Kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma Makao Makuu, wote imekuwa ni njia moja Dar

Mkuu kwa mtazamo wangu mm huyu mama hawezi kua rais bora kabisa kwa kifupi mm smukubali hata kidogo nimejipa mda ili nijirizishe kwanza na utendaji wake.
Akheri yako bado unampa muda; mimi naelekea ukingoni kutegemea lolote la maana kwa nchi yetu katika miaka yake hii minne.
 
Kwani magufuli alikukataza kuitafuta acha uoga
 
Bwana yule alikua anaenda Sana chato mbona mawaziri wake hawakuiga kwenda huko kitovuni?
Si ajabu, baadhi yao (mawaziri), walianza kutafuta viwanja Chato, wakiamini makao makuu yatahamia huko!
Waziri wa utalii huenda hata msingi wa nyumba yake alishajenga huko!
 
Aliyefikiria ni Julius Nyerere waliofuata walikuwa hawana mapenzi na watanzania. Akaja aliyezaliwa huko kijijini akatekeleza, ameondoka bahati mbaya sana na funguo za Ikulu ndio maana kila wakiingia wanaona mauzauza. Wataikwepa Ikuklu ya Chamwino lakini ndiko angalau funguo za kuchonga zinaweza kutengenezwa na kazi ikaendelea. Kaacha barabara nyingi za mitaa iliyokuwa ya kienyeji lakini zimetandikwa barabara za zege (Mfano Mazense, Magomeni, Vingunguti, Kigogo, Sinza, Mwananyamala, Kinondoni nk)
 
Hizi kelele za katiba ni kutafutia watu ulaji tu ili hiyo katiba wanayoitaka ilazimishe nao wateuliwe kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya pia wawe mawaziri hamna kingine na kabisa wapo nje ya uwanja ndio kabisa njaa imewapiga kweli kweli, hizo ni drama tu na kutuvurugia amani yetu tuwaapuuze na tuchape kazi.
 

..siyo kweli.

..moja kati ya mapendekezo ya katiba mpya ni kuondolewa kwa nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya.
 
Unaongea mambo theoretical zaidi ambayo ndiyo mwanzo wa false expectations. Ni kweli wananchi ndio waliowaweka viongozi madarakani, lakini walifanya hivyo wakati wa uchaguzi. Wananchi hawana power ya kumwambia kiongozi kuwa umefanya makosa tunakufukuza kazi na tunaajiri kiongozi mwingine kirahisi namna hiyo. Itabidi wasubiuri uchaguzi mwingine (miaka mitano ijayo).

Uingereza hawana katiba lakini serikali inafuata sheria. Hilo ndilo swala la kujiuliza, je sheria tunazoijiwekea zinafuatwa na serikali? ndiyo maana nikasema katiba ni kitu kimoja, na utekelezaji wake ni kitu tofauti. Usimamizi wa sheria ni kazi ya serikali. Sasa hivi sheria inasema makao makuu ya serikali ni Dodoma, kwa serikali isiitekeleze sheria hiyo kama ilivyo? katiba mpya itasaidia nini kwa serikali kutimiza jukumu lake la kusimamia sheria?

Kwa hiyo wewe hujui kuwa Trump alichochea watu kubomboa ofisi za bunge, ambalo siyo tu kuwa ni kosa la jinai lakini pia ni kinyume katiba ya marekani inayotenganisha Article 1 na Article 2. Vile vile hutambui kuwa wakati wa utawala wa Trump safari zote za jeshi la marekani kuelekea Ujerumani zilikuwa zinalazimishwa kulala Scotland kwenye hotel za Trump ambayo ni kinyume cha Katiba. Vile vile huelewei kuwa Pence alipokwenda safari ya kikazi huko Ireland alilazimika kulala hoteli ya Trump kinyume cha katiba. Kuna msululu mrefu wa mambo ya uvunjaji wa katiba na sheria yaliyofanywa ambayo bado yanashhughulikiwa. Trump aliondolewa madarakani baada ya miaka minne kwa njia ya uchaguzi uliofuata.
 
Baada ya kuyaona yote haya, na wananchi wakaona upuuzi wakamwondoa kwenye uongozi, bado huoni kwamba sheria zao zinafanya kazi, ikiwa ni pamoja na katiba yao?
Baada ya kukariri yote hayo aliyokuwa akifanya Trump, bado unashindwa kutambua kwamba alikuwa 'impeached', tena mara mbili?

Katiba yao haiweki madaraka yote kwa mtu huyo mmoja kiasi cha mtu huyo ndiye aamue kila kitu na hawezi kuwajibishwa, hili hulioni? Trump hata leo anaweza kufikishwa mahakamani kwa makosa aliyofanya akiwa rais, hilo halina maana kwako?
Sasa angalia mfano kama huu ulioweka hapa, sijui unataka kueleza kitu gani katika kutetea hoja yako, kama siyo kuipinga moja kwa moja bila kutambua kuwa unajipinga mwenyewe.
Huko Uingereza kuna kitu gani kinachowafanya viongozi wa huko watii sheria wanazojitungia, ambacho sisi hapa hatuna?
Una maana kwa vile hapa viongozi hawafuati hizo sheria zinazotungwa, tuache kuhimiza sheria zisifuatwe na kutafuta njia za kuwafanya wafuate hizo sheria, ikiwa ni pamoja na kuondoa udhaifu uliomo kwenye hizo sheria ili ziwabane zaidi wasiweze kuzikiuka?
 
Labda wanamjaribu mama, au dodoma hawapapendi.
 
We kiboko kweli, umemmiss nani!
Mtu anakufanya uishi kama mtumwa ndani ya nchi yako mwenyewe, wewe unammiss! Fimbo ni kwa mgongo wa mpumbavu"

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Asante elimu nzuri mkuu.
 
Hapo sasa ndo mana nikasema huwez elewa nilichoandika..
Unasema wananchi hawana utambuzi wakati mm nazungumzia utambuzi kwa wenye madaraka..Farewell bro...
 
Viongozi bakini huko huko Dodoma huku Dar mnafuata nini??
 
Kweli ee!
 
Sasha miaka yake 5 kisha itakua vizuri awapishe wanamapinduzi kuendesha nchi kimagufuli. Bila hivyo mafanikio yote yatapotea.
 
Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifanyuka bila upembuzi yakinifu.
Ila sasa ndio tushahamia. Vigogo wasiturudishe dar. Ni suala la rais tu kua mkali na kua mfano yeye mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…