Kwa wale wenye "MAJINI" vichwani au pembeni yao

Kwa wale wenye "MAJINI" vichwani au pembeni yao

jamii forums ukiweka uzi intelligence bila walokole kufanya yao basi jua hujaweka uzi bali quote halafu unaweza kusema wasafi kweli kumbe mmmmnhh!

#Rakims
 
Group ya whatsapp ya watu wenye majini.
.nimelipenda Hilo..
 
vizuri nimeshalifunga maana hapakunukia palichafuka
 
vizuri nimeshalifunga maana hapakunukia palichafuka

Mkuu Rakims unalalamika sana!
Na umesahau humu changanyikeni sana, after all ni wewe ndie ulieruhusu hilo kwa maana umeweka mada ila unakataa kujadili na unalazisha watu waje wazapu, si umeona hata uko wazapu yamekushinda!
 
Katika ufalme wa Majini, Shetwani ndiye Mfalme.

Vv

Mkuu Rakims unalalamika sana!
Na umesahau humu changanyikeni sana, after all ni wewe ndie ulieruhusu hilo kwa maana umeweka mada ila unakataa kujadili na unalazisha watu waje wazapu, si umeona hata uko wazapu yamekushinda!

Ndio Uwezo Wako Wa Kufikiria Umeishia Hapo?

"Rakims"
 
Swali dogo kwa mwanzisha mada.....anajua Lusifer (shetani) alihasi na malaika zake?

Utawaitaje malaika waliotupwa huku duniani pamoja na bwana wao Lusifer? acheni kudanganywa .......hakuna jini zuri .....jini ni jini.....kitofautiana tabia kwa majini hakufuti kuwa ni waasi waliokwisha hukumiwa .......
 
Kwa KUANZA Naushusha UZI Huu Maalumu Kwa Watu Mwenye Marohani/Majini WASAFI Yaani ASIE Kutesa Wala Kukushurutisha Yupo Tu Labda Kukushauri Au Mambo Mengine Sizungumzii Kuwaalika Watu Hapa Wasio Na MAJINI vichwani au Ndotoni Tofauti Na Majini Wachafu(pepo mbaya).... Wala Wasioamini Uwepo Wa Hawa Viumbe.. wala wenye imani (-) na Hawa Viumbe HIVYO tafadhali Kama Haikuhusu KAA Mbali na Huu UZI....

Kwa Kuanza:

Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;

Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile

vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.

Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.

Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.
Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.

Majini Ni Viumbe Ambao WAPO Kama WANAADAMU Kwa kuwa na free wills yani maamuzi ya uhuru kwamba naamini au siamini iwe katika mungu au shetani.. sita waelezea sana kwa maana wameshaelezewa sana ila mimi napiga mng'arisho au msasa ili ufahamu wa watu uzidi kuongezeka..

VIUMBE Hawa wamegawanyika makundi mawili wapo waliomuamini mungu mmoja hawa huitwa marohani na wapo ambao hawajaamini wanamfuata shetani pia wao wanaitwa mapepo wachafu au majini wabaya mradi tu wawekwe kwenye ubaya ubaya..

ila wao kwa jina la kundi tunaweza kuwaita walioasi au waislamu huwaita makafiri wa kijini na wakristo huwaita mapepo wachafu.

Pepo wachafu au makafir wa kijini kwa ujumla majini waliumbwa kabla ya wanaadamu na walipewa machaguo ya uhuru wengi wao wakamuasi mwenyezi mungu ndio amri ikashuka kwamba waangamizwe wote na malaika viumbe watiifu wakashuka na kuja kuangamizi majini wengi..

Lakini hawakuangamizwa wote kwa maana wengine walipewa uwezo na mwenyezi mungu kuingia popote vyovyote hivyo waliingia majabarini chini ya mabahari na wengine waliingia katika matumbo ya wanyama..
.
vile malaika hawakupewa uwezo huo wakarudi na kumtaarifu mwenyezi hali halisi ndipo wakaruhusiwa kuwaacha wale waliokimbia....

