Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu hatutakiwi kuinajisi (kuichafua), ushauri wangu kwenu ni kuvumilia hadi utakaporudi kwa mke au mume wako. Mungu ameweka hii kama ni hiari, una uhuru wa kuabstain au kuzini, hawezi kuja kukushika au kukufunga kufuli usizini, ila amekupa maelekezo kwamba unatakiwa usizini, ukizini kuna madhara kimwili na kiroho. Kiroho ni kwamba utakosana na Mungu, utapoteza utukufu wa Mungu na mwisho wa siku kama hautaitubia dhambi yako utaend amotoni. kimwili ni kwamba, mshahara wa dhambi ni mauti, mauti ya kimwili kabisaa, utapata magonjwa na utakufa, jilinde tafadhali.
Maishani mwako kati ya vitu unaweza kuwa navyo vyenye thamani zaidi ya pesa na madini yeyote yele, ni UWEPO WA MUNGU/UTUKUFU WA MUNGU. ukiwa na utukufu wa Mungu hakika yake una vyote, kwasababu yeye ndiye muumba wa vyote, ukipoteza utukufu wa Mungu, umepoteza vyote na mlango wako upo wazi shetani anaweza kukuingia na kukufanya lolote, anaweza kukuletea gonjwa lolote, anaweza kukuletea matatizo yeyote yale, na anafurahia unavyoteseka. ila ukiwa na utukufu wa Mungu shetani hawezi kukufanya chochote.
uchaguzi ni wenu, tafuta kuishi katika utukufu wa Mungu/uwepo wa Mungu kwasababu ndio pona yako. ukichagua kunajisi mwili wako na kutenda dhambi utakapoanza kula matunda yake usilalamike. Mwanamke kuruhusu mwanaume asiye mumeo kuingiliana, unakuwa unanajisi mwili wako, mwili wako hata kama utaona umebaki vilevile lakini kiroho umenajisika, hivyo hivyo na kwako wewe mwanaume, ile kwenda kumuingilia mwanamke asiye mkeo unajinajisi. yaani mnaingiliana, uchafu ule wa kwako unaenda kwake na wa kwake unakuja kwako, kama ni laana, kama ni mikosi, kama ni magonjwa, kama ni mapepo n.k, unashea naye, na shetani mnakuwa mmempa nafasi kuwaingia kwasababu mmekataa njia za Bwana.
Kumbukumbu 30:19, Nazishuhudia mbinguna nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima ili uwe hai, wewe na uzao wako, kumpenda Bwana Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye, kwani hiyo ndio uzima wako, na wingi wa siku zako.