Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
vizuri nimeshalifunga maana hapakunukia palichafuka
Katika ufalme wa Majini, Shetwani ndiye Mfalme.
Vv
Mkuu Rakims unalalamika sana!
Na umesahau humu changanyikeni sana, after all ni wewe ndie ulieruhusu hilo kwa maana umeweka mada ila unakataa kujadili na unalazisha watu waje wazapu, si umeona hata uko wazapu yamekushinda!
Kwa KUANZA Naushusha UZI Huu Maalumu Kwa Watu Mwenye Marohani/Majini WASAFI Yaani ASIE Kutesa Wala Kukushurutisha Yupo Tu Labda Kukushauri Au Mambo Mengine Sizungumzii Kuwaalika Watu Hapa Wasio Na MAJINI vichwani au Ndotoni Tofauti Na Majini Wachafu(pepo mbaya).... Wala Wasioamini Uwepo Wa Hawa Viumbe.. wala wenye imani (-) na Hawa Viumbe HIVYO tafadhali Kama Haikuhusu KAA Mbali na Huu UZI....
Kwa Kuanza:
Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;
Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.
Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile
vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.
Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.
Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.
Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.
Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.
Majini Ni Viumbe Ambao WAPO Kama WANAADAMU Kwa kuwa na free wills yani maamuzi ya uhuru kwamba naamini au siamini iwe katika mungu au shetani.. sita waelezea sana kwa maana wameshaelezewa sana ila mimi napiga mng'arisho au msasa ili ufahamu wa watu uzidi kuongezeka..
VIUMBE Hawa wamegawanyika makundi mawili wapo waliomuamini mungu mmoja hawa huitwa marohani na wapo ambao hawajaamini wanamfuata shetani pia wao wanaitwa mapepo wachafu au majini wabaya mradi tu wawekwe kwenye ubaya ubaya..
ila wao kwa jina la kundi tunaweza kuwaita walioasi au waislamu huwaita makafiri wa kijini na wakristo huwaita mapepo wachafu.
Pepo wachafu au makafir wa kijini kwa ujumla majini waliumbwa kabla ya wanaadamu na walipewa machaguo ya uhuru wengi wao wakamuasi mwenyezi mungu ndio amri ikashuka kwamba waangamizwe wote na malaika viumbe watiifu wakashuka na kuja kuangamizi majini wengi..
Lakini hawakuangamizwa wote kwa maana wengine walipewa uwezo na mwenyezi mungu kuingia popote vyovyote hivyo waliingia majabarini chini ya mabahari na wengine waliingia katika matumbo ya wanyama..
.
vile malaika hawakupewa uwezo huo wakarudi na kumtaarifu mwenyezi hali halisi ndipo wakaruhusiwa kuwaacha wale waliokimbia....
Baadhi waliogopa sana kwa kuona mwenyezi mungu ni mkali wa kuadhibu wakaanza kutubu ndio hawa huitwa leo Majini wema Au Maruhani..
Waliobaki wengine walijiona wenye nguvu na waliweza kujihisi wamemkimbia mwenyezi na Wakaendelea Kufanya Maasi Yao...
kitu kingine watakiwa kujua majini wapo mara 300 yako wewe yani kila binaadamu wapo mara idadi hiyo yake Viumbe Hawa huishi miaka mingi wengine hufika hadi miaka 1000/-
majini wema hawamkalii mtu kwa ubaya humpenda na kutamani kumsaidia.. hawampotoshi imani yake alionayo humuangalia tu nakumsaidia mambo mengi tu bila kujijua kama mtu kufaulu vema bila kujijua wala kusoma sana, kupendwa pendwa na watu, kupenda mambo ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili, humfanya mtu awe na huruma.
