Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Mara kubwa! Uko Tarime au Musoma au Bunda au Majita au Serengeti au hapo Musoma mjini!? Kote huko kuna biashara tafauti tofauti unazoweza kufanya kwa mtaji huo wa laki tano.

Kwa mfano nunua sangara uza, nunua ndizi Tarime uza Musoma au Bunda, nunua kuku Bunda au Tarime uza hata Mwanza. Biashara ziko nyingi hata hivyo itakubidi wewe mwenyewe ulichambue soko husika. Ziko nyingi.
 
starrony[U said:
[/U];4873093] Jamani naomba msaada wenu,nina mtaji wa laki tano tu, naitajikufanyabiashara,nasijui nifanye biashara gani,iliniweze kutimiza malengo yangu.

uko wapi mkuu


Mkuu Mshauri tu kama vipi coz inawezekana wengi wakafaidika na ushauri wako.
Asante kwa kuonesha moyo wa kusaidia.
 
Nadhani ni muhimu pia kutaja sehemu ulipo ili wachangiaji waweze kukupatia fursa zilizopo hapo mahali ulipo. Mfano unaweza kushauriwa kulima ufuta kwa mtaji ulionao endapo tu upo eneo ambalo ufuta una stawi.
Mkuu Mshauri tu kama vipi coz inawezekana wengi wakafaidika na ushauri wako.
Asante kwa kuonesha moyo wa kusaidia.
 
Unaweza kufnya biashara ya loan sharking, kwa kukopesha watu waaminifu wenye shughuli zinazowaingizia kipato kila siku kwa masharti na riba nafuu ila kwa muda mfupi. Mfano ukawa unakopesha kuanzia Tsh 10,000/- hadi Tsh 100,000/- kwa mtu mmoja kwa riba ya 10% kwa wiki au 40% kwa mwezi.

Tafuta mwanasheria au wakili akuandalie mkataba utakaokuwa unawakopesha wateja wako, pia uwe unaandikishiana nao kwa mjumbe, serikali za mitaa au afisa mtendaji wa kata pamoja na mashahidi.

Ukiwa interested niPM nikupe taratibu, sheria, changamoto, mikakati na mbinu za hii biashara.
 
Chupi za kike zinatoka sana, japo sijajua malengo yako ni yapi
 
Jamani naomba msaada wenu,nina mtaji wa laki tano tu, naitajikufanyabiashara,nasijui nifanye biashara gani,iliniweze kutimiza malengo yangu.

Huwa kabla ya kumshauri mtu,napenda kumsikia mtazamo wake wa awali kwakuwa lazima kuna ullichowaza,yawezekana ukawa na wazo lenye kuwa na tija ila linatakiwa kuboreshwa tu au kurekebishwa kidogo au kuongezewa kitu.

Changamoto katika biashara ya kumkopesha mtu ni RISK kubwa sana,ingawa ina returns kama itafanikiwa. Daima kwa mtaji kama huo ni vyema kuelewa risk ya biashara uitakayo,upatikani wa wateja na faida yake.

Huo ndiyo ushauri wangu,ukishasema ulichowaza naamini kunaweza kupatikana kitu kizuri sana kutoka kwa wachangiaji.
 
Wadau habari!jamani mimi ni kijana niliyemaliza elimu yangu miaka kadhaha (zaidi ya mitano) iliyopita!ila tokea wakati huo sijabahatika kuajiriwa,nimeshakata tamaha,na nimeonelea bora nijiajiri!

Nina mtaji wa Tsh laki tatu (300,000/=) na wazo kuu ni kuanzisha kilimo hasa cha mahindi na baadae mpunga hasa mkoani Morogoro,naomba maoni yenu wadau je kwa mtaji huo naweza kuanzisha kilimo kweli?asanteni.
 
Kama unategemea fedha hizo hizo kwa kukodisha mashamba, kununua mbegu, mbolea, kulipa vibarua, kulinda na shughuli nyingine za shamba; fedha hizo hazitoshi. Hata tukisema shamba lako na utalima, kupanda na kupalilia,kulinda na kufanya shughuli zotemwenyewe bado utahitaji mbegu, mbolea, usafiri.
 
