Kwa wale wana CCM mnaoutaka Urais 2030, Je mtaiweza nguvu ya Ridhwani Kikwete?

Dola ndio wao ……
You say bring something on the table …… what if I am the table ?
 
Na Riz mwenyewe ni wewe uliepost humu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2030 ni Dr. Emmanuel John Nchimbi.
 
Tanzania tunabahati mbaya sana, tunapenda kuongozwa na watu tusiowajua focus zao. Huwa tunahisi tu kwamba fulani anafaa kuwa Rais na hisia hizo zikitukolea ndo wachache wenyewe power wanaanza kututafutia vi-element vya ubora wake. Nadhani ni marais wawili tu Nyerere na Mkapa ambao kabla ya kupata urais walitoka hadharani kupitia wananchi, vyombo vya habari na midahalo kwamba wanaenda Ikulu kufanya nini au kuleta nini katika nchi hii. Ni vema watu tunao wahisi ni viongozi wazuri tuwasukumize mbele ya wananchi kupitia vyombo vya habari, midahalo ili tu-unlock vilivyomo kwenye vichwa vyao kabla hatujawapa madaraka makubwa. Haya mambo ya kusema tu fulani anafaa kuwa Rais tuachane nayo ndio yanatupelekea kwenda mbele na kurudi tulipotoka. Kila anaeingia anaonekana " huyu haijawahi tokea" akimaliza mda wake ndo tunaona matatio yake.
 
CCM hairuhusu Midahalo

Hakuna anaejua road map ya Samia ;

Ila si wanasema anaupiga mwingi

Kazi na utu 🤣
 
Hii nchi tumelogwa wallahi..!! 😹😹
 
Ukristo mbele.
Palipo na ukristo kuna ushindi.
Naungana na wewe

Dini ya kwanza ni Uyahudi. Wakaja wakiristo then Islam

Ila tunaambiwa Uislam ndio dini ya kwanza na ulianza tangu Adam anaumbwa if Adam ever existed

Confusing 🫤
 
kwasababu zanzibar inaongozwa na binamu yako na tanzania awamu ya pili iliongozwa na babu yako si ndio

mimi sijaleta hoja ya zanzibar, bali nimeleta hoja ya Tanzania

hujui kama zanzibar na Tanzania ni nchi mbili tofauti ambazo kila moja ina raisi wake, je umewai kuona rais wa Tanzania anateua waziri wa zanzibar ama mkuu wa wilaya wa zanziba?

zanzibar ni nchi inayojitegemea na Tanzania ni nchi inayojitegemea
 

Mkuu ushawai kuramba asali wewe?
Ukalamba mara moja, ukarudia tena na tena na tena?

Inahitaji Uzalendo wa kweli sana na Utakatifu wa kwenda Mbinguni kufanya unachokisema.
 
Mkuu ushawai kuramba asali wewe?
Ukalamba mara moja, ukarudia tena na tena na tena?

Inahitaji Uzalendo wa kweli sana na Utakatifu wa kwenda Mbinguni kufanya unachokisema.

Mkuu issue sio kulamba asali, issues ni kuridhika tu na maisha yako halafu uchukie umasikini wa mamilioni ya Watanzania.

Unaweza kuwaondolea watu umasikini na kustawisha maisha yao wakaishi kwa furaha na wewe ukajinyonyea bila kelele.

Viongozi wengi wa Africa bado hawajajua hii style yakuwapa watu wote good life na kuweka kila kitu halafu viongozi mkaishi kama wanaume kimya bila kelele.
Waarabu wameshaligundua hili sasa ndio maana unaona pale GCC raia wanaishi good life na wale royal families hakuna anayewapigia makelele.
 
kina Makamba, Nape, Doto, Mwigulu, Emmanuel, Kassimu , Makonda the great ….mtamuweza huyu mtoto wa kishua aliyezungukwa na ufalme wa Adam and Ev?

Hawa Vijana Watauwana kwa kuutaka Urais. Hapo umemsahau Hussein Mwinyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…