Kwa sera za namna hii, Tanzania inaweza badilisha hali yake ya kiuchumi na kuwa taifa imara ukanda wa Kusini mwa Afrika ama inahtaji mageuzi zaidi?

Kwa sera za namna hii, Tanzania inaweza badilisha hali yake ya kiuchumi na kuwa taifa imara ukanda wa Kusini mwa Afrika ama inahtaji mageuzi zaidi?

Mkuu umemaliza kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu ccm .
Kwa kila mtu ana haki ya kusema analo ona ni sawa lakini kwa namna hali ilivyo je hata wengine wakipata nafasi wanaweza kulifikisha taifa sehemu tunayo dhani linaweza fika?
Nadhani haya tunayo hitaji ni zaidi ya hili wana jamii
 
Uchumi unapoelekea anajua alie juu tu walai!
Mahondow Kama jambo lipo sawa ni vizuri kulisema, kama uchumi wa watu wa chini una mashaka inawezekana pia kutoa namna ya mambo yafanyike ili kunusuru, alipo yeye au wao mpaka kujua na kuelewa hali za wa chini ni ngumu mno.

Na ni ngumu kubadilisha hali ya watanzania wote kuwa sawa, ila inawezekana kubadili mfumo wa vitu vinavyo wakutanisha watanzania hata wa chini akipata changamoto basi anapoingia sehemu za uma ana ona afadhali mfano hospitalini, kwenye usafiri, na mengine ya kijamii.
 
Kwa kila mtu ana haki ya kusema analo ona ni sawa lakini kwa namna hali ilivyo je hata wengine wakipata nafasi wanaweza kulifikisha taifa sehemu tunayo dhani linaweza fika?
Nadhani haya tunayo hitaji ni zaidi ya hili wana jamii
Mkuu naheshimu sana andiko lako na ni nzuri
Lakini ukweli ni huu maandiko na mawazo mazuri kama haya ya kwako serikali wanayo lakini wameyafungia kwenye makabati

Maendeleo tuliyonayo na rasilimali tulizonazo haviendani
Ccm imekuwa ni chama wizi ruswa na ufisadi na kwenye mambo haya hamuwezi kuwa na maendeleo
 
Shukrani sana nikweli kabisa Benny Haraba huenda wapo wa namna hiyo lakini yakijadiliwa nadhani haitoweza kutokea viongozi wa namna hiyo
90% ya viongozi wetu Wana sera binfasi na sio ya Nchi , ndio maana wanawafundisha kila mtu awe mla rushwa , injinia, Daktari, Mwalimu, polisi NK NK
 
Mahondow Kama jambo lipo sawa ni vizuri kulisema, kama uchumi wa watu wa chini una mashaka inawezekana pia kutoa namna ya mambo yafanyike ili kunusuru, alipo yeye au wao mpaka kujua na kuelewa hali za wa chini ni ngumu mno.

Na ni ngumu kubadilisha hali ya watanzania wote kuwa sawa, ila inawezekana kubadili mfumo wa vitu vinavyo wakutanisha watanzania hata wa chini akipata changamoto basi anapoingia sehemu za uma ana ona afadhali mfano hospitalini, kwenye usafiri, na mengine ya kijamii.

Raia Kuubadili Mfumo ni kitu ambacho hakiwezekani!
Mfumo ni mpana sana wanaoweza ni walioushikilia tu

Cc Smart911
 
Mkuu naheshimu sana andiko lako na ni nzuri
Lakini ukweli ni huu maandiko na mawazo mazuri kama haya ya kwako serikali wanayo lakini wameyafungia kwenye makabati

Maendeleo tuliyonayo na rasilimali tulizonazo haviendani
Ccm imekuwa ni chama wizi ruswa na ufisadi na kwenye mambo haya hamuwezi kuwa na maendeleo
Shukrani sana, inawezekena ni kweli yapo lakini wenye nia ya kweli huenda ni wachache na hiyo kutokana wengi wetu hatuna uwezo wa kureasoning kiasi ambacho wenye nia na walio wengi wakaona kana kwamba hawapewi kesi naweza sema kuwa offended. Cha msingi wenye nia nzuri na wenye hayo mawazo wanabidi kuyagusia na kuyapeta juu taratibu kwa sababu namna mambo yanavyo enda duniani tukishangaa tutakuwa na maisha magumu sana
 
Nchi yenye demokrasia, hata demokrasia uchwara-haiwezi kuendelea.
Hili nilikuwa sitambui kwahiyo kwa maana hiyo nchi inayotaka kuendelea lazima iwe na sheria kama za Torati ama Msaafu kosa moja kubwa ni litakufanya uweke maisha yako rehani right?
 
