Kwa niliyoyashuhudia katika Uchaguzi huu, Poleni viongozi wa Upinzani

Hii post inaonyesha kuwa uligundua watu hawakupigia kura upinzani! Watanzania siyo wajinga, na ukiamini kuwa wamepiga kura kwa ujinga basi usiwaombe kura zao.
Ujinga wao utadhihirika wakianza kulalamikia matendo ya walio wachaguwa.
 
Sio suala la kuwashawishi kwa maneno tu bali kwa kuwaletea wanamuziki ka kina diamond bure, kuwapa fedha buku tano, kuwatisha kupitia ujinga wao kuwa tutakuwa kama libya. Hiki ni kitu ambacho mtu mwenye akili hawezi kufanya ili kumshawishi mtu.
Mziki huwakusanya watu, mziki huwaleta watu pamoja zaidi hata siku ya mwisho parapanda litalia sasa wewe usiende ubaki pekeyako duniani
 
Kweli wewe ni matope
 
Ujinga wao utadhihirika wakianza kulalamikia matendo ya walio wachaguwa.
Uchaguzi siyo jambo jipya Tanzania kwa hiyo usidhani kuwa kweli watanzania ni wajinga kisi kuwa hawajui maana ya uchaguzi. Uwepo wa akina Lema, Sugu, Mdee, Zitto na wengineo wa upinzani kwenye mabunge yaliyopita ni maatokeo ya uchaguzi huu huu.
 
Sasa ni yapi uliyoyashuhudia mkuu, maana umeishia kuzungumzia na kulaumu kiujumla jumla tu bila ya kuyataja!

Unamlaumu Mwalimu Nyerere bure, miaka yote hiyo baada ya yeye kuondoka madarakani bado umhusishe na huu upuuzi unaoendelea sasa?

Hata hivyo, unasahau kwamba ni Mwalimu mwenyewe aliyefundisha waTanzania wajitambue na wawakatae viongozi wabovu. Leo wewe unatafuta umaarufu kwa kumtupia lawama bila hata ya kutambua mchango wake katika kumkomboa mwananchi wa kawaida kifikra ili aweze kupigania haki zake zinapoporwa na viongozi kama hawa wa leo.
 
Kweli kabisa ulichoongea mkuu,viongozi wa upinzani wanajitoa sana katika siasa lkn wananchi wanawavunja moyo
Unapo jitoa kuipigania haki ya mtanzania basi jua atakuachia wewe uipiganie haki yake huku yeye akiwa amesimama pembeni ,
usitegemee na wala usifikiri kuwa atakuja kuungana na wewe ili mpambane wote haki yake ipatikane , hivi ndivyo nilivyo wajua watanzania tangu tupate uhuru 1961.
 
Hii hoja yako ingekuwa na maana kama kungekuwa na mazingira saw a kati ya upinzani na chama tawala.upinzani wanafanyiwa kila aina ya uovu kupitia chama na nguvu ya serikali lakini wanaohangakiwa wapo wamelala usingizi wa pono.

Hapa neno ujinga nimetumia kupunguza ukali wa maneno,neno sahihi sio kuwa sisi ni wajinga bali ni wapumbavu na matahira.
 
Lisu asipokua Rais sioni haja ya kufanya uchaguzi tena kwa ngazi ya urais mambo yatajirudia yaleyale Bora hela za uchaguzi tufanyie mambo mengine CCM waendelee kubaki madarakani tu huku vyama vya upinzani vijiandae vizuri ili kuhakikisha siku ya kubali kufanya uchaguzi wanajua na kila mbinu ya kuiondoa CCM madarakani , mambo yanakatisha tamaa kabisa
 
Kweli wewe ni matope
Kabisa matope yale meusi tiii,,
2015 nilikuwa karai la kubenea
Kapiga hela zake bungeni katimkia ACT
Kiinua mgongo chake kabeba yupo poa
Mm nilikaa kituo cha kupigia kura kuanzia asubuhi saa 2 mbaka saa 7 ndio napiga kura alafu faida sijaiona kabisa ya kukaa foleni pale badala yake naona waheshimiwa wabunge wamekula bata tu bungeni kwa style ya zomea zomea
Pumbaff mwaka huu nimegoma kuwa karai
 
Amsterdam out
 
Kwanini tunakata tamaa?
Tujiandae kupinga matokeo kwa namna zote kwa kuwa tuna ushahidi tayari wa kutosha wa mambo kwenda hovyo
 
Hii post inaonyesha kuwa uligundua watu hawakupigia kura upinzani! Watanzania siyo wajinga, na ukiamini kuwa wamepiga kura kwa ujinga basi usiwaombe kura zao.
Hivi wewe shule ulikwenda kusoma au kunywa uji,hapa sizungumzii watu kutowapigia kura upinzani bali dhuruma za wazi wanazpfanyiwa kama kutowaruhusu mawakala,wizi wa kura,unyasasaji,kutopewa fomu,kutolewa nje na mambo mengine mengi.

Lengo likiwa ni kuidhinisha ushindi mchafu dhidi ya wagombea wa upinzani.
 
Hivi mkuu..ulikaa kabisa ukadhani lisu anaweza kuwa Rais au unatania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…