Baadhi waliogopa sana kwa kuona mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu wakaanza kutubu ndio hawa huitwa leo Majini wema Au Maruhani..

Waliobaki wengine walijiona wenye nguvu na waliweza kujihisi wamemkimbia mwenyezi na Wakaendelea Kufanya Maasi Yao...

kitu kingine watakiwa kujua majini wapo mara 300 yako wewe yani kila binaadamu wapo mara idadi hiyo yake Viumbe Hawa huishi miaka mingi wengine hufika hadi miaka 1000/-

majini wema hawamkalii mtu kwa ubaya humpenda na kutamani kumsaidia.. hawampotoshi imani yake alionayo humuangalia tu nakumsaidia mambo mengi tu bila kujijua kama mtu kufaulu vema bila kujijua wala kusoma sana, kupendwa pendwa na watu, kupenda mambo ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili, humfanya mtu awe na huruma.

Kumletea ndoto njema akilala na humpunguzia maumivu ya mwili bila kujijua.. kumfanya afikirie jambo jema mtu hadi alifanye.. hawana roho mbaya hulia pale unapofanyiwa ubaya wengine hupanda kichwani na kulia sana pale unapouziwa wengine hukupitishia kitu kama hope rohoni au barafu unajiskia umekaa sawa na kusema one day yessss! huomba pamoja na wewe pale unapotupa malalamiko yako kwa mwenyezi mungu kwa imani yako....

majini wabaya au pepo wachafu humfunga mtu riziki zake na humrudisha nyuna mtu mambo yake na kumbaka kumfedhehesha mpaka akaanza kumkufuru mola wake, na kuanza kujihusisha na ushirikina ndio anaona anafanikiwa humnyanyasa ndotoni kwa kuota anakimbizwa anapigana anatukanwa.. anadhalilishwa anaumwa anateswa na akiamka anakuwa hana raha... humjaza mtu ujasiri anapotaka kufanya tukio chafu....

jinsi ya kujijua kama una jinni:

MSAFI/MCHAFU AU Huna tu

kwa kuwa hawa ni viumbe tuwafananishe na bacteria wanapokuingia huwaoni lakini madhara mwili unapata...

ZIFUATAZO NI DALILI ZA KUJUA KAMA UNA JINI MSAFI AU MCHAFU KIIMANI
..

1: Kuumwa kichwa kisichojulikana mwanzo wala mwisho mradi tu kinauma kila siku muda wowote

2. Uzito ktk Mabega au hata kichwani kwenyewe.

3. Kuota vitu vya kutisha usingizini

4. Kuchukia kuona au kuolewa km bado hujaoa au kuolewa.

5. Kwa alie Oa au kuolewa huchukia Tendo la ndoa

6. Kupatwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada

7. Baadhi ya wanawake hukosa Maji maji katika UKE wakati wa kufanya tendo la ndoa na hivyo wakati mwingine hupatwa na michubuko endapo lita lazimishwa tendo hilo

8. Baadhi ya wanaume hushindwa kumalizia vizuri tendo la ndoa au kumaliza haraka zaidi na kisha kupatwa na usingizi Mzito Mara tu baada ya kumaliza Tendo la ndoa.

9 Km una mke au Mme hutaki kufanya nae tendo la ndoa na usiku huo ulio kataa unaota unafanya na mtu mwingine.

10.Kuwa na hasira za ajabu wakati wa kuamka asubuhi.

11.Wakati mwingine huona km kuna mtu kakuinamia wakati ukiwa umelala taa imezima(kiza)

12.Wakati mwingine huhisi km kuna mtu anatembea ndani ya chumba ulicho lala. Ukijaribu kuwa makini kumsikiliza au kuwasha taa humuoni mtu yeyote.