Kumletea ndoto njema akilala na humpunguzia maumivu ya mwili bila kujijua.. kumfanya afikirie jambo jema mtu hadi alifanye.. hawana roho mbaya hulia pale unapofanyiwa ubaya wengine hupanda kichwani na kulia sana pale unapouziwa wengine hukupitishia kitu kama hope rohoni au barafu unajiskia umekaa sawa na kusema one day yessss! huomba pamoja na wewe pale unapotupa malalamiko yako kwa mwenyezi mungu kwa imani yako....
majini wabaya au pepo wachafu humfunga mtu riziki zake na humrudisha nyuna mtu mambo yake na kumbaka kumfedhehesha mpaka akaanza kumkufuru mola wake, na kuanza kujihusisha na ushirikina ndio anaona anafanikiwa humnyanyasa ndotoni kwa kuota anakimbizwa anapigana anatukanwa.. anadhalilishwa anaumwa anateswa na akiamka anakuwa hana raha... humjaza mtu ujasiri anapotaka kufanya tukio chafu....
jinsi ya kujijua kama una jinni:
MSAFI/MCHAFU AU Huna tu
kwa kuwa hawa ni viumbe tuwafananishe na bacteria wanapokuingia huwaoni lakini madhara mwili unapata...
ZIFUATAZO NI DALILI ZA KUJUA KAMA UNA JINI MSAFI AU MCHAFU KIIMANI
..
1: Kuumwa kichwa kisichojulikana mwanzo wala mwisho mradi tu kinauma kila siku muda wowote
2. Uzito ktk Mabega au hata kichwani kwenyewe.
3. Kuota vitu vya kutisha usingizini
4. Kuchukia kuona au kuolewa km bado hujaoa au kuolewa.
5. Kwa alie Oa au kuolewa huchukia Tendo la ndoa
6. Kupatwa na maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au baada
7. Baadhi ya wanawake hukosa Maji maji katika UKE wakati wa kufanya tendo la ndoa na hivyo wakati mwingine hupatwa na michubuko endapo lita lazimishwa tendo hilo
8. Baadhi ya wanaume hushindwa kumalizia vizuri tendo la ndoa au kumaliza haraka zaidi na kisha kupatwa na usingizi Mzito Mara tu baada ya kumaliza Tendo la ndoa.
9 Km una mke au Mme hutaki kufanya nae tendo la ndoa na usiku huo ulio kataa unaota unafanya na mtu mwingine.
10.Kuwa na hasira za ajabu wakati wa kuamka asubuhi.
11.Wakati mwingine huona km kuna mtu kakuinamia wakati ukiwa umelala taa imezima(kiza)
12.Wakati mwingine huhisi km kuna mtu anatembea ndani ya chumba ulicho lala. Ukijaribu kuwa makini kumsikiliza au kuwasha taa humuoni mtu yeyote.
13: kujilaumu hadi kuhisi kulengwa na machozi kwa kosa dogo tu
14: kuchukia kutumwa na hupenda kujiajiri
15: kuchukia sana dhambi
16: ukikaa sehemu ya kimya sana unasikia watu wanaongea kichwani
17: kuota unasali kila mara hali ya kuwa kama unajilazimisha kusali ikiwa imekupita hata sala moja
18: kustuka saa nane usiku baada ya kuota umeamshwa kusali au adhana ya kwanza kwa mwislamu
19: kuota unamuombea mtu na mwili wako kujaa nguvu kwa mkiristo
20: kuota unaongea na kiumbe asiekuwa binaadamu either mnyama au ndege..
zipo hizo ni baadhi tu.. hii ni fursa kwako wewe mwenye majini kujitambua je ulionayo ni mema au mabaya? na unayatumia au yanakaa tu? unayatoa au unabaki nayo unaongeza elimu ili usimkufuru mwenyezi kwa kuwa na majini....
karibuni
P.M Namba Yako Tutengeneze group ya WHATSAPP Ya watu wenye maruhani tufundishane namna ya kuwatumia vema ili wasitupotoshe ikiwa unao na unajificha basi kumbuka huwezi kukimbia kivuli chako..
Walikupeleka wapi walikufundisha nini? yapi ya ajabu uliyaona? yapi yalikufanya ukainua mikono juu ukasema kweli mwenyezi umeumba hawa viumbe? haya na mengine mengi tutayaangalia humo kwenye group.
kuna watu hawana na wanawish wawajue na wawe nao nafasi zipo 15 tu na kuingia kwenye group jini wachafu hatuta fundisha...
. 30 wale wenye marohani wasiojuwa jinsi ya kuwaongoza na kuwatumia...
karibu tujadiliane....
#Rakims
Swali dogo kwa mwanzisha mada.....anajua Lusifer (shetani) alihasi na malaika zake?
