Wow, well narrated, nimependa ulivyo shuka kuanzia kichwa nini la msingi na hitimisho.
Nitalifanyia kazi kuhusu mpangilio na kuhusu south korea pia nimeeleza japo nimejumuisha kwa ujumla na kuto chambua kitu kimoja baada ya kingine.
Kuhusu swala la wasomi na wenye ujuzi wa mambo baadhi ya kulisaidia taifa nilishawahi lifikisha sehemu muitikio ulikuwepo tatizo ni namna ya kuliwasilisha kutokana na mambo yanavyo enda kwa sasa watanzania tukiweza muda kwenye teknolojia na maendeleo waliopewa dhamana wangeweza onesha zaidi kwenye hayo maswala.
Tatizo ni kwamba nguvu yetu itakapo lalia kiongozi hana budi nae kuonesha nini watu wanataka waone lakini naimani itafika wakati watu watafunguka ila itakuwa muda umeshaenda japo tukiwahi tunaweza kuelekezea upepo huko kwenye mapinduzi ya kiuchumi.
Mkuu 'Rijali jandoni', nikushukuru tena kwa kuanzisha mada muhimu sana kama hii hapa JF.
Pamoja na kwamba sijui ngazi yako katika maisha, lakini inaonyesha wazi kwamba unao msimamo mzuri sana katika mstakabari mzima wa maisha ya wananchi wa nchi hii na heshima ya nchi yetu mbele ya mataifa mengine duniani.
Kama ulivyo eleza toka mwanzo, kwa jinsi Tanzania ilivyo jaaliwa; kwanza kwa kuwa hapo mahala ilipo kijografia, na kuwa na raslimali muhimu ilizo nazo; hii nchi siyo nchi ya kuwa maskini hata kidogo. Tatizo letu kubwa ni kukosa uongozi wenye dira wa kuliongoza hili taifa kufikia malengo katika muda stahiki. Mbaya zaidi, sasa hata yale malengo yaliyokuwepo awali ya kulisukuma taifa mbele kwa haraka nayo yanavurugwa tu bila fikra. Kila kkiongozi sasa anaye shika madaraka, anataka aanzishe mipango yake mipya ambayo haikupangiliwa italiongezea nini taifa hili katika juhudi za kwenda mbele. Akiondoka huyo, anaingia mwingine, na yeye anaanza kivyake!
Lakini, bila kutaka kuchosha wasomaji hapa: Tatizo kubwa zaidi linalo tukabili sisi kama wananchi, ni hizi fikra za kudhani kuna watu toka huko nje watakao kuja kuijenga Tanzania na kuleta maendeleo; kwa jina la uwekezaji. Hili haliwezekani kabisa. Hakuna muujiza kama huo unaoweza kutokea hapa.
Uwekezaji ni njia tu moja ya kutusaidia sisi wenyewe katika juhudi zetu sisi wenyewe za kujenga taifa letu kwa mipango yetu.
Kwa hiyo hakuna mbadala wa sisi wenyewe kujenga uwezo wetu wa kufanya mambo yetu ya maendeleo. Huo uwekezaji uwe nyenzo tu ya kujijengea uwezo kuyafanya mambo hayo.
Nitoe mfano rahisi hapa: Unakabidhi shughuli za bandari kwa mwekezaji, miaka 30, au hata zaidi; na kabla ya hapo ulikuwa umewapa wawekezaji wengine walikokaa hapo takribani, zaidi ya miaka 25!
Sasa niambie, hawa watu wako, waTanzania wana vichwa vya namna gani kutoweza kupata/kujifunza maswala ya kuendesha bandari kwa ufanisi miaka yote hiyo? Isitoshe, kabla hujaikodisha hiyo bandari, umekwenda kuchukua mikopo kuiboresha, halafu unamgawia mwekezaji apate faida, na wewe akugawie kidogo kitakacho patikana kama faida!
Na baada ya hiyo miaka thelathini, hadithi itakuwa ni hiyo hiyo, kwamba waTanzania hawawezi kuendesha bandari, na mzunguko mpya utaendelea kutafuta wawekezaji (wawekezaji, wamewekeza nini hasa?)
Huu ni mfano mmoja tu, unao wakilisha mifano chungu nzima ya jinsi tusivyo kuwa na fikra za kuiendeleza Tanzania.
Katika yote niliyo eleza humu, ni maneno machache tu yanayoweza kuwasilisha yote hayo.
WaTanzania ni lazima tujiamini kuwa tunao uwezo wa kujiendeleza wenyewe. Tuwe na uthubutu wa kufanya mambo sisi wenyewe. Tusipo kuwa na uwezo, tutafute msaada, lakini msaada huo iwe njia ya kujijengea uwezo sisi wenyewe.
Nakusihi sana usikose kufuatilia juhudi za waKorea wa Kusini, na nchi nyinginezo katika eneo hilo kujuwa walicho weza kufanya na kupata mabadiliko makubwa katika muda mfupi.