Mkuu Nenda Sokoni Kisutu kuna Korosho nzuri safi zilizokaangwa(Rosted and Salt) zinauzwa Elfu 9 hadi 10 Kwa Robo kilo nunua vifuko special vile vidogo vinauzwa elfu Tano kwa pcs 50 yaani kimoja ni Mia Korosho unaweza nunua robo kilo unajaza kwenye kifuko kwa kutumia Mzani ile midogo digital gram 20 ukimaliza kujaza vifuko vitatoka vifuko 25 kila kifuko kilichojaa Korosho utakiuza kwa bei ya Shs 1,000/= so ukifanikiwa kuuza vyote mauzo yatakuwa elfu 25,000/= gharama za Matumizi ya kuandaa bidhaa itakuwa 5000/=vifuko,Korosho 9,000/= Jumla 14,000/= Faida itakuwa 11,000/= Hapo unaweza tumia akili zako kama umezaliwa nazo ukaenda kwenye maduka ukawauzia kwa bei ya jumla kifuko komoja ukawauzia mia 600 au 700 upate faida ya 400 au mia tatu kwa kila kifuko au unaweza omba mwenye duka akuuzie faida mgawane n.k but unatizama mauzo yakiwa fresh unaongeza mzunguko wa kutafuta masoko ila hakikisha Korosho zile Tamu na Safi ikiwezekana unachambua unaondosha zile mbaya ukiendlea unaweka na namba yako ya simu kwenye vifuko maisha yataenda... ukiwa na mkono wa Biashara hiyo pesa unaweza rudisha mkopo ndani ya siku kadhaa tu. Nimekupa Mtaji mdogo kabisa wa kuanzia ambapo ni robo ya ulichonacho.
kama Umependa Gonga Like. Utashukuru ukifanikiwa