Kwa njia za kawaida, uwezo huo hauna. Ila kiheshima, eti unao….

Juzi hapa Rais wenu kapewa tena udaktari wa heshima huko India.
Anastahili
Tayari sasa katika utambulisho wake, watu wameshaanza kumwita eti Dr. Samia Suluhu Hassan.
Hili kweli is not right, PhD za honoria causa, hazibadili title ya mtu kuitwa Dr!. Mwalimu Nyerere alipewa na hakuitwa Dr, Ali Hassan Mwinyi alipewa na hakuitwa Dr. Benjamin Mkapa alipewa na hakuitwa Dr. Jakaya Kikwete alipewa na akaitwa Dr, sasa kama JK aliitwa Dr kwa PhD ya honoria causa, na hatukusema wala kupinga, now Mama kapewa, why sasa ndio tunasema na tunapinga?.
Tuiombe TCU ilifafanue hili, nakuikumbuka vizuri hoja ya Prof. Kironde.
Naye kwa kupenda ujiko, hata hagomi kuitwa hivyo.
Usikute sio yeye, au usikute...
ila kwa vile JK aliitwa na hakugoma, why not her?.

Sisi washauri wa bure, tumeikubali hii title ni well befitting her na tumeshauri Baada ya kutunukiwa PhD na kuwa Dkt. mnaonaje jina la "Mama" sasa tukaachana nalo ila Nyumbani wanaweza kuendelea kumuita Mama?
P
 
Wivu na chuki binafsi 😂😂😂😂

Wewe Hadi unakufa hutokaa upewe heshima ya hivyo,ukiweza somea ila hizo status ni Kwa watu maalumu tuu
Wewe vipi Utaweza kupewa?! Manake umekazana kutetea degree za kijinga.
 
“I’d like to differs”. Umeanza kwa kuandika hivyo.

I have never taken you seriously. You’ve 100% turned into a Samia shill.

That’s why most of the time I don’t even bother responding to your foolishness.

You rarely make sense. You’re long winded.

I don’t remember a time when you made any cogent argument.

Weirdo.
 
Dkt Joseph Kasheku alivyoshiriki kufutilia mbali Bandari ya DSM mikononi ya watanzania na kupewa DPw. Akiwa tayari anajiita Dkt Musukuma alienda Dubai na wenzake. Ni katika safari hiyo deal la DPw ilikamilika na yeye akawa mtetezi wa hao waarabu mwanzo mwisho.
Hadi hapo nguvu ya degrees za mtaani tumeshuhudia waziwazi
 
Hata mimi nashangaa, eti barabara ya mtaa wameita kwa jina langu.
 
Kwa kawaida, vilaza huwa wakipewa sifa fake za kuwakweza kama kuitwa dr, prof. huwa wanafuraaahi balaa!.
 
Kuna watu Tanzania tumewashudia, wana PhD lakini wakiongea Kingereza ni kichefuchefu.

Hamuwajui PhD za mchongo?
 
Ule ujinga ujinga wa awamu ya nne umerejea kwa kasi awamu ya mchongo ya sita.

Awamu ya nne tulikuwa na rizimoko sasa hivi ni Abdul.
 
Kwa Uandishi huu tuna safari ndefu sana huko tuendako ili kufikia matarajio ya walio wengi na wenye maono yenye tija. hebu soma tena ulichoandika na namna ulivyoandika kisha jitafakari kama upo katika jukwaa sahihi kujadili mambo na watu sahihi na hatimaye kupata dira tuitakayo.
Tanzania inabidi ianze upya vita ya kupambana na maadui watatu ambao Mwalimu Nyerere aliwabainisha Ujinga, Maradhi na Umaskini.
 
Kama kawaida Chawa unarudisha mashambulizi.
Badala ya kujenga hoja kinzani au kutetea jambo husika CHAWA hukimbilia kwenye neno WIVU. Na naamini kwa hakika hata maana ya neno wivu huwa hawaijui na muktadha na matumizi yake. Umuonee wivu Rais wakati hujawahi kuwa na ndoto za kugombea Urais, wanasahau Rais sio mali ya mtu binafsi ni mali ya Umma, Hivyo umma una haki ya kujadili kuhusu mambo na mawenendo unamhusu Rais wa nchi iwe ameteuliwa au amechaguliwa. Bado maaduli wa maendeleo aliyowainisha Mwalimu Nyerere Ujinga Maradhi na Umaskini tunao. KUPAMBANA NA CHAWA NI KIPAJI MKUU
 

..Maza alitakiwa awe muungwana kwa kukataa kuitwa Dr.

..Wanaoitwa Dr ktk mazingira ya kawaida ni Madaktari wanaouguza hospitalini.

..Wenye shahada za Uzamifu / PhD huitwa Dr wakiwa miongoni mwa wanataaluma wenzao ktk shughuli zao za kitaalamu. Wakiwa ktk shughuli nyingine yoyote ile hawatumii utambulisho huo.
 
Chuo cha Kihindi kikupe udaktari wa heshima kwa jambo la kutunga la kijingajinga, sasa hiyo si aibu jamani? Kwanza huo udaktari wa mchongo ni kama rushwa.
 
 
Excellent
 
Sio kweli, tuambie hawezi kwa sababu zipi na Kwa vigezo vipi? PhD hiyo si kapewa na chuo, tena na maprofesa kwa hiyari yao!

Tuanamsakama Rais kama vile amekiomba au amekilazizisha au amekishurutisha hicho chuo kimtunuku hiyo PhD.

Kapewa kama walivyopewa waliomtangulia. Kama ni kulaumu wakulaumiwa ni hicho chuo sio Rais samia.

Sioni mantiki ya kusema asiitike, kwani kapewa ya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…