Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Huyu amekosa weledi wa kuwa Mkuu wa nchi, uwezo wake unaishia kwenye ujenzi wa barabara tu.
 
Kiukweli mh. Amewaangusha sana watanzania namna ya kupambana Na ugonjwa huu, alishauriwa mipaka ifungwe ili usiingie nchini, lakini akapuuza.Kwa sasa dar ndo inatumika kusambaza mikoani huu ugonjwa, serikali imeshauriwa itenge dar Na mikoani mingine lakini bado viburi vimetawala.Nikiangalia bunge letu pale Dodoma halina msaada kabisa namna ya kusaidia umma kupambana Na ugonjwa huu, yaani hata kujadili tu kama taifa barakoa Na sanitizer zinawafikiaje wananchi kwa bei ya chini hakuna.
 
Mleta uzi unapodai lockdowns vile vile dai na mikakati ya kiuchumi kuwasaidia hao mnaotaka wafungiwe ndani!!
Msipokuwa makini njaa, sonona n.k vitaua watu wengi zaidi ya #Covid-19
Lockdown sio lazima kuwafungia ndani ndugu, twaweza Fanya kama mataifa mengine.mfano dar Na mikoani mingine watu wazuiwe kutoka Na kuingia.
 
Hawana maarifa hayo Mkuu, wao wanachoweza ni kuteka na kupoteza raia wema tu. Serikali ya hovyo mno hii.
 

Lets do the necessary mkuu. Ugonjwa ni mpya hivyo hakuna mwenye uhakika fully kama ilivyp kwa mengine ya muda mrefu kama HIV. Ila tayari tushaelekezwa ni ni cha kufanya mwanzoni ila kama zikitokea findings zinginezo hautodhuru
 
Hii ni petition
Ungeiandika na kuattach majina na sahihi zako pia ukatuomba na sisi kuongeza sahihi kesho ifowadiwe kwa Rais kupitia account yake ya twiter na email ya ikulu
 
Mpaka sasa ventilators zimepungua mloganzila na amana.
Soon zinachukuliwa za muhimbili wakati za Mkapa zimefuatwa.
Tutakufa haswaaaaa
 
Wenzio marekani wanaandamana hawataki lock down. Wewe unaleta ngonjera zilizowashinda wenye uwezo kiuchumi. Iko hivi, maisha yako yanathamani kwako. jifungie ndani wewe na familia yako na serikali itakuunga mkono. Hivyo videbe vyako vya mahindi ulivyoweka stock visikutie kiburi ukaona umeyapatia maisha.
 
Nimekwambia huko ulaya nchi nyingi watu wanapukutika haijarishi aliyefanya uzembe au asiyefanya ila wewe bado unashikilia habari za uzembe na huko Russia watu 300 washapukutika na wakati wao walifunga mapema tu mipaka yake.

Mkuu unajielewa lakini?

Hiki hapa nilichokuandikia:

"Kwamba ulaya au marekani ugonjwa uliingia hakuhalalishi kutokuwepo uzembe uliopelekea ugonjwa huu kuingia kwetu."

Unaionaje statement hiyo pamoja na maelekezo iliyoambatana nayo?

Palikuwa na nyuzi nyingi tu kabla ya ugonjwa kuingia na kabla sana ya ugonjwa kusambaa:

Corona ni uzembe wetu isingetufikia, na itatumaliza tusipoamka sