Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Kuna siku nilisafiri usiku kutoka mwanza kuelekea kishapu shinyanga aiseeh ile barabara ni nyembamba alafu malori yanawasha full na bado yanatanua kilichonisaidia ni zile sport lights nilifunga kwenye gari vinginevyo.......
 
Umesema vyema sana ila Kwa sasa 2022 na 1992 utakubaliana na Mimi kuwa Hali ni tofauti, sababu kubwa haikua barabara tu ila ni Ulinzi na usalama kutokana na mapori makubwa ila Kwa sasa, kwa mfano Kahama to Nyakanazi ya 1992 sio Kahama to Nyakanazi ya 2022, Eneo kubwa limejengwa na Eneo lote ni lami , sasa Kuna sababu Gani magari ya Bukoba kwa mfano, yalazimishwe kulala Kahama na sio Nyakanazi? Huu ni mfano.,..
Pia uhitaji wa abiria kusafiri Usiku umekua mkubwa sana, je tuwaache waendelee kudandia Malori na magari ambayo sio official kubebea abiria au tu-officialize?

Kumbuka, Kwa sasa, mabasi yapo yanayofika Dar asubuhi au Usiku wa manane kama Yale ya Kutoka Kigoma, Kasulu, Bukoba, Karagwe na Katavi, au Yale ya Mbeya to Mwanza, wanafika alfajiri, point Yangu ni kwamba hizi route ziruhusiwe, hazina madhara kama hayo makubwa kiasi hicho kikubwa madereva wawepo wawili kama wale wa Songea to Mwanza ambao hufika siku inayofuata......
 
Ewaaaaaaa Majinja alikua anaanzia Lindi nadhani, Dar then Mbeya pia alikuepo Rungwe na Osaka au Chakito kama sijakosea, akaja Dar Express au Kilimanjaro wote hawa wamezuiliwa ila coaster zinaruhusiwa...sasa hizi ni akili au matope?!
 
Root ya usiku imekaa Poa…Japo kuna changamoto kwenye barabara zetu haziruhusu root hyo ifanyike kwa fasaha.

Changamoto nyengine ni mabasi na madereva.
Hakuna shida kwenye barabara, ni kuongeza tu madereva
 
You nailed it Bro
 
Uchumi utachangamka saa 24.
Vituo vya mafuta watauza saa 24,wausau chakula watauza saa24.wenye mabasi watasafirisha abiria mara 2 zaidi.

Uchumi utakuwa angalau mara 2,mchana na usiku ni kuendelea kulijenga taifa.

Miji itasafishwa mchana na usiku.
Ajira itaongezeka mara 2, wenye viwanda watafanya kazi usiku na mchana.
 
Yes, hakika umeeleza vyema?
 
Ewaaaaaaa Majinja alikua anaanzia Lindi nadhani, Dar then Mbeya pia alikuepo Rungwe na Osaka au Chakito kama sijakosea, akaja Dar Express au Kilimanjaro wote hawa wamezuiliwa ila coaster zinaruhusiwa...sasa hizi ni akili au matope?!
Akili za polisi utaziweza? Sasa zikutane na za wanaccm wenye uchu wa madaraka na kupenda sifa wasizonazo wala wasizozistahilu, hapo unategemea nini?
 
Kweli kabisa, mimi nikisafiri hua natapika sasa hua nalala ili kuzuia hiyo hali. Safari ikiwa usiku ni raha mana ntakuja na net kabisa na dawa ya kuua mbu.
Ukiwa unasafiri fungua kioo cha dirisha tazama nje,vuta hewa ya nje hiyo ndiyo dawa ya kuzuia kutapika.Mimi hiyo ndiyo dawa yangu siku hizi sitapiki tena.
 

Usafiri wa ndege ni bora sana sababu kubwa ni kuwa hauna vizingiti vya wapumbavu wote.
 
Nauli za ndege ziwe rafiki, serikali iruhusu ushindani wa ndege kwa mashirika mengi ya ndege kuja kuoperate Tanzania.

Treni ya Mwendokasi Dar-Dom-Mwanza/kigoma iharakishwe, reli ya kusini kuelekea Mbeya to Tunduma iboreshwe.

haya yote yakifanyiwa kazi idadi ya wasafiri kwenye mabus itapungua na wengi watakayoyatumia watakuwa hawana haraka hivyo maspeed na mambo ya hovyo barabarani yataondoka.

Usafiri wa barabara Km1000 na zaidi ni ujinga sana na ni risk sana na mpaka sasa unachukua sana roho za watu.
 
Kipindi Fast jet anakwenda Mwanza kwa bei bwerere abiria wa mabus kiasi fulani walipungua, tumeruhusu ATCL amemonopolize soko na kuufanya usafiri wa ndege ni anasa kwa mabei ya nauli ya ajabu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…