Kwa nini post za nje ikihusisha Tz inapata engagement kubwa kubwa ya wabongo mitandaoni kuliko nchi nyingine za Afrika ?

Kwa nini post za nje ikihusisha Tz inapata engagement kubwa kubwa ya wabongo mitandaoni kuliko nchi nyingine za Afrika ?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja ..

Hili nimefuatilia sana ;

1. Kipindi Samata kajiunga Aston Villa , page ya Aston Villa ilijaa wabongo mpaka na aliponyimwa pasi wabongo walimshambulia sana Grealish

2 . Aziz Ki ; alipojiunga Wydad page ya Wydad waarabu walikimbia walijaa wabongo kupiga stori na kumtaka Admin ampost Aziz wa kwanza kwenye picha . Pacome alivyoitwa timu ya Taifa pia ile page ilikuwa mpaka wenyewe wanajiuliza jamaa mbongo au ?

3. Page ya CAF content za Simba na Yanga ndizo zinaReaction na engagement kubwa kuliko vilabu vingine vyovyote .

4. Watu wa nje (Wazungu , Thailand nk ) wakipiga Content inayohusu bongo Hilo nyomi balaa , na sasa wanapiga sana mpaka za kuongea kiswahili.

5. Mamelodi hawasahau kipindi wanacheza na Yanga jinsi page yao ilivyovamiwa na mashabiki wa bongo mpaka wakaamini kabisa bongo wana mashabiki wengi sana .

6. Mambo ya Miss grand wabongo walikichafua sana mitandao kisa kumpambania mwenzao .

Hata juzi Liverpool walijaribu kupost caption ya Kiswahili hawakuamini hizo comments na reactions , post hiyo ndio iliTrend zaidi kuliko zote
IMG_20261024_194824.jpg

Mfano ipi mingi sana wakuu ukipita ukiwa mtu wa mitandaoni utaona .

Je , wabongo ndio tunaongoza kwa Matumizi ya mitandao ya kijamii kuliko nchi nyingi Afrika , wakarimu au tunapenda sana vya kwetu ?

Yapi maoni yako ?

#UziTayari
 
Sasa sie waswahili kwa shughuli, sherehe, mihemko na umbea, na furaha bandia ndiyo zetu.
Huku nyumbani hali mbaya hatupumui.
Ukiongea mambo ya msingi au siasa unayeyuka mfano wa barafu huonekani tena mitaani.
Mitandaoni tunatafuta furaha ya muda ya bandia kupunguza fukuto la magumu tunayo pitia.
Hatutaki kazi wala mambo magumu ya sayansi na teknolojia.
 
Naunga mkono hoja
 
Hii nchi tunapenda kufatilia vitu ambavyo sio serious kwenye maisha

Ila mambo serius Kama uchumi na siasa ni zero.

Ukisema Samia kajinyea au Lissu kamkojolea mtu utapata engagement kubwa sana kuliko kusema Kwanini Tundu Lissu anasingiziwa kesi za uongo ??.

Udaku na umbea ndio tunafatilia Sana

Ata mange alipata umaarufu kupitia udaku baada ya kupata wafuasi ndio akarudi kwenye siasa

Hii nchi ukitaka trend tengeneza content zisizo na maana kwenye jamii.
 
Back
Top Bottom