Kwa wanaume. Hakikisha hukosi hivi nyumbani kwako

Kwa wanaume. Hakikisha hukosi hivi nyumbani kwako

Nina kila kitu hapo juu .katika vitu sipendi ni fundi kuja kufanya kikaz kidogo tu anataka elfu ishirin.sasa hata kudrill bomba za pazia inakutoka laki kiulaini kabisa.unashindwa vipi kudril mwenyewe.
Wakati kwa hiyo laki ungekuwa ushajipatia haka kamashine na kanakuwa ka kwako daima
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    17.8 KB · Views: 5
Nilikuwaga nachanganya tester na screw driver, matokeo yake nikawa natumia tester kwenye kazi za screw driver, hapo nimekuelewa, ngoja nitafute screw driver.
Si itapinda mzee.
 
Kwa wanaume wenzangu habari za muda huu, naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika kama nilivyoitambulisha hapo juu. Ikiwa una familia au unaishi bachelor tafadhali zingatia hili linakihusu.

Nyumbani kwako hakikisha mwanaume hukosi essential tools kadhaa kwa ajili ya kupunguza changamoto ndogo ndogo ukizingatiwa wewe ni mwanaume, familia nzima itakutegemea wewe. Vifaa muhimu kabisa hutakiwi kukosa kwako ni kama ifuatavyo:

1. Tester ya umeme. Hakikisha hiki kifaa hukosi kwako, kitakupunguzia ajali kwako za umeme kwa kutambua wapi kuna leakage ya umeme pia itakusaidia ku repair issue ndogo ndogo zinazohusiana umeme kwako, imagine hata kubadilisha holder ya balbu ya taa chumbani kwako uende kumwita fundi aingie chumbani kwako na mkeo.

2. Nyundo ndogo. Vifaa vingi ndani ya nyumba vimeundwa kwa misumali, sasa hata kugongea msumali ulio loose ushindwe?

3. Screw driver. Wengine wanaiita "bisibisi" siku hizi kuna set hata machinga wanaziuza itakusaidia hata kukaza nati ya kitasa chako cha chumbani

4. Panga. Licha ya kazi nyingine ni silaha pia.

5. Jembe. Kila mtu anajua kazi yake

6. Shoka, sururu, kwanja hii inategemea na mazingira yako

7. Tool box, sio lazima liwe special weza tengeneza la mbao au chuma, hifadhi powertools zako.

8. Drills, siku hizi kuna simple drills zinauzwa madukani tena za kuchaji ambayo una regurate speed unaweza tumia kama drill au hata kama screw driver, bei yake inategemea ila ni tool muhimu sana, imagine chumban kwako sasa hivi ukitaka tundika tv ukutani unafanyaje? Utamwita fundi chumban kwako? Kuitumia ni rahisi sana tena YOUTUBE WANAFUNDISHA.

9. Spana. Hapa si lazima uwe na set nzima angalau hata ile adjustable ambayo inaweza fanya kazi kwenye nati tofauti tofauti.

10. Koleo (pliers) siku hizi zipo zenye kazi hadi 4 ndani ya moja

11. Chepe. Hata kuzoa taka ndani ya nyumba uweze, usishindwe hata chimba shimo la taka

12. Reki. Usiwe kila siku wa kuazima reki ya sh 5000

13. Baiskeli. Hii kwa mazoezi, kama nafasi yako ni ndogo siku hizi zipo unazoweza kuzikunja na kuhifadhi sehemu ndogo.

14. Misumari, akiba ya misumali saizi tofauti tofauti itakusaidia repairs zisizotarajiwa

15. Air pump yoyote hata ya mkono. Kama unamiliki chombo chochote cha usafir kilicho na tire ya kujaza upepo usikose hii kitu, imagine umeamka pikipiki au gar imepungua sana upepo utafanyaje? Ndio wamwita fundi? Jaza upepo ukusogeze kwenye tire services

16. Torch. Kazi ya tochi inajulikana kuna wenzetu hata tochi ya battery hana, dharula haina hodi

17. Mashine ya kunyolea (homecut). Kama una watoto hakikisha una mashine yako, weekend watoto unawanyoa mwenyewe, hii inaongeza mapenz ya baba na watoto.

