Wiki iliyopita Alhamisi nilikuwa narudi maskani nikakutana na bidada kabeba jiko la mkaa kichwani na kiContainer mkononi papohapo akiwa kadaka dela lake(ile style yao ya kuyakusanya mkononi).Ikawa;-
Mimi:Mambo?
Yeyeπoa
Mimi:nikusaidie kubeba?
Yeye:Yani nimechoka we acha tu
Mimi:Hujajibu swali,nimeuliza nikusaidie kubeba?!
Yeye:sawa
Nikamsaidia ikafika mbele kidogo hapo kila mtu akawa anatawanyika njia yake nikampa jiko lake.Akauliza naishi wapi,nkamwambia hapo mbele tu.Mara mkeo yupo?πDah nkaona hii kali nkamwambia sijaoa,sasa ile time nafikiria labda niombe namba Manzi akaniuliza namba yako ni 07 ngapi mbeleπnkaona kishaumana nikamtajia fresh tukaachana pale.
Ikapita io siku hakunitafuta me nikawa nimetulia.Kesho yake napita pale Nyerere Bridge ikajiona ikanisimamisha et namba yako cp mbona naitafuta inazingua,nikadhani labda alikosea kuandika kwahiyo nikaanda mwenyewe kwenye simu yake nikampa na hiyo siku pia kimya.
Zimepita siku kama tatu au nne hv nikakutana nayo kitaa,yenyeweilikuwa mbele ikaniona ikanisubiri tena eti mbona namba yako siipati?,nikaandika yake kwangu nikampigia hapohapo.Anauliza kwahiyo nikutafute saa ngapi au utanitafuta saa ngapi?!πManzi anauliza hivo mkavu kichizi,Nikamwambia mida mida sahivi kuna mikakati nafatilia.Baadae yake night ikanitafuta kwa namba nyingine niipigie kwenye simu yake kwamba haina salioπMaongezi hata hayajafika sekunde 5 nikaskia mwenzio nina shida My pleaseππnikajua kwisha. Nikamwambia duniani kuna shida nyingi sasa yako ni ipi?!.Eti natakiwa niende kwenye msiba sijui wapi(nmesahau)na nauli 64000/= ila nnayo kidogo niongezee basiππnikamwambia sina mikakati imekaza na hela nilikuwa nayo
Sasa nikajiuliza huyu demu siku zote kakomaliza namba ili aniombe hiyo hela?,ina maana msiba haujaisha siku zite hizo..Mpaka sahivi haijajitafutaπ