90% ya viongozi wetu Wana sera binfasi na sio ya Nchi , ndio maana wanawafundisha kila mtu awe mla rushwa , injinia, Daktari, Mwalimu, polisi NK NK
Hili ni changamoto kama hali ni hii August, lakini naimani inawezekana kulitatua wapo viongozi bado wana uchungu na upendo kwa taifa ama?
 
Hili ni changamoto kama hali ni hii August, lakini naimani inawezekana kulitatua wapo viongozi bado wana uchungu na upendo kwa taifa ama?
Wapo lakini jinsi ya kupita katika msitu wa mafisi ndio shida, labda itoke tu kwa mapenzi yake Mungu au wananchi wajielewe
 
Wow, well narrated, nimependa ulivyo shuka kuanzia kichwa nini la msingi na hitimisho.

Nitalifanyia kazi kuhusu mpangilio na kuhusu south korea pia nimeeleza japo nimejumuisha kwa ujumla na kuto chambua kitu kimoja baada ya kingine.

Kuhusu swala la wasomi na wenye ujuzi wa mambo baadhi ya kulisaidia taifa nilishawahi lifikisha sehemu muitikio ulikuwepo tatizo ni namna ya kuliwasilisha kutokana na mambo yanavyo enda kwa sasa watanzania tukiweza muda kwenye teknolojia na maendeleo waliopewa dhamana wangeweza onesha zaidi kwenye hayo maswala.

Tatizo ni kwamba nguvu yetu itakapo lalia kiongozi hana budi nae kuonesha nini watu wanataka waone lakini naimani itafika wakati watu watafunguka ila itakuwa muda umeshaenda japo tukiwahi tunaweza kuelekezea upepo huko kwenye mapinduzi ya kiuchumi.
Mkuu 'Rijali jandoni', nikushukuru tena kwa kuanzisha mada muhimu sana kama hii hapa JF.
Pamoja na kwamba sijui ngazi yako katika maisha, lakini inaonyesha wazi kwamba unao msimamo mzuri sana katika mstakabari mzima wa maisha ya wananchi wa nchi hii na heshima ya nchi yetu mbele ya mataifa mengine duniani.

Kama ulivyo eleza toka mwanzo, kwa jinsi Tanzania ilivyo jaaliwa; kwanza kwa kuwa hapo mahala ilipo kijografia, na kuwa na raslimali muhimu ilizo nazo; hii nchi siyo nchi ya kuwa maskini hata kidogo. Tatizo letu kubwa ni kukosa uongozi wenye dira wa kuliongoza hili taifa kufikia malengo katika muda stahiki. Mbaya zaidi, sasa hata yale malengo yaliyokuwepo awali ya kulisukuma taifa mbele kwa haraka nayo yanavurugwa tu bila fikra. Kila kkiongozi sasa anaye shika madaraka, anataka aanzishe mipango yake mipya ambayo haikupangiliwa italiongezea nini taifa hili katika juhudi za kwenda mbele. Akiondoka huyo, anaingia mwingine, na yeye anaanza kivyake!

Lakini, bila kutaka kuchosha wasomaji hapa: Tatizo kubwa zaidi linalo tukabili sisi kama wananchi, ni hizi fikra za kudhani kuna watu toka huko nje watakao kuja kuijenga Tanzania na kuleta maendeleo; kwa jina la uwekezaji. Hili haliwezekani kabisa. Hakuna muujiza kama huo unaoweza kutokea hapa.
Uwekezaji ni njia tu moja ya kutusaidia sisi wenyewe katika juhudi zetu sisi wenyewe za kujenga taifa letu kwa mipango yetu.
Kwa hiyo hakuna mbadala wa sisi wenyewe kujenga uwezo wetu wa kufanya mambo yetu ya maendeleo. Huo uwekezaji uwe nyenzo tu ya kujijengea uwezo kuyafanya mambo hayo.
Nitoe mfano rahisi hapa: Unakabidhi shughuli za bandari kwa mwekezaji, miaka 30, au hata zaidi; na kabla ya hapo ulikuwa umewapa wawekezaji wengine walikokaa hapo takribani, zaidi ya miaka 25!
Sasa niambie, hawa watu wako, waTanzania wana vichwa vya namna gani kutoweza kupata/kujifunza maswala ya kuendesha bandari kwa ufanisi miaka yote hiyo? Isitoshe, kabla hujaikodisha hiyo bandari, umekwenda kuchukua mikopo kuiboresha, halafu unamgawia mwekezaji apate faida, na wewe akugawie kidogo kitakacho patikana kama faida!
Na baada ya hiyo miaka thelathini, hadithi itakuwa ni hiyo hiyo, kwamba waTanzania hawawezi kuendesha bandari, na mzunguko mpya utaendelea kutafuta wawekezaji (wawekezaji, wamewekeza nini hasa?)