13: kujilaumu hadi kuhisi kulengwa na machozi kwa kosa dogo tu

14: kuchukia kutumwa na hupenda kujiajiri

15: kuchukia sana dhambi

16: ukikaa sehemu ya kimya sana unasikia watu wanaongea kichwani

17: kuota unasali kila mara hali ya kuwa kama unajilazimisha kusali ikiwa imekupita hata sala moja

18: kustuka saa nane usiku baada ya kuota umeamshwa kusali au adhana ya kwanza kwa mwislamu

19: kuota unamuombea mtu na mwili wako kujaa nguvu kwa mkiristo

20: kuota unaongea na kiumbe asiekuwa binaadamu either mnyama au ndege..

zipo hizo ni baadhi tu.. hii ni fursa kwako wewe mwenye majini kujitambua je ulionayo ni mema au mabaya? na unayatumia au yanakaa tu? unayatoa au unabaki nayo unaongeza elimu ili usimkufuru mwenyezi kwa kuwa na majini....

karibuni
P.M Namba Yako Tutengeneze group ya WHATSAPP Ya watu wenye maruhani tufundishane namna ya kuwatumia vema ili wasitupotoshe ikiwa unao na unajificha basi kumbuka huwezi kukimbia kivuli chako..

Walikupeleka wapi walikufundisha nini? yapi ya ajabu uliyaona? yapi yalikufanya ukainua mikono juu ukasema kweli mwenyezi umeumba hawa viumbe? haya na mengine mengi tutayaangalia humo kwenye group.

kuna watu hawana na wanawish wawajue na wawe nao nafasi zipo 15 tu na kuingia kwenye group jini wachafu hatuta fundisha...
. 30 wale wenye marohani wasiojuwa jinsi ya kuwaongoza na kuwatumia...

karibu tujadiliane....

#Rakims

We ndio bure kabisa, mkuu unamjua kifaa mmoja mtu wa Ajemi anaitwa MziziMkavu ? Huyu alienda deep balaa kwenye issue za majini! We endelea na ile issue yako ya vampires ya akina Damon na Stefan
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada, kwa mtazamo wangu na jinsi nijuavyo jini ni jini tu, kila siku yeye ni adui mkubwa wa binadamu. Mimi kidogo namna ya ku link watu bado kunagongana, ila kuna jamaa anaitwa mustapha Songoro, anazungumzia vizuri kuhusu majini na kwa kina kirefu kuhusu hawa viumbe wa ajabu alipotembelea kule nchi ya Burundi kufanya mihadhara ya kidini.

Viumbe hawa wanahusika na madhara mengi tunayoyapata sisi binadamu kwa hiyo jaribuni kumsikiliza Mustapher Songoro na topic yake kuhusu MAJINI mle kafafanua mambo niliyokuwa siyajui kuhusu hawa jamaa wa binadamu na wapinzani wetu wakubwa ktk huu ulimwengu.M/Mpamba.

Last edited by a moderator:
Distruction nyingi zinafanya na haya madude na kupitia shetani hata majanga tunayopata sababu ni haya majini.
 
Swali dogo kwa mwanzisha mada.....anajua Lusifer (shetani) alihasi na malaika zake?

Utawaitaje malaika waliotupwa huku duniani pamoja na bwana wao Lusifer? acheni kudanganywa .......hakuna jini zuri .....jini ni jini.....kitofautiana tabia kwa majini hakufuti kuwa ni waasi waliokwisha hukumiwa .......

Imani Yako Inaamini Wote Majini Ni Wakupelekwa KUZIMU JEHANAMU MOTONI Eti?

na kama ni hivi basi kumbe mungu wako sio mtukufu kama mungu ninaemuabudu mie yule ambae sifa zote ni zake pekee..

za kuhukimu,kusamehe na Kuongoa...

na kama unaamini hivyo means hata wewe ni muasi maana huwezi kujua umetokana na mlolongo wa jamii ipi baba etu afam pia alimuasi mungu na kuhukumiwa miaka 40 na baadae akasamehewa je, kama mungu wako hajui kusamehe anajua kuhukumu hapa si angemuhukumu moja kwa moja adam? lakini kwa nini? kutuonyesha sisi utukufu alionao akamsamehe kwa sifa zake mwenyezi mungu mwingi wa rehma...

