Kwahili la Mabasi kusafiri Usiku, nampongeza Mbunge Tulia Ackson

Mbona unakuwa so pessimistic? Kwa nini ufikiri au uamini ni mabaya tu yatatokea?
Kwa kweli mkuu nami huwashangaa sana watu wa hivi. Na ikitokea mtu wa hivi akapewa madaraka na fursa ya kufanya maamuzi basi ujue mtarudi kwenye ujima, they don't like changes and always they think of negativity.
 
Hayo ni mawazo yako tuu, na siyo lazima ya reflect ukweli wowote. Spika aliwahoji maofisa wa polisi kwenye kile kikao je mna any scientific evidence ya hilo zuio? Wao kimyaaa, mbona gari za maiti zinasafiri usiku? Wao kimyaa. In short wamekariri tuu na hata huo mwaka 1992 waziri mkuu alivyozuia it was mihemko tuu ya wanasiasa ya kutoa matamko kupata political millage kwa sababu ilitakiwa ufanyike utafiti kabisa wa kitaalamu kabla ya kuweka zuio.
 
Well said... Kingine kwa nini wasiende kujifunza kwa nchi nyingine ambako usafiri wa usiku ni kawaida kabisa?
 
Ndio, Kwa sasa ni Kigoma tu ndio Ina changamoto
Kipande kidogo sana kimebaki maybe 150 km majuzi nilipanda nice bus, nimesahau jina, yaani full kipupwe mpaka tukafika, ila tukalala sijui ni Kaliua pale kama sijakisea.
 
Na haya ndiyo maendeleo 24 hours watu wanafanya kazi...
 
Kwa madereva watanzania hawa gari kutembea usiku ni hatari

Wengi walevi na hawapati muda wa kulala
Kukiwa na options za bus za usiku na mchana nyie waoga wa kupanda Bus za usiku si mtapanda za mchana?? Tatizo liko wapi? Mbona kuna watu wanapanda mpaka gari za usiku za magazeti na coaster? Ninachosema ni kwamba tuache kupangiana maisha...
 
Hatari zipo nyingi

Ilishawahi kutokea saa sita usiku dereva akasinzia kwenye usukani gari iliacha njia
Mungu saidia ilikuwa tambarare
Tupe statistics kwamba ajali ngapi kwa mwaka kwa usiku ukilinganisha na mchana? Tuongee kwa data, na kwa nini wasiwepe chuo cha taifa cha usafirishaji na UDSM watufanyie tafiti na kuja na majibu based on research??
 
Kipande kidogo sana kimebaki maybe 150 km majuzi nilipanda nice bus, nimesahau jina, yaani full kipupwe mpaka tukafika, ila tukalala sijui ni Kaliua pale kama sijakisea.
Itakuwa Aifola wako poa na higher zao
 
Umeongea vema mkuuu.. Mimi katika vitu ambavyo nimemkubali spika ni hili la kukemea hili zuio la kijinga kabisa la bus zisisafiri usiku.
 
Mimi kwa Safari za usiku labda kwa sharti moja kubwa Tuu wanaondesha mabasi usiku lazima umri wao uwe kuazia miaka50 kwenda Juu ili Dreva awe na nidhamu kubwa usiku
Mkiwapatia awa madreva vijana kumbukeni hili ni muhimu sana
Utachagua bus za mchana, hakuna wa kukulazimisha... Hata sasa hivi kuna choices mbalimbali, bus la kawaida, semi luxury, super luxury lenye mpaka choo ndani nk it's your choice..
 
Sasa huko nchi zingine za Africa, hata jirani zetu Kenya tuu hapo wanasafiri usiku. Nyie huo uzoefu mnautolea wapi?
 
Nafikiri nia ya serkali kutoruhusu magari kutembea usiku ilikuwa njema, hasa ukizingatia sababu za kiusalama. Ni kweli nchingi zilizotuzunguka magari yanatembea saa zote. Lakini kwetu kimekuwa na matatizo ya kiusalama hasa yale maeneo yaliyopakana na Rwanda, Congo, na Burundi. Pia kwa ile njia ya kati kumekuwa na utekaji mwingi na raia kunyang'anywa kila kitu. Mimi mwenyewe kidogo linipate hili, bahati nzuri tulijulishwa mapema. Hili likiruhusiwa lazima tuangalie utekelezaji wake. Pia kuna hili tatizo la mwenda kasi na ajali. Kama madereva wataendesha kwa kasi na kupata ajali itakuwa kazi kupata msaada. Mara nyingi ajali zikitokea raia huchangamkia mali za majeruhi badala ya uwasaidia. Tujiulize, je tukiruhusu mwendo wa usiku tumejitayarisha vipi kutoa msaada iwapo itabidi.
 
Yaani Tanza-nia peke yetu ndio tunaojua kuendesha speed? Hili hapana, suala la usalama Hilo ni udhaifu wa Jeshi la Polisi ila Kwa sasa maeneo mengi ya nchi Yako salama Baada ya Ujenzi wa barabara, kwa mfano mtu anayekwenda Arusha, anapita Wami (lilikua Eneo hatari) then anafika Mkata unamzuia! Hili nalo tunaliwekaje?
 
Tupe statistics kwamba ajali ngapi kwa mwaka kwa usiku ukilinganisha na mchana? Tuongee kwa data, na kwa nini wasiwepe chuo cha taifa cha usafirishaji na UDSM watufanyie tafiti na kuja na majibu based on research??
Yaani wanaamini kwenye ajali Zaidi kuliko usalama, ni sawa na Mtu aseme "sitaenda kazini/kibaruani Leo mvua inaninyeshea maana nje Kuna wingu". Ndio AKILI za Wabongo Wengi
 
Kilimanjaro waliruhusiwa siku mbili tu nadhani

Nilisafiri kwa raha Jamani, Mara ghafla wakanyimwa kibali

Tukarudi kwenye coaster zetu zilizojaa usumbufu na pia ni very uncomfortable.

Serikali iachilie mabus yasafiri usiku tu Manake Kama ni ajali hata mchana zipo Za kutosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…