Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

aha kuandika kihuni wewe dogo
kama huna la kumsaidia kaa pemben,sio kusema anaandika kihun.hapo mkuu kama utaweza hyo laki nne na nusu kafungue fixed acc. af iweke then bum lingine litakavoingia la mwanzo wa muhula tafuta kifrem ambacho utakua unalipia hata 40 kwa mwez afu anzisha hata biashara ya nguo za ndan kujumua dar tafuta wa kukujumulia na kuagiza,maelezo meng mno km vp tupia email au phone number ako nkupe idea cos we are on the same boat
 
Mpesa kijana au Tigo Pesa.
Kwa haraka haraka fanya survey hapo chuo uone majority wanatumia mtandao gani wa simu sana kati ya tigo na voda.
Kwa uzoefu wangu wengi wao wana line za tigo. Sasa cha kufanya anza na biashara ya tigo Pesa coz tigo wanapanuka haraka sana kwa sasa kwenye tigo pesa. Pili ni cheap kuanza na tigo pesa koz hawana longo longo kama walivyo Voda.
Kingine ni kwamba wateja wengi sasa hivi wa mitandao ya simu wanatumia huduma hizi mbili kwenye mobile pesa kati ya voda na tigo so lazima utapata wateja wa kutosha.
Commission yake iko vizuri so jiunge huko uanze biashara mzee. Uzuri wa hiyo kitu unaanza kula faida mapema ukiwa hauna stress halafu unaweza ku manage vizuri biashara yako hautahitaji mtu wa kuajiri mpaka itakapo panuka zaidi huko mbele. Unaweza jikuta unaanza kujiajiri mapema hata ukimaliza usiwe na hamu tena ya ajira.

Mkuu hivi unajua tigo pesa na m-pesa till zao wanauza tsh ngap? Ni tsh 1,000,000 na ili biashara iende vizuri lazima uwe na si chini mil.2 kwa kila line.

Na ili upate comission nzuri lazima uwe na mtaji mkubwa vilevile uwe unafanya transactions kubwa kwa wanaotoa na kuweka.
 
Habari wana jf mm ni mwanafunzi wa chuo natarajia kuhitimu chuo mwakani Mungu akipenda na ningependa kuanzisha biashara yangu ndogo naombeni mawazo yenu ni biashara gani ndogo itakayonitoa
 
Inabidi liwe wazo lako hasa ukiangalia matatizo katika eneo lako na kutumia tatizo hilo kama fursa.
Mf. Tatizo la maji safi na salama katika eneo lenu unaweza kulitumia kama fursa ya kuanzisha kiwanda kidogo cha maji ya kunywa na kuwauzia watu kwa bei nafuu.
 
Habari wana jf mm ni mwanafunzi wa chuo natarajia kuhitimu chuo mwakani Mungu akipenda na ningependa kuanzisha biashara yangu ndogo naombeni mawazo yenu ni biashara gani ndogo itakayonitoa

Ndugu maelezo yako hayajitoshelezi, hivi mtu akikujibu kifupi tu "kachome mahindi" atakuwa amekusaidia!?? Sema uko wapi, mtaji wako, muda wako, fursa ganí unazozióna, una uzoefu wowote e.t.c ndipo ushauriwe... kha!
 
Habari wana jf mm ni mwanafunzi wa chuo natarajia kuhitimu chuo mwakani Mungu akipenda na ningependa kuanzisha biashara yangu ndogo naombeni mawazo yenu ni biashara gani ndogo itakayonitoa

Ndugu maelezo yako hayajitoshelezi, hivi mtu akikujibu kifupi tu "kachome mahindi" atakuwa amekusaidia!?? Sema uko wapi, mtaji wako, muda wako, fursa ganí unazozióna, una uzoefu wowote e.t.c ndipo ushauriwe... khaa!
 