Jina Lako Si Mtazamo? je, mtazamo wako haukufika huku? kuona kama babaako aliasi basi na nyie kizazi chote mmehukumiwa..

kwanza mungu yupo unamuamini ww? nijibu kwa kishindo hapa....

mungu wangu mimi anasamehe kila aombae msamaha wako anasamehe vipi?

je mungu wako kuna viumbe kawaumba kwamba hawa nimewaumba tawatia moto wa milele tu? mungu gani unaabudu?

Miungu Wanaohukumu hivyo ni hawa yupi wako?

1:sanam
2:mti
3:jua
4:mwezi
5: mdoli
6:shetani
7:mtu
8;budhaa
9:Moto
10:uchi

hao ndio miungu ya wasioamini mungu mmoja...

lakini yule alietakasika mwenyezi mungu mmoja yeye hana mshirika wala anaefanana nae huukumu kila kiumbe bile atakavyo yeye who are you kuhukumu majini wote kwenda motoni? au wewe ni mwenyeji wao kule?

MTAZAMO badili username maana huitendei haki..
mtazamo hauoni mbali

"Rakims"
 
Ndugu zangu,

Wakati wa misukosuko hiyo ya kupambana na jini,mara nyingi kuna ukosefu wa elimu na utaratibu wa kumtambua kiumbe yule yupo kwa ajili gani mwilini mwa binadamu.Kwa wale majini waliopo kwa minajili ya uharibifu wanayo tabia ya kufunga ufahamu mzima wa binadamu na huzungumza na kufanya mambo mengine bila ya mwenye tatizo lile kujua kinachofanyika.

Hii inatokana na jini yule kuwa na hasira ya kuingiliwa kwenye himaya aliyopo kwa wakati ule kwa kazi yake.Hii husababisha mtu kuwa na nguvu sana kiasi cha kuweza kuwasukuma na hata kuwaumiza watu wanaomkamata yule mwenye tatizo.Sasa hapa ndipo kuna tatizo.

Utakuta wanaofanya kazi ile iwe ni maombi au "Kukemea" kwao hawawezi kubaini kwamba kiumbe yule yupo kwa shari au amani.Hapa Watendaji wanakosa subira na elimu na kukurupuka kama kinahotaka kufukuzwa ni paka au mbwa.Mwishowe huwa ni purukushani na kuumizwa.

Na ikumbukwe kwamba jini yule haonekani na ikiwa ataamua kutulia na kusogea pembeni,mliyofanya kazi ile mtajiona mmeweza bila kujua kwamba jini yule atatoka akiwa na hasira na kwenda ama nyumbani au popote na baadaye kurudi akiwa na ghadhabu maradufu na kumuadhibu binadamu yule kwa namna anavyojua yeye.Hii ni aina ya kwanza ya jini.

Ya pili,kuna jini yupo kwa sababu ni wa asili katika ukoo ule na yupo kwa sababu ya kumsaidia binadamu yule katika maisha yake.Mathalan mtu yule hajijui kuwa anaye kiumbe kama yule.Sasa basi nataka tuelewane hapa.Majini wa aina hii hawafanyi uharibifu ila wanampa wakati mgumu na hata mambo yake kutokwenda vizuri.

Na hata ikitokea akaenda kwa watu wenye ujuzi wa kuwatambua viumbe hawa,na inapotokea kiumbe yule kuzungumza mara nyingine binadamu mwenye kiumbe yule husikia na kuelewa kinachofanyika.Utakuta kwamba anampa wakati mgumu mtu yule kwa sababu yapo makosa anayoyafanya kama kutosali,kwenda sehemu za starehe zenye mabo ya ajabu na hata kuwa na mahusiano na wanawake/wanaume zaidi ya mmoja,kutokuwajali wazazi na mengine mengi.

