Swali zuri sana..... nami naomba kujibu kama ifuatavyo, ndoa sio tendo la ndoa tu, sasa ukiacha tendo la ndoa yapo yafuatayo:
1. Ulinzi wa mali zako, mwanamke aliye mke wako atajitahidi kulinda mali zako huku akifikiria kuna kesho maana yake anawaza future ya maisha yenu, wengi wakiambiwa kuna kesho huwa wanawaza labda kufa, hata usipokuwa kesho inakuja.
2. Anakupatia watoto, hii unaweza sema aah! nitazaa huko nje, mke akizaa anakuwa na kiu ya kuongeza uzao wako na anawatunza watoto kwa mapenzi yote kwa sababu anajua mume wake uko pembeni, kumbuka kuzaa sio kazi, kazi kulea mwana.
3. Mwanamke ataunganisha familia, kiuhalisia kuna familia ndugu hawaelewani, uwepo wa mke anakuwa mtu kati(mediator) na hapa upate mke sahihi wengine wanakuja kugombanisha.
4. Mke ni msaidizi wa mwanaume, na hapa sio usaidizi wa kazi za ndani noo, ni kumsaidia mwanaume kutimiza malengo yake, kumbuka malengo ya mwanaume ndo huwa malengo na msimamo wa familia, mwanamke hawezi kuja na ya kwake lazima atasimama na kumsupport mume, kumbuka hakuna mwanamke atapenda kusemwa kwamba hapo shost ulikosea kuchagua, kwahiyo hata kama mwanaume hayuko njema kiuchumi, atasaidiwa, tuna mifano kuna wanaume hata mahari walisaidiwa na wake zao.
5. Mke anakuletea Heshima katika jamii, sio heshima tu na kuaminika, kuna nyumba ukienda kupanga hujaoa au kuolewa huruhusiwi kwanini unaonekana huna heshima, huwezi kuwa Raisi wa nchi hii hujaoa, ukiachana Katoliki mengine huwezi kuwa Askofu hujaoa: Kiufupi kama haujaoa au kuolewa unawekwa kundi la wahuni, kama ndugu zangu kataa ndoa