Kwa Wanawake na Wanaume ambao hawajawahi kuolewa wala kuoa

Kwa Wanawake na Wanaume ambao hawajawahi kuolewa wala kuoa

Habari za Majukumu wanajukwaa.....

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, naomba leo niongee na vijana ambao bado hawajaingia Kwenye ndoa.

Yote nitakayoyaongea hapa ni mtazamo na mawazo binafsi, hayaakisi mtazamo wa kundi au taasisi yoyote na Nakaribisha maoni yenye Lengo la kujenga na kusaidia Jamii yetu....

Sasa hivi ni nadra kumkuta kijana anakula kiapo cha ndoa akiwa hajashiriki ngono.

Na jambo hili linaonekana ni jambo la kawaida sana kwenye jamii zetu, ndiyo maana utakuta kwenye social media, movies, miziki na story za vijiweni zinazungumzwa sana story za MAHUSIANO [MAPENZI] lakini kwa bahati mbaya

kinachohamasishwa ni mahusiano kabla ya ndoa na maana isiyohalisi ya mapenzi [sura, maumbile kama tako, handsome, kifua, akipita anadatisha].... Mahusiano/mapenzi ni zaidi ya hivi...

Kwanza katika mapenzi au mahusiano UNAHITAJI MTU AMBAYE ATALEA NA KUZIENZI HISIA ZAKO, MTAJENGA PAMOJA KESHO YENU, ATAKUWA MAMA AU BABA WA FAMILIA YAKO, ATAUNGANISHA UKOO AU FAMILIA YAKO, ATAKUHIFADHI HESHIMA YAKO UKIWA NAYE AU MBALI NAYE, ATAHAKIKISHA USALAMA WAKO WA KIHISIA, KIUCHUMI NA KIJAMII UKIWA NAYE AU UKIWA MBALI NAYE... Je sura pekee itakuhakikishia haya?

Jambo la pili: Kuingia kwenye ndoa ukiwa tayari umetumika ni inshara kuwa tayari ushakuwa na majeraha ya kihisia na pia inawezekana kabisa hisia zako hazijafungwa kwa uliye Naye kwenye ndoa Bali zinaweza kuwa somewhere else.... a bit controversial, right?

Mfano hymen of girl kwa mwanaume atakayeitoa katika mazingira ya makubaliano ni kama agano lililofungwa baina yake na huyo mwanaume ndiyo maana wengi huishia kukumbushia na kuharibu nasaba nyingi kwa kuzaliwa watoto wasio wa yule mwenye ndoa...

Jamani tujitunzeni na tuingie kwenye ndoa tukiwa hatujatumika..... kugawa ngono siyo ishara ya upendo na anayetaka kupewa ngono ili kuonesha kweli anapendwa ajue ule siyo upendo BALI KUTUMIKA KAMA KIFAA CHA STAREHE TU... mahusiano yenye future na kuheshimiana hayawezi kuwa ya mashariti ya vitu [kupiga mizinga au kutaka ngono]....

Mahusiano ya sasa hasa kabla ya ndoa ni biashara isiyo rasmi ya ngono NDIYO MAANA WANAUME WANAGAWA FEDHA NA ZAWADI ZINGINE NA WANAWAKE WANAGAWA URODA... HAPA NI BIASHARA HIVYO UKIJERUHIWA JUA KABISA UPANDE WA PILI IS NO LONGER NEED YOU...

Nashauri tujitunze na tuingie kwenye ndoa with our virginity... hata ndoa zetu zitakuwa na baraka za Mola Mlezi
Hakuna kitu inakatatisha tamaa kama kuwa mpenzi mtizamaji.
Yaani uko kwenye mahusiano alafu hakuna kufanya eti hadi muoane?yaani muwe wapenzi watizamaji tuu???kinachouma au katisha tamaa unaweza vumilia hivyo ukakuta demu kuna njemba inakula tena kimasihara huku wewe unapngwa eti hadi unioe ndo unapata.
 
Ndoa ni kuomba Mungu tu wanaume wa sahizi hawashtuki na bikra wanaongoza kutoa na kuoa hawaoi hao wanaowaanzishia
Ndoa MUNGU ndo anaandika na kudumu inategemea na Tabia zenu sio kuolewa ukiwa bikra
 
Alisema hawezi kunioa bila mimba,nimebeba hajanioa.nafunga namba ya simu.UMEANDIKWA IVO
Polesana kuzaa sio kigezo Cha ndoa muhimu kakupa funzo Lea mwanao mwaya na Utapata wako na wew
 
Pole
Maisha lzm yaendelee
Utapata mume wako,hakuwa wako huyo
Sasa unaharibu mrembo...kule umeongea point hapa sasa unasemaje hakuwa wako huyo wakati kosa ni la bidada kubeba mimba wakati hajaolewa
 
Ndoa ni kuomba Mungu tu wanaume wa sahizi hawashtuki na bikra wanaongoza kutoa na kuoa hawaoi hao wanaowaanzishia
Ndoa MUNGU ndo anaandika na kudumu inategemea na Tabia zenu sio kuolewa ukiwa bikra
Munguu aandiki ndoa bwana....hayo ni maamuzi yetu wenyewe. Ukiendekeza tamaa za mwili na ujinga utaishia kuliwa mbususu na watu kusepa. Miongozo tulishapewa sema hatutaki kuifuata
 
Munguu aandiki ndoa bwana....hayo ni maamuzi yetu wenyewe. Ukiendekeza tamaa za mwili na ujinga utaishia kuliwa mbususu na watu kusepa. Miongozo tulishapewa sema hatutaki kuifuata
Sawa
 
Uzi Bora kwa matumizi ya baadae kwa wale wadogo zangu
 
Munguu aandiki ndoa bwana....hayo ni maamuzi yetu wenyewe. Ukiendekeza tamaa za mwili na ujinga utaishia kuliwa mbususu na watu kusepa. Miongozo tulishapewa sema hatutaki kuifuata
Miongozo inafuatwa sana na wanawake wamejiongeza maarifa wanatengeneza za kichina maisha yaende hayanaga formula haya[emoji24]
 
Miongozo inafuatwa sana na wanawake wamejiongeza maarifa wanatengeneza za kichina maisha yaende hayanaga formula haya[emoji24]
Formula ipo sema ubishi wetu tuu....ndio tunaishia kuchukuliana kama vyombo vya starehe tuu
 
Back
Top Bottom