Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Dah naskitika hukujibu maswali yote ipasavyo.well, zingatia ushauri wa kufuga kuku hata kama hupendi.
 
Jibu haya maswali halafu nitarudi badae

1. Elimu yako
2. Ujuzi au/ uzoefu wako wa kazi yoyote .
3. Una penda nn?

haya uliyo muiliza yana uhusiano gani na na hiyo hela yake?. mia
 
haya uliyo muiliza yana uhusiano gani na na hiyo hela yake?. mia

vinahusiana kwa vile ana pesa (mtaji) lakini hajui cha kufanya sasa ili kumshauri idea ya biashara kuna vitu inabidi kuvijua kutoka kwake.
 
habari wana jf mimi n kijana ambae nafanya kaz kwa m2 inayoningizia elfu 5 au 4 kwa siku ila nataka nianze kivyangu nikiwa na sh lak 3 msaada please




Kilimanjaro, mbege vipi? Uza mbege na makande ili watu wakilewa wale chakula chako si lazimawaende nyumbani. Wale hapo hapo.
 
Mimi nakushauri kaka funguwa genge lina faida sana na utakuja kuniyambia

'mwajuma ndala ndefu,asha ngedere,chausiku na kina cheupe dawa ndo muflisi wa biashara kama hizi asee,heh heh'
 
Njoo hapa nikuambie. Jaribu hii:

kufuga kuku wa kienyeji;

mchanganuo:
-Tsh.60k kwaajili ya kujenga/kuandaa banda, chakula na virutubisho vya kuku.
-Tsh.50k kwaajili ya kuku wa kuanzia. Usinunue kuku wakubwa, ni ghali sana na wanakua used/wametumika sana, nunua kuku wadogowadogo waliotoka tengana na mama yao sio muda. Kwa huku (ir) bei ni tsh.5,000 so hapo utanunua kama 10 hivi. Ila make sure una mix, majogoo mawili ni tosha kabisa, vongine vijike (tetea).
-najua vitu kama maji, mtu wa kuhudumia huna haja ya kuajili mtu. Wewe mwenyewe husika maana bado ndio unaanza.
-Hadi hapo unakua umetumia Tsh.110k tu. Nyimgine iliobaki weka kwaajili ya backup ya madawa, chakula, pesa ya kumlipa docta (hii muhimu sana, usiwe bahili kuwalipa wale jamaa, ata kama kuku zako ziko poa kiafya, muite azicheki tu, sio gharama, akija mara moja unaweza mtoa buku 3 hivi fresh)
-Kuku (hao madogo ulionunua ambao umri wao ni kama miezi 4 hivi) watachukua tena kama miezi 2 ili waanze kutaga au ata kuuza. Hapo pesa itaanza kuzunguka.

Baada ya hii stage, hujamaiza:

-unaweza anza na kufuga kuku wa mayai, wale ambao hawaatamii mayai. Hapa utaanza pata mayai na kuyauza. Hivyo utakua unapiga pesa kwenye mayai na kuku.
-Unaweza pia ukanunua na zile mashine za kutotoleshea vifaranga(bei zake ni kama 80k hivi, ila lazima kuwe na umeme unapokaa).

Hitimisho;
-ukianza leo najua baada ya muda kama wa miezi 8 unaanza kupiga hela ya mayai na nyama.

Pesa ulionayo sasa (laki 3) usijidanganye ukaanzisha duka, genge, au biashara za uchuuzi wa mazao au vitu toka mjini upeleke kijijini. Hizo waachie wenye pesa ndefu, ambao ata shoti (hasara) ya laki 5 ikitokea hawayumbi. Wewe hapo ukipoteza/ukipata hasara ya laki 1 tu, kuirudisha daah itachukua muda.

Thanks.

Ila ukitoka kaka nikumbuke, mwenyewe hali mbaya hapa.

'ee bwana mkuu are you serious kaka hiyo incubator ya 80k naeza pata wapi mkuu na inachukua vifaranga wangapi na kwa mda gani mkuu,manual au automatic ndugu'
 
'ee bwana mkuu are you serious kaka hiyo incubator ya 80k naeza pata wapi mkuu na inachukua vifaranga wangapi na kwa mda gani mkuu,manual au automatic ndugu'

ushauri mzuri huu, ila angalau ktk lak 3 hiyo, ungemlipa angalau alf 20 huyu mshauri, ni sehemu ya gharama za mradi
 
Ushauri mzuri sana umetolewa na mkuu Secret Service, mi hapa nina shs laki saba cash! Mchanganuo alioutoa bwana mkubwa, nataka niutumie kumfumbua macho kaka yangu kule shamba! Namkabidhi mtaji huo kabisaaa!
Sitaki shida!
 
Last edited by a moderator:
'ee bwana mkuu are you serious kaka hiyo incubator ya 80k naeza pata wapi mkuu na inachukua vifaranga wangapi na kwa mda gani mkuu,manual au automatic ndugu'

hizi incubator jamani naombeni maelezo jinsi zinavyofanya kazi jamani!
Zinapatikana wapi? Viwango vyake vya utendaji kazi ukoje?
images
 
habari wana jf mimi n kijana ambae nafanya kaz kwa m2 inayoningizia elfu 5 au 4 kwa siku ila nataka nianze kivyangu nikiwa na sh lak 3 msaada please


Endelea kufanya kazi na akiba uliyonayo itumie kuanzisha biashara ndogo kama duka la bidhaa, kila mwezi utakuwa unaongeza mtaji ukipokea mshahara.

Kwa kuanzia kama huna mke usimwamini mtu, duka lako fungua asubuhi sana kwa mahitaji yale ya asubuhi majani ya chai na sukari na ufungue baada ya kazi saa 11 mpaka saa 2 usiku
 
Back
Top Bottom