Huu ni mfano mmoja tu, unao wakilisha mifano chungu nzima ya jinsi tusivyo kuwa na fikra za kuiendeleza Tanzania.

Katika yote niliyo eleza humu, ni maneno machache tu yanayoweza kuwasilisha yote hayo.
WaTanzania ni lazima tujiamini kuwa tunao uwezo wa kujiendeleza wenyewe. Tuwe na uthubutu wa kufanya mambo sisi wenyewe. Tusipo kuwa na uwezo, tutafute msaada, lakini msaada huo iwe njia ya kujijengea uwezo sisi wenyewe.

Nakusihi sana usikose kufuatilia juhudi za waKorea wa Kusini, na nchi nyinginezo katika eneo hilo kujuwa walicho weza kufanya na kupata mabadiliko makubwa katika muda mfupi.
 
Mada nzuri Sana hii, kwa kuongeza at least kwa upande Wangu, hasa hapo kwenye Human capital, nashauri shule zetu zibadilishwe kabisa (total reform) kutoka kwenye ufaulu Hadi kwenye skills development!

Wakati nasoma primary, I think darasa la TATU au la nne, tayari nilikua na tuta la spinach, mchicha n.k. Kaka Zangu walikua na mabanda ya sungura, Kaka Yangu mmojawapo alikuja kutengeneza Banda zuri Sana la Kuku!

Tulikua na mafundi -technicians wazuri Sana WA kidato cha nne..... Leo hamna kitu
Tume ichezea sana ellimu yetu, na sasa inatugharimu sana kama taifa.
Matatizo yetu mengi sana yanaanzia huko kwenye elimu mbovu wananchi wetu wanayo ipata.
 
Kwani ukiwa hauna demokrasia ndiyo unakua hivyo?
Hapana kukosa demokrasia sio lazima kufanya hivyo, lakini kwa mifumo ya namna hiyo kuhukumu na kutoa adhabu pasipo kuzunguka huwa inafanyika hasa nchi zenye mifumo ya kifalme, kuendeshwa na dini moja ama chama kimoja.

Sasa kwako wewe kuandika ynayojiri nibkwa sababu ya demokrasia nilihitaji kuelewa kwa namna ya sheria kali ziwekwe ili kusaidia nchi kuwa katika mstari ulio nyooka zaidi, lakini hii sio mada sahihi hapa kutokana na namna tulivyo
 
Tatizo kubwa zaidi linalo tukabili sisi kama wananchi, ni hizi fikra za kudhani kuna watu toka huko nje watakao kuja kuijenga Tanzania na kuleta maendeleo;
Kalamu ahsante sana nime quote hiki kipande, ni kweli kuna muda tunatafuta wawekezaji wakubwa na tuna watamani tatizo lina angukia pale kwenye point yako ya rasilimali watu, wawekezaji wa ndani wakipewa mazingira mazuri wanaelewa soko letu kwa uzuri na undani.

Mfano kuna nchi ya Asia kabla ya wao kuwekeza na kutumia magari waliendesha sana baiskeli miaka ya 80's na 90's na hii ndio ilikuwa Era yao wananchi wakainuka na hiyo ikachangia hata viwanda vyao vya ndani kuendana na uhitaji wa watu wao maana wamiliki wengi walikuwa wazawa hapa tunavyo ongea ni nchi huenda inayo ongoza kwa utengenezaji wa magari ya kisasa na electric cars yaani yenye mfumo wa umeme.

Hili lifanyike kwetu pia tuanze na ambacho tuna kimudu kama ni pikipiki basi zitengenezwe bei iwe nusu ya sasa ama hata chini zaidi kwa watumiaji wa ndani, huo wakati utatumika utaisha tutaenda wa bajaji, then magari, ila tukija kwenye magari ya kuundwa na kuungwa hapa lakini kila kitu kinatoka nnje ni hatua nzuri lakini bei itakuwa haina tofauti na kuagiza hapo tutakuwa tunaua nguvu kazi iliowekwa na sera zitaonekana si nzuri kwa watu wanaokuja kuwekeza.

Kama nia ya kweli ipo basi wakae na wajasiriamali na wafanya biashara wakubwa wazawa kama ni kiwanda kiwe kina chambua kuchakata mpaka kuunda hapa hapa.

Kiwanda sio lazima kiwe na ukuta mrefu na mpana moshi kila upande hapana tulenge uzalishaji utakao punguza bei za ndani na kuchochea mauzo ya nnje kwa nchi za afrika tuu sio ulayaa yaani hela ikiwa na nguvu ndani inatosha
 
Back
Top Bottom