Kiujumla kukiuka kulikokithiri kwa mafundisho ya dini.Hapa lazima mtu aonje joto ya jiwe.Na inapotokea mhusika akaenda kwa watu sahihi na siyo kwa makelele na kufukuzana,hapo tatizo litajulikana na jini yule kuzungumza chanzo cha matatizo ya mtu yule ni nini na inatakiwa afanye nini.na ikitokea mkamwelewa jini yule na kutekeleza yaliyosemwa,mambo huwa mazuri na amani kutawala.

Lakini ikitokea akapelekwa sehemu za watu kukurupuka na kuanza biashara ya kupigiana kelele,nyimbo na amri za kufukuzana,hapa niwaambie wazi madhara yake kwa aliye na kiumbe yule,waliyo hodari kwa kelele na amri bila kuwa na elimu nalo ni makubwa. inatokea mkaadabishwa kwa namna nyingi.wengine kupoteza mali,hadhi na kazi.hayo ni machache tu katika mengi niliyo nayo
 
We ndio bure kabisa, mkuu unamjua kifaa mmoja mtu wa Ajemi anaitwa MziziMkavu ? Huyu alienda deep balaa kwenye issue za majini! We endelea na ile issue yako ya vampires ya akina Damon na Stefan

eti eenh? hata mimi nimeelewa vema kweli kweli kuna sehemu kaongea kina belbez na lucifer je unajua ni aina gani ya jamii ambayo yeye kawaingia deep kwenye uzi wake kule kawachambua wale kina ibilisi na wajukuu zake na watoto wake na vifanyakazi vyake na majeshi yao all in all hata yeye kama yupo around hapa atakubali kwamba hapa nazungumzia majini wema yeye anazungumzia majini waovu wote.... takupa mfano ngoja nikakuibie kwenye uzi wake nikuletee hapa...
yeye kule anazungumzia mashetani wa kijini mimi nazungumzia majini walioamini... tupo tafauti kidogo halafu mi naozungumzia hawatishi naongelea jini unaemuuliza swali anakujibu ndotoni yeye anawaongeleeni majini unaemuuliza swali anakwambia nichinjie mbuzi ngombe siku likitaka kubadili radha linakwambia nipe mtoto wako hapo ndio utamtafuta mzizi usimuone wala gome mwisho wa siku unakimbilia kwa walokole na mashehe wakusaidie wakusaidie nini uliyataka mwenyewe....?

"Rakims"
 
Last edited by a moderator:
Imani Yako Inaamini Wote Majini Ni Wakupelekwa KUZIMU JEHANAMU MOTONI Eti?

na kama ni hivi basi kumbe mungu wako sio mtukufu kama mungu ninaemuabudu mie yule ambae sifa zote ni zake pekee..

za kuhukimu,kusamehe na Kuongoa...

na kama unaamini hivyo means hata wewe ni muasi maana huwezi kujua umetokana na mlolongo wa jamii ipi baba etu afam pia alimuasi mungu na kuhukumiwa miaka 40 na baadae akasamehewa je, kama mungu wako hajui kusamehe anajua kuhukumu hapa si angemuhukumu moja kwa moja adam? lakini kwa nini? kutuonyesha sisi utukufu alionao akamsamehe kwa sifa zake mwenyezi mungu mwingi wa rehma...

Jina Lako Si Mtazamo? je, mtazamo wako haukufika huku? kuona kama babaako aliasi basi na nyie kizazi chote mmehukumiwa..

kwanza mungu yupo unamuamini ww? nijibu kwa kishindo hapa....

mungu wangu mimi anasamehe kila aombae msamaha wako anasamehe vipi?

je mungu wako kuna viumbe kawaumba kwamba hawa nimewaumba tawatia moto wa milele tu? mungu gani unaabudu?