Habari wana jf mm ni mwanafunzi wa chuo natarajia kuhitimu chuo mwakani Mungu akipenda na ningependa kuanzisha biashara yangu ndogo naombeni mawazo yenu ni biashara gani ndogo itakayonitoa

mawazo yako ni safi lkini lazima tuambizane ukweli. ili kuweza kufanya biashara hata ndogo ni lazima kuzingatia ubora wake na sustainable one. wengi wetu wanalipua kwa kutaka kupata haraka faida kubwa! ningeomba tuangalie wenzetu kupanga vizuri halafu we dont to think big kwa sababu cha muhimu hapa ni kuwa na kiabiashara cha uhakika as a starting base
 
Mtaji ni kama laki 4 au 5 hivi na mda ntakua na mda wakuengange kwenye hyo biashara full time mana ntakua nmemaliza shule mda huo
 
Nafikiri ni vyema kuchunguza zaidi ili uweze kufanikisha lengo kulinga na mtaji mdogo uliyo taja pia ukubwa wa mtaji hutengemea zaidi aina ya biashara na mazingira husika.

Mc!

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
jameni, nadhani mwanafunzi anachouliza je ni kwa kivipi anaweza kuanzisha biashala,

ingekuwa vyema tukamsaidia ki mawazo kwani na amini kuwa kuna biashala ndogondogo anazoweza anzisha na zinahitaji mtaji kidogo wa fedha, kwani mtaji mkubwa na yeye mwenyewe
 
Tafuta mtu anaeuza kitu chake kwa bei ya hasara na waponwengi wanakua na shida na uwe unakaa nacho utapata anaihitaji yani uwe dalali hapo chuo
 
Wa tz hatuna tabia ya kusema uzoefu halisi wa shughuli tuzifanyazo,tunatoa ideal za maneno ya kwenye vitabu tu
 
Mimi nina uzofu na biashara ya network marketing, ya Syntek Global, kupitia bidhaa ya Xtreme Fuel Treatment.

Wakati una fanya biashara tambua bidhaa au huduma utakayotaka kuiuza. Je ina sifa ya kuuzika, upande wa vyakula tuchukulie mayai una weza ukawa hauna uwezo wa kufuga kuku ila kuna watu unao wafahamu wana fuga kuku, wewe una kazi ya kutafuta watu ambao wangpenda uwa supplie mayai, hivyo tumia ushawishi wa kibiashara kama punguzo la bei na kadhalika.

Biashara ina hitaji uvumilivyu, moyo wa kujituma na creativity. Chukuwa muda kujijenga na kujiweka na watu wenye mawazo ya kujiendeleza.
 
Nahitaj kuanzisha biashara ndogo mpaka saa nina kiasi cha shiling laki 600000 ktk akaunt yangu bank
Naomba kusaidiwa kupata mawazo ya biashara ip nifanye nikiwa na hiyo lak sita
 
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima,

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?
Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe

2. BADILISHA HOBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?
Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYALI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. Kununua Franchise
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustalehe
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TECHINOLOGIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI ZINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza

11. ANAGALIA NEWS NA MAKALA MBALIMBALI
Kunachaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa inamakala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. CPY BUSINESS AIDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copya aidea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika

13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyesho ya biashara
-Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
-Kwa marafiki

14. UNAWEZA GUNDUA KITU?Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikoa kwako

SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUOATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA
 
Duh,Chasha nimekuinulia mikono mkuu.

Mungu akubariki kwa kazi unayoifanya,maana mie mwenyewe imebidi ni Print hizi points niwe nazipia.Mungu atakulipa kwa unalofanya,maana wengine hapo ungesikia hembu ni PM nikupe wazo kumbe wanataka pesa,lakini wewe umetoa muda wako kuweka wazo na njia za kujikwamua tena kwa kina.Wengi tumefaidika kaka.

Mungu yupo naye na kwa kila atakaefanikiwa basi jua mungu amekuwekea fungu lako hapa duniani na siku ya mwisho.

Maana wengine wangemkatisha tamaa kwamba pesa ni ndogo,ila wewe umeweka wazi kwamba hakuna pesa ndogo kwenye kuanza maisha
Stay blessed

Ila wazo kwako,inaoneakana una uzoefu sana mkubwa wa masuala ya ushauri,ningeomba anzisha kitabu au vitabu vyenye siries ya ujasiriamali katika nyanja mbali mbali
 
Back
Top Bottom