Utawaitaje malaika waliotupwa huku duniani pamoja na bwana wao Lusifer? acheni kudanganywa .......hakuna jini zuri .....jini ni jini.....kitofautiana tabia kwa majini hakufuti kuwa ni waasi waliokwisha hukumiwa .......
We ndio bure kabisa, mkuu unamjua kifaa mmoja mtu wa Ajemi anaitwa MziziMkavu ? Huyu alienda deep balaa kwenye issue za majini! We endelea na ile issue yako ya vampires ya akina Damon na Stefan
Imani Yako Inaamini Wote Majini Ni Wakupelekwa KUZIMU JEHANAMU MOTONI Eti?
na kama ni hivi basi kumbe mungu wako sio mtukufu kama mungu ninaemuabudu mie yule ambae sifa zote ni zake pekee..
za kuhukimu,kusamehe na Kuongoa...
na kama unaamini hivyo means hata wewe ni muasi maana huwezi kujua umetokana na mlolongo wa jamii ipi baba etu afam pia alimuasi mungu na kuhukumiwa miaka 40 na baadae akasamehewa je, kama mungu wako hajui kusamehe anajua kuhukumu hapa si angemuhukumu moja kwa moja adam? lakini kwa nini? kutuonyesha sisi utukufu alionao akamsamehe kwa sifa zake mwenyezi mungu mwingi wa rehma...
Jina Lako Si Mtazamo? je, mtazamo wako haukufika huku? kuona kama babaako aliasi basi na nyie kizazi chote mmehukumiwa..
kwanza mungu yupo unamuamini ww? nijibu kwa kishindo hapa....
mungu wangu mimi anasamehe kila aombae msamaha wako anasamehe vipi?
je mungu wako kuna viumbe kawaumba kwamba hawa nimewaumba tawatia moto wa milele tu? mungu gani unaabudu?
Miungu Wanaohukumu hivyo ni hawa yupi wako?
1:sanam
2:mti
3:jua
4:mwezi
5: mdoli
6:shetani
7:mtu
8;budhaa
9:Moto
10:uchi
hao ndio miungu ya wasioamini mungu mmoja...
lakini yule alietakasika mwenyezi mungu mmoja yeye hana mshirika wala anaefanana nae huukumu kila kiumbe bile atakavyo yeye who are you kuhukumu majini wote kwenda motoni? au wewe ni mwenyeji wao kule?
MTAZAMO badili username maana huitendei haki..
mtazamo hauoni mbali
"Rakims"
Mungu wetu si kigeugeu ........anatimiza ahadi zake.....wewe mwenyewe kwa kutumia ulichoandika kwa mujibu wa imani yako utaona ni hadithi tu za kufurahisha .....yaani Mungu mwenyewe aagize malaika wakaangamize majini wote alafu eti wengine wakimbilie kwenye matumbo ya wanyama na baharini ndio iwe salama yao? Yaani mission ya Mungu ifeli? kisa sijui malaika hawana uwezo huo na Mungu alipoambiwa nae akakosa cha kufanya na kuamua kuwaacha?
Hii si kweli ila itakuwa kweli kwa Mungu wenu ...........nipe jibu.....malaika walioasi na Lusifer na kutupwa duniani nyie mnawaitaje?
Binadamu ndio kiumbe pekee kilichoumbwa na kupewa utashi na kuwa mfano wa Mungu mwenyewe na hiki ni moja ya kitu kinachofanya binadamu kuwa kiumbe cha kilichopendelewa kuliko hata Malaika.Msamaha ni kwa wanadamu tu na si kiumbe kingine chochote na hao malaika waasi na baba yao Lucifer walishahukumiwa........mpango wa Wokovu ni kwa wanadamu tu na si malaika waasi hata wafanye nini......hukumu yao ipo pale pale ............
Sasa hili somo la kuwepo viumbe wengine wenye utashi kama binadamu lina ukweli gani? Hamuoni haya mafundisho ndio yanayopelekea watu kufuga majini na kuyatumia kinyume na maagizo ya Mungu? Mungu anataka tumtegemee yeye TU......na Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu ......iweje aruhusu kiumbe chake binadamu kutegemea msaada wa majini wakati ametupa Malaika watutumikie kwa msaada wa utenda kazi wa Roho yake mwenyewe?
Well said mkuu