Kwa wenye Uzoefu na Biashara ya Vituo vya Mafuta [Fuel Stations]

Wengi waliofanikiwa hawapendagi kuweka mambo hadharani
Kwa ishu kama hii wanakua wachoyo tu.
Maana hatujuani vzur lakn tukifanya hesabu ndogo, je 50% ya watu walioko JF wana mitaji mikubwa kias hiki?
Also, kila kona kuna vituo na wote wanapata faida, hakuna monopoly kama ilivo tanesco, so shida iko wap wakitema madini?
Kwa mfano huyu jamaa akifanikiwa kufungua kituo chake, kwan atakula faida ya mwingine?
Wabongo sisi wabinafsi sana sometimes
 
so far biashara ya mafuta sio monopoly in oligopoly kwenye hii biashara kuna ewura ambao hupanga bei ya ukomo kwa wauuzaji wakubwa na ma retailer meanwhile monopoly bei anaipanga yeye monopoly
 
kwa nyoongeza tu hakuna hela rahisi broo nao wanakabiliwa na ushindani ukiangalia wanauza bidhaa tofauti tofaouti though ni hio hio dizel na ni hio hio petrol lakn zimetofautiana ubora mafuta wanayouza total,puma,Bp na gapco sio sawa na mafuta ya wauzaji wengine ingawa yote ni mafuta hapo nakuelekeza kwamba sio monopoly.yaani ni kama mapishi mwengine ataweka Nazi mwingine hataweka
 
Kitu kinachongeza gharama kwenye petrol station ni mahengo ya ziada na kiwanja otherwise ukiwa na 100M unajenga vizuri tuu
Mil 100 humalizi Kituo hata kama una kiwanja ndugu yangu. Vibali tuu kuanzia building permit, andiko la nemc, certificate ya nemc, construction approval, OSHA, wakala wa vipimo, calibration, CRB, fire, halmashauri, roughly hapo mil 20 inaenda kwenye ivyo vibali. Tenk Mbili za Lita elfu 25 lazima zikule mil 28, canopy ndogo lazima ilaze mil 30 pamoja na Ufundi na hapo upate fundi mwaminifu, pump Moja ya Bei chee mil 12 yenye two product ivyo pump Mbili mil 25 pamoja na usafiri, stand by jenereta KVA 20 mil 23 mpk 28, Mfumo wa tra VFD mil 9, zege la chini kwenye canopy tuu mil 6, bango la Bei the cheapest mil 4 Bado wiring na vifaa vya Umeme na mataa. Nakupa uzoefu nimetoka kwenye Ujenzi Mwezi mmoja uliopita tuuna nimetumia force account, mkandarasi alitaka kunilaza juani na nakupa ushauri mkandarasi atakufanya ukitelekeze kabla hakijaisha maana ela itapukutika kama maji
 
Mbna wataalam wengi humu ndani hawataki kuweka madini hadharani?
Piemu piemu ya nini?
Share here kila mtu apate chochote
1.biashara ya mafuta ni nini?
2.bidhaa gani zinahusika katk biashara
3.unazifahamu kwa kiasi gani kuhusu hizo biashara hapa unatakiwa ujifunze japo kwa udogo bidhaa inazalishwa vip mzunguko wake mpaka inaitwa bidhaa
3.ujue njia angalau wanazotumia kutengeneza hio bidhaa
4.sasa ukijua hilo la juu inabidi ujiulize kwa umakin unaweza kuitengeneza
5.kama unaweza kuitengeneza basi jikite katika utengenezaji koz utapata faida kubwa zaidi na kama umeshindwa kuitengeneza utaipata vip sasa ? hapo unatakiwa upate njia rahisi ya kuipata
6.Ndio umepata njia ya kuipata basi jifunze namna gani unaifanya hii biashara hapa unatumia muda mwingi sana
7.unaangalia namna gani upate soko la uhakika
8.hapo unaweza kuanza kutendea kazi mradi wako.
Ukweli ni mchungu in biashara nzuri lakin kwa watu wanaojifunza kila Siku koz mifumo inabadilika technolojia zinabadilika
 
Duh

Mkuu unanivunja moyo boss
 
Umeongea sahihi sana mkuu

Wengi wetu tuna roho ya Kwanini, hawajui nikifanikiwa nitaweza kuajiri, kulipa kodi, kusogeza huduma jirani n.k
 
Hakuna biashara ambayo unaweza kuanza bila kuwa na misukosuko.

Wakati nimeanza biashara ya nyumba ya kulala wageni ilikuwa na changamoto Lukuki lakini baadaye nikawa napokea maoni na kujifunza.

Huezi amini kwasasa mtu anapiga simu kuomba kuwekewa chumba siku 3 au mbili kabla.
 
Hoja sio kuwa na ekari 5, hoja ni eneo lipo maeneo gani na linaweza kufaa hiyo biashara? Maana kila mmoja humu anaweza kuwa na eneo popote pale, ila haimaanishi kuwa kila eneo litafaa.

Kama una ekari 5 sehemu ambayo ni hotcake, basi hauwezi kuteseka juu ya mtaji.
 
Ni shihihi mkuu ila eneo langu lipo barabarani kabisa, Barabara ya Dsm - Mbeya.
 
Ni wazo zuri sana na nakupongeza ila ukiweza anza na oil chafu.. Hii mtaji ni mdogo faida ni kubwa na uwekezaji wake sio complicated
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…