Kwa wanawake wote wanaotupenda wanaume tusio na kitu

Sina pesa.
Sina umvuto.
Sijui kuvaa vizuri.
Mabinti wote wananipita kushoto kama hawanioni vile.
Hata niliyemuamini naye kayeyuka kama barafu la mvua.
 
Ni wapenzi wangu..kama ishu ni kukwepa laana basi soma scenario hii hapa chini halafu unambie ningefanyaje kuikwepa...

Nilikua kwenye mahusiano na huyu mmoja ni single mother, nilimpenda mnoo..lakin yeye alikua kama hajali. Kuna Siku akaja kupost kitu kama anamshukuru jamaa fulan kwa upendo wake sijui kumjali lakini status ilifutwa (niliiona kwakua natumia yowhatsapp yenyewe ina mod ya ant delete). Sikumuuliza chochote nikaamua tuu kuachana nae bila kumwambia chochote.
Wakati huo pia nilikua na rafiki ambaye yeye alinifariji sana kipindi kile, na ikaja ikatokea tukaingia kwenye mahusiano.

Baadae kidogo yule single mom akarudi, na akanielekeza kila kitu kwamba hata kupost vile ilikua ni kwa sababu jamaa kwa miaka yote ile tangu mtoto amezaliwa hajawah kufanya chochote kwa ajili yake ila Siku ile alimnunulia nguo na viatu kwahyo akapost kumshukuru kwa hilo. Sababu zake zikaniingia nikaelewa, nikamsamehe maisha yakaendelea. Tukarudisha mapenz yetu upya, na akaniomba msamaha kuwa kipindi chote alikua kama hajali ila haikua vile alikua anaogopa kunionesha kwamba ananipenda sna kwa kudhan kuwa ntakuja kumuumiza nikijua hilo. Baada ya hapo tukawa deep sana mapenzini.

Siku kadhaa baadae yule mwingne akaja kuniambia kuwa ni mjamzito. Na kiukweli tukihesabu Siku pale kwa Siku ambazo tumekutana ujauzito ni wangu.

Utata ukawa namwambia vipi yule mwingne kwamba kuna mtu amenibebea Na ndo kipindi hicho tuko deep sana! Na kiukweli nisingeweza kumuacha mama kijacho au nimuumize hasa kipindi ambacho amenibebea. Sikutaka aumie hata kdg.

Ikafika Siku nikaona bora tuu nimwambie. Nikamuita nikamuelekeza, alichanganyikiwa hatar..akaondoka na kuniacha pale. Lakini badae akaniomba tuonane, akasema kuwa amefikiria situation nzima na anaona kuwa yeye ndo alinikosea, na kama asingenikosea haya yasingetokea japo pia nimempa adhabu kubwa sana..lkn hawez bila Mimi. M pia nikakiri kwamba bado nampenda.

Hapo sasa ikabid tukubaliane kuwa hata kama tunakua pamoja je ni kwa terms zipi..Mimi nikamuweka wazi kwamba makosa yashatokea lakini siwez kum treat yule mwanamke kama sehem ya kosa..yule ni bahati kwangu. Nae akakubaliana na hilo, akasema pia atajitahidi kumpenda mwanamke mwenzie mana yeye hana makosa. Mi nikamwambia zaidi ya kumpenda inatakiwa pia amheshim, kumheshim japo hawajuani. Tukakubaliana pia asiwe anakuja ghetto kwangu zaidi ya mi na yeye kukutana kwake.

Sasa bwanaa kila mtu kwa wakati wakee ananipenda mnoo, japo bado natafuta namna ya kumuacha huyu asie mjamzito
 
kama wanakupenda wote usiache mtu hapo

acha atae ona yamemshinda ajitoe mwenyewe

wapende wahudumie kila mtu ajihisi kama yeye ndo anapendwa

atae ona yamemshinda usimlazimshe abaki mpe nauli aende anapotaka

baki na utaebaki nae kisha Mu oe kabisa. kwisha.
 
Sasa we unampenda nani kiukweli kweli?
 
Asante sana mpenz wang kwa kunipend mimi kapuku sura ya buti,kula kwa kubangaiza,umekubali udharaulike sabab yangu.
 
Seriously am proud of ma wife. .she supported me whenever I needed her assistance.

She changed me alot mpaka ndugu zangu wananishangaa sikuhizi.
Alinikubali Kipindi sina kitu akanivumilia kwa hali yoyote

Alinifariji sana nilipokata tamaa
Mungu si jf nashukuru kwa hatua tuliyofikia sasa nina uwezo wa kumuhudumia yeye na mwanetu yote ni kwa uvumilivu baraka na ushauri wake.
Nina mpango wa kimsuprize Christmas hii na mungu atujalie afya furaha amani tele na maisha marefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…