Miungu Wanaohukumu hivyo ni hawa yupi wako?

1:sanam
2:mti
3:jua
4:mwezi
5: mdoli
6:shetani
7:mtu
8;budhaa
9:Moto
10:uchi

hao ndio miungu ya wasioamini mungu mmoja...

lakini yule alietakasika mwenyezi mungu mmoja yeye hana mshirika wala anaefanana nae huukumu kila kiumbe bile atakavyo yeye who are you kuhukumu majini wote kwenda motoni? au wewe ni mwenyeji wao kule?

MTAZAMO badili username maana huitendei haki..
mtazamo hauoni mbali

"Rakims"

Mungu wetu si kigeugeu ........anatimiza ahadi zake.....wewe mwenyewe kwa kutumia ulichoandika kwa mujibu wa imani yako utaona ni hadithi tu za kufurahisha .....yaani Mungu mwenyewe aagize malaika wakaangamize majini wote alafu eti wengine wakimbilie kwenye matumbo ya wanyama na baharini ndio iwe salama yao? Yaani mission ya Mungu ifeli? kisa sijui malaika hawana uwezo huo na Mungu alipoambiwa nae akakosa cha kufanya na kuamua kuwaacha?

Hii si kweli ila itakuwa kweli kwa Mungu wenu ...........nipe jibu.....malaika walioasi na Lusifer na kutupwa duniani nyie mnawaitaje?

Binadamu ndio kiumbe pekee kilichoumbwa na kupewa utashi na kuwa mfano wa Mungu mwenyewe na hiki ni moja ya kitu kinachofanya binadamu kuwa kiumbe cha kilichopendelewa kuliko hata Malaika.Msamaha ni kwa wanadamu tu na si kiumbe kingine chochote na hao malaika waasi na baba yao Lucifer walishahukumiwa........mpango wa Wokovu ni kwa wanadamu tu na si malaika waasi hata wafanye nini......hukumu yao ipo pale pale ............

Sasa hili somo la kuwepo viumbe wengine wenye utashi kama binadamu lina ukweli gani? Hamuoni haya mafundisho ndio yanayopelekea watu kufuga majini na kuyatumia kinyume na maagizo ya Mungu? Mungu anataka tumtegemee yeye TU......na Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu ......iweje aruhusu kiumbe chake binadamu kutegemea msaada wa majini wakati ametupa Malaika watutumikie kwa msaada wa utenda kazi wa Roho yake mwenyewe?
 
Hivi wakati jini anaamini ww ulikuwepo? Utathibitishaje kuwa jini anaamini Mungu? Kuna mmoja alisema jinni mwingne anakuwa wa kifamilia anamsaidia mtu katka mambo flan flani..hahhaha na Mungu je? Huyu anaesema anasaidiwa na jinni basi huyo ni washetani...

Pili, eti baadhi ya majini walijificha kwny matumbo ya wanyama.Ndio wengne waka surrender na wengne kukubali kuwa mungu ana hasira sana. Aisee mm nasema hayo ni mafundsho ya kishetani na baadhi shetani kesha wanasa wamehararisha majini,wkt Mungu aliyatupa huku kutokana na uasi..

Nyinyi mliopotea sasa ndio mnayaabudu kwa namna moja ama nyngne,,kuthibitisha hilo kuna mmoja alisema humu,kuwa yanasaidiwa familia!! OMG familia isaidiwe na majin? Na sio Mungu,kama sii kuyaabdu ni nini? Jini linaamuru liletewe,sijui ubani,mara kaniki nyeusi,mara udi ,mara sijui nn nini? Na unatekeleza ili likupe siri sijui limeona nn aise,,huko ni kupotea kabisa...

