadhali...
Je ni biashara gani itaniweka mjini ndani ya kianzio cha laki4?.
Nipo kigamboni.
 
nimekaa na kujishauri kuhusu swala la ujasiriamali nimewaza sana lakini nimeshindwa pata jibu ni biashara gani naweza fanya nanina mtaji wa laki 5
Anzisha biashara ya dagaa wakavu au wa kukaangwa hutojutia, me ndo biashara yangu nauza jumla na leja leja ukihitaji nambie
 
Nunua mashine ya cherehani 150,000

Nenda machinga complex kodisha kizimba kwa mwezi 20,000

Anza kushona nguo kwa pesa zilizobakia kisha nenda ukauze madukani kariakoo na posta na mnazi mmoja

NB: Ubunifu ni muhimu
mpaka leo bei ipo hivyo kizimba kukodi
 
Wapendwa poleni na majukumu,

Ninaomba mnisaidie mawazo kuhusu hili wazo langu

Nina cash shilingi 500,000 na sijui nifanyie biashara gani cause sijawahi kuwa na biashara ila ninaweza kuendesha biashara

Aksanteni
ungesema eneo ulilipo ingekua atleast nafuu kwa wanaokushauri ila pia napenda kushauri wam JF kua sio lazma uanze biashara ukiwa peke yako unaweza mtafuta mtu mnaeendana ktk mawazo mkachanga na kukuza mtaji halafu mkaanza kufanya harakat pamoja
 
Kama kawaida mtu wenu apa Jstar1, naomba kupata uzoefu wa biashara ya kupaka rangi, kucha za wadada.

kuuza vinywaji hasa hasa maeneo ya stand, yaani kuanzisha kama genge.


ila wakuu mdogo wenu nina mshahara wa laki 5, ivi ipi kati ya izo mbili itanifaa, au kipi ntaanzisha nkiwa na mtaji wa laki 5.

naomba msaada na baada ya mwaka mmoja ntaleta mrejesho apa, namaanisha,
 
Back
Top Bottom