18. Msumeno, yes kwenye toolbox yako uwe na msumeno mdogo hata ule wa 5000 utakusaidia siku moja

19. Mzani, hata ule simple wa spring unaoishia kilo 5 wa bei ndogo sana, kuna siku utakupunguzia kazi hapo kwako.

20. Toroli, kama unaishi nje ya mji toroli muhimu sana kwa shughuli ndogo ndogo nyumbani, usipende kila kitu kubeba utapata madhara ya mgongo.

21. Extension ya umeme, yes kaa na extension ya ziada ya umeme, kuna siku utahitaji kuliko kwenye wagongea majiran upate fedheha.

Kwa mwingine anaeweza endeleza list, share nasi
Acha uchoyo wewe. Kuwa na hivi vitu vyote nyumbani kutazidi kusababisha ukosefu wa ajira kwa mafundi wa aina mbalimbali. Haya basi ongezea na mwiko wa kuchotea zege na kono-bao la kunyooshea plaster za nyumba
 
Condom sio powertools mzee, hiyo ni sehemu ya medical supplies ndio maana sjaongelea hata Paracetamol, cotton wool au iodine tincture ambavyo pia ni muhimu kuwa navyo nyumbani

Condoms ndio the most powerful tool of all, hizo power tools zingine ndio zifuate.. Bila condoms, ukafa utatumia hizo power tools zako, Condoms kwanza, uhai kwanza, afya kwanza, ndio utumie hizo zana zingine..

Edit your post plz, 1: Condoms

Alafu zingine zifuate.
 
Acha uchoyo wewe. Kuwa na hivi vitu vyote nyumbani kutazidi kusababisha ukosefu wa ajira kwa mafundi wa aina mbalimbali. Haya basi ongezea na mwiko wa kuchotea zege na kono-bao la kunyooshea plaster za nyumba
Hivyo ninavyo sikutaja tu sababu si muhimu sana kwa kila mtu, unataka ajili mtu kuja kubadili koki ya maji ya chumba chako cha master? Aibu hiyo mkurungwa, chumbani ni siri
 
Wakati kwa hiyo laki ungekuwa ushajipatia haka kamashine na kanakuwa ka kwako daima
Zipo mpaka za manually unanunua bits tu.inakula ukuta kama sponch .
Ulaya kaz nying unafanya mwneyewe ndio mana unakuta had waschana wanapaint wenyewe kwa maana kuita fubdi ulaya sio fundi maiko.unalipa contractors kabisa.so unakuta vitu ving wanafanya family members
 
Condoms ndio the most powerful tool of all, hizo power tools zingine ndio zifuate.. Bila condoms, ukafa utatumia hizo power tools zako, Condoms kwanza, uhai kwanza, afya kwanza, ndio utumie hizo zana zingine..

Edit your post plz, 1: Condoms

Alafu zingine zifuate.
Kwani UKIMWI unaua? Ilikuwa zamani siku hizi hauui sijui mara ya mwisho ulimwona nani kafa kwa ukimwi, siku hizi hadi machagudoa wana kunywa dawa za kinga kuzuia ukimwi, na wengine wanywa arv
 
Kimsingi hazitakiwi kuuzwa,omba zile self test ni nzuri sana na ni rahisi kufanyia screening ya HIV
Kwa sera ya afya ya tanzania, rapid test ambayo mtu anaweza ji test nayo ni ile ya kutumia mate tu, hizi zingine zinatakiwa kutumiwa na mtaalamu wa afya tu, tumia at your own risk, usisahau kuna forced positive na forces negative, imagine unampima ikasoma neg kumbe ni positive
 
Nimejaribu kufikiri huyo mwanaume awe kapanga chumba kimoja halafu ana hivyo vifaa vyote!

Si atakuwa analala stoo sasa.
 
Maduka gani wanauza kwa hiyo bei?
Kama uko dar tembea kariakoo, waduka ya hardware, ziko za kila aina hata chini ya bei hiyo, pia maduka ya used powertools zipo za kila aina
 
Nimejaribu kufikiri huyo mwanaume awe kapanga chumba kimoja halafu ana hivyo vifaa vyote!

Atakuwa analala stoo.
Angalau kimoja wapo, tutajua unajali uanaume wako
 
halafu nikakata mbao na fito nizipeleke wapi? Sina interest na ufugaji wa kuku
Nunua vile ambavyo una matumizi navyo.

Mtoa mada kaeleza kila kifaa na kazi yake, sasa kulingana na uhitaji wako kulingana na mazingira ndio uchague vya kuwa navyo ndani.
 
Back
Top Bottom