Kwa tabiri hizi, CCM tukiendelea kumchekea Rais Samia soon tutageuka kuwa wapinzani!

Huku sasa ndio tunaita " connecting the dots" na "kufikiri nnje ya box".
Kuna vitu vinafikirika vyema.
Kongole.
 
Ndiyo!
 
Aisee,kuna harufu ya kwenda kutimia kwa tabiri hizi,Mungu saidia
 
Umeeleza vyema.

2024/2025 Kuna mabadiliko ya kimfumo.
 
Ccm wanajali sana Madaraka kuliko Maendeleo ya hii nchi, hii ni kitu imenifanya nizichukie Rangi za Kijani na Njano tangu niko Nursery maana sikua najua saana siasa ila Rangi za vyama.
 
Stori yako ndefu iliharibikia hapa.

Samia anakabidhi 2025; haendi mbali zaidi ya hapo.
 
Kumekucha !
Hujamwelewa huyu 'desperate'; yeye anasema msubiri Hichilema wenu baada ya 2030!

Naona huyu jamaa ni kama kapungukiwa kidogo! Au kwa vile kajitambulisha kuwa yeye ni hao hao CCM?

Nani atasubiri hadi huko 2030 huku nchi ikiendelea kuvurugika chini ya Samia?
 
Uwe na dabu. Ina maanaa hutakiki mimi baba yenu nichangie? Kwanini useme wana wema kama kwamba wote ni wana. Mie ni baba wa nyote. Hivyo, nipe heshima yangu. Unataka tuwe wapinzani mara ngapi wakati tushachuuzwa. Heri tungeuzwa. Tumechuuzwa na kusalitiwa ile mbaya. Hata hivyo, ukweli useme. Watendaji wazalendo waliokuwa wakiendesha bandari nao ni wezi tu. Kinachopaswa kufanya ni kuwakamata na ku-audit mali zao ili tuone nini cha kuwafanyia hawa wezi uchwara.
 
Mkuu kama ni unabii tu;-

Nabii Boniface victor anatabiri ccm itaendelea kutawala daima,na Rais anaefuata baada ya samiah ni Gwajima josephati sasa sijui tushike lipi!!!

Mi nadhani tuendelee kufanya kazi KWA bidii huku tukiomba amani iendelee kutawala nchini!!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yangu niipendayo SANA!!
 
Kuweni macho kabla utabiri wa Nyerere nao kutimia, "Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM".
Hapa unaweza kuwa umeshika penyewe, lakini picha bado ni mbovu sana, haionyeshi ni akina nani huko CCM wanaoweza kutimiza ubashiri huu.
Laiti pangekuwepo na watu wawili au watatu hivi wenye ushawishi wa kutosha kwa wananchi, hili ndilo jambo watu wangetegemea litokee.
Akina nani, Majaliwa, Lukuvi, Kalamaganda, Polepopo, Nchimb, Mtaka, Kalemani, n.k.i?
Wataanzia wapi na lini?Mbona muda unapita haraka sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…