Hivi Mungu aliyeweza kuangamiza Dunia yoote kwa Maji ashindwe kuwa maliza hao majini walio jificha ndani ya matumbo????? Mungu aliyeangamiza Sodoma na Gomora kwa Moto ashindwe kuwaangamiza majini waliojificha kwenye Matumbo....Kweli shetan haangali hadhi ya mtu,haangalii kijana,mzee,mbaba,mama wala kibibi akikupotosha na ww ukaingia mazima basi ndo kwa heri..
 
1gb, well said mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mungu wetu si kigeugeu ........anatimiza ahadi zake.....wewe mwenyewe kwa kutumia ulichoandika kwa mujibu wa imani yako utaona ni hadithi tu za kufurahisha .....yaani Mungu mwenyewe aagize malaika wakaangamize majini wote alafu eti wengine wakimbilie kwenye matumbo ya wanyama na baharini ndio iwe salama yao? Yaani mission ya Mungu ifeli? kisa sijui malaika hawana uwezo huo na Mungu alipoambiwa nae akakosa cha kufanya na kuamua kuwaacha?

Hii si kweli ila itakuwa kweli kwa Mungu wenu ...........nipe jibu.....malaika walioasi na Lusifer na kutupwa duniani nyie mnawaitaje?

Binadamu ndio kiumbe pekee kilichoumbwa na kupewa utashi na kuwa mfano wa Mungu mwenyewe na hiki ni moja ya kitu kinachofanya binadamu kuwa kiumbe cha kilichopendelewa kuliko hata Malaika.Msamaha ni kwa wanadamu tu na si kiumbe kingine chochote na hao malaika waasi na baba yao Lucifer walishahukumiwa........mpango wa Wokovu ni kwa wanadamu tu na si malaika waasi hata wafanye nini......hukumu yao ipo pale pale ............

Sasa hili somo la kuwepo viumbe wengine wenye utashi kama binadamu lina ukweli gani? Hamuoni haya mafundisho ndio yanayopelekea watu kufuga majini na kuyatumia kinyume na maagizo ya Mungu? Mungu anataka tumtegemee yeye TU......na Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu ......iweje aruhusu kiumbe chake binadamu kutegemea msaada wa majini wakati ametupa Malaika watutumikie kwa msaada wa utenda kazi wa Roho yake mwenyewe?

Vyote Umeongea Nimekubali Ni Imani Yako Ndio Imekutuma ila Hapo uliposema kwamba shetani ni baba wa malaika waliohasi inaonyesha umeshamtukuza Shetani Kuwa Ni Mkubwa Wa Baadhi Ya Malaika Waliohasi Na MAJINI Umedai Tayari ni Malaika... ila waliohasi
"hivi unawajua harutta na maaruta?"

kama huwajui hawa ndio malaika wawili tu walioinamishwa kwenye uchafu wa dunia yote na ndio waliohasi

sasa jini unaambiwa kaumbwa kwa moto na malaika kwa mwanga au nuru na binadamu kwa mavumbi huyo ibilisi shetani kaumbwa kwa ulimi wa moto..

huo umalaika anautoa wapi?

hii inaonyesha kichwa chako hakijafuga ufia dini tu na ujinga upo sana tu..

unaita majini malaika waliohasi we unaumwa kweli yani..

"Rakims"
 
1gb same question for you: kabla sijaenda mbali, umeniuliza wakati jini anaamini kama nilikuwepo? SIKUWEPO. Sasa na Wewe Wakati Mungu Anakuumba Ulikuwepo?

"Rakims"
 
Last edited by a moderator:
Well said mkuu

He Still 1gb as His Name State..
angalia swali alioniuliza la kishabiki.. wakati jini anaamini nilikuwepo vipi yeye nikimuuliza wakati yesu anasema ni mungu alikuwepo?

nisije nikakufuru bure.. mungu anisamehe kufundisha mbumbumbu kazi...

"Rakims"
 
Back
Top Bottom