Aisee kwanza hilo jina sijawahi kulisikia kwingine kokote, Taradadi; umenikumbusha mbali sana mkuu, for sure huu uzi nimeukubali.
cc Ntuzu
Disco la mwanaisungu, tabora hotel.
Basketball kwenye grounds za uhazili.
Nani alisoma mwenge, kipindi cha mwalimu chiboni?
Duh!! Wewe unakumbuka sana shule ya Mazoezi Mwenge. Huyu Mwalimu Chiboni alikuwa headmaster, alikuwa anajua kiingereza kizuri na fasaha sana but alikuwa Mlevi wa Pombe, Alikuwa mwenyeji wa Dodoma(Mgogo) na mara ya mwisho nilimwona 1993 Salanda-Dodoma nikipita na treni akiwa hana chochote.
Pia kulikuwepo na walimu wengine kama:
1/Mwalimu Shigela(Inadaiwa huyu mama alianza kufundisha na Nyerere enzi za Mkoloni, alinifundisha kusoma na kuandika!!)
2/Mwalimu Mihayo.
3/Mwalimu Pongo(Nilisikia huyu mama alikufa kwenye ajali ya Mv Bukoba 1996)
4/Mwalimu Husein.
5/Mwalimu Maduhu.
Sijui kama unakumbuka ile mihogo mizuri ya kupikwa iliyokuwa na Pilipili ikiuzwa wakati wa break?
*TABORA NA MADAKTARI.
Nikiwa Tabora katika miaka ya 1980s na 1990s nilifanikiwa kufahamu mengi kuhusu Madaktari wa binadamu na maishha yao, kwa kifupi nina wakumbuka hawa zaidi. Dr.Kisenge, Dr.Kobello, Dr.Mohamed.
Kwa mfano Dr.KISENGE
Alikuwa na zahanati yake katikati ya mji pembeni mwa jengo la kampuni ya sigara ikitazamana na Jengo la shirika la Bima(NIC) na benki ya zamani ya CRDB(Benki ya ushirika na maendeleo vijijini).
Alifariki 1994.
Watoto wake watatu wakaja kuwa madaktari Dar, Mmoja Dr.Sabuni(Ni daktari bingwa wa watoto pale Muhimbili), Dr.Peter Kisenge(Ni Daktari bingwa wa Moyo pale Muhimbili) na Dr.George(Ni daktari wa Mifugo, yuko Dar akifanya biashara ya vipuri vya Magari Kariakoo).
Yupo mtoto mwingine wa Dr.Kisenge anaitwa Endrew kwa sasa yupo Dar anakula bata tu, yeye ni kupiga hela na kuponda raha, enzi zile kila mrembo mkali aliyekuwa Uhazili jamaa alikuwa anamsaka kwa udi na uvumba, muda mwingi alikuwa akiendesha Kwa kasi Pikipiki Kubwa XL ya Ofisi(Zahanati), Gari ya Baba yake(Pigot 504) na baadaye alinunua Carina yake Nyekundu ili kusaka warembo, jambo la ajabu ni kuwa marafiki zake aliokuwa nao Tabora na baadhi ya warembo wengi wa Uhazili walikufa kitambo sana kwa Ukimwi lakini huyu jamaa inadaiwa mara zote alipopimwa alikuwa yuko Fit kabisa!!
Kuna Matunda huenda yako Tabora tu, kwa mfano Ntalali, Mbuguswa, Mamtonga nk.
Nilijaribu kuyatafuta mikoa mingine lakini sikufanikiwa.
Asante sana.Mkuu jipe Moyo ndivyo wanadamu tulivyo!
Mkuu Nahisi km ulikua jirani na Hiyo familia?
umenikumbusha mbali sana, yani milambo secondary enzi hizo, tulikuwa tunajiita milambo mens, kwenye umiseta au mchakamchaka tukikutana na tabora boys tegemea ngumi kali sana, nawakumbuka warsaw ndo walikuwa mapozeo yetu, nani anamkumbuka mwalimu msemakweli ( Milambo sec), namkumbuka Nehemia msechu mkurugenzi wa NHC kwa sasa na Magesa Mlongo ( Mkuu wa mkoa wa Arusha) wote tulikuwa tunapiga nao ngema, Deusidedit Kibamba ( mambo ya katiba kama sikosei) na kumbukumbuka mwalimu wangu wa chemistry Mr. Kyala, ilikuwa raha sana kipindi kile, na tuligoma mwaka 94 mgomo ulifanikiwa na kumuondoa mkuu wa shule (mr. Msemakweli) enzi zile za Dr. lawrence Gama ( Mungu amlaze mahala pema peponi amin)
Wakuu salama?
Nimeona tukumbushane mambo na vituko vya mboka na story kibao za mkoa ule! Na mitaa, matunda ya porini km Magongoti, vijana Wa mboka, Mwanaisungu etc.
Wakuu Mwenye story ya mboka Au Mwenye chochote kile aje tupige porojo kidogo!