Kama unategemea fedha hizo hizo kwa kukodisha mashamba, kununua mbegu, mbolea, kulipa vibarua, kulinda na shughuli nyingine za shamba; fedha hizo hazitoshi. Hata tukisema shamba lako na utalima, kupanda na kupalilia,kulinda na kufanya shughuli zotemwenyewe bado utahitaji mbegu, mbolea, usafiri.

Asante mkuu,mashamba tayari nimekodi maeneo ya Kiteto Kilosa,ni mashamba yenye udongo wenye rutuba yasiyohitaji mbolea,niwaza labda nianzie na heka mbili kutokana na mtaji mdogo!

Kwa kulima shamba kule ni 35,000= mpaka 40,000/= kwa heka!kupanda ni 15,000/= kwa heka!tatizo sijawa mzoefu na kilimo kwa kua ndio naanza ndio maana nahitaji ushauri wenu wakuu!
 
Usikatishwe tamaa, maamzi yako ni mazuri. Minimkulima na kidogo nina uzoefu. Sifahamu jiografia ya moro. Kwa Sumbawanga unaweza. Mpunga kukodi ekari 1 ni laki 1.

Kulima kila eka elf 25. Huhitaji mbolea. Ni very fertile. Shughuli zote unaweza baki na change. Na mavuno si chini ya gunia 20. Faida ni zaid ya mara 4.
 
Pia kumbuka hilo jina lako linaweza kukugharimu.

Majina/maneno yanaumba.

Ha ha ha ha!mkuu umenichekesha sana,sasa nitafanyaje wakati ndio natambulika hivyo hapa J.F,tukipambana jina litabadilika tu automaticaly!
 
Asante mkuu,mashamba tayari nimekodi maeneo ya Kiteto Kilosa,ni mashamba yenye udongo wenye rutuba yasiyohitaji mbolea,niwaza labda nianzie na heka mbili kutokana na mtaji mdogo!kwa kulima shamba kule ni 35,000= mpaka 40,000/= kwa heka!kupanda ni 15,000/= kwa heka!tatizo sijawa mzoefu na kilimo kwa kua ndio naanza ndio maana nahitaji ushauri wenu wakuu!

Kukodi ?
Kulima = 40,000
kupanda = 15,000
kupalilia = 80,000 ( kama pana rutuba palizi huwa 2 kila moja nimekadiria 40,000
kulinda = 50,000 (makisio)
kuvuna = 100,000 (kuvuna, kukusanya na kupiga)
usafiri = 80,000 (hapa itategemeaa ukiyatoa shamba unapeleka home kusubiri soko au unapeleka sokoni, gharama zinaweza kuzidi.
magunia tupu = 40,000
unaona, inakaribia 500,000 ingawa haya si mahesabu rasmi. Ningekushauri umtafute mkulima mkweli wa eneo lile akupe picha kamili ili uone kama inawezekana. 300,000 haitoshi.
 
Usikatishwe tamaa, maamzi yako ni mazuri. Minimkulima na kidogo nina uzoefu. Sifahamu jiografia ya moro. Kwa Sumbawanga unaweza. Mpunga kukodi ekari 1 ni laki 1. Kulima kila eka elf 25. Huhitaji mbolea. Ni very fertile. Shughuli zote unaweza baki na change. Na mavuno si chini ya gunia 20. Faida ni zaid ya mara 4.

Asante sana mkuu,nashukuru kwa kuzidi kunipa moyo wa kuthubutu,jiografia ya Moro kwa maeneo xa Kilosa,Dumila,Mvomero na Mikese ni maeneo yanayokubali sana mahindi,na kukodi heka moja huku ni kati ya 10,000/= mpaka 25,000/= kwa msimu!target yangu ni kuanza hii ya mahindi angalau nipate mtaji wa kuanzisha heka 5 hivi za kilimo cha mpunga kwa umuagiliaji maji
 
h=Hela hii ungewekeza kwenye bustani ya lisilo zidi robo hekari ingekulipa zaidi kuliko hicho kilimo unachotaka kwenda. sikukatishi tamaa ila kilishaniliza kwa kiasi fulani.

Vinginevyo kwa kuwa huna kazi kabisa basi fanya kwanza biashara ya kuku na huku ukiendelea kulima kwa kuwafata kijijini na kuwaleta mjini inaweza ikakutoa saaaana
 
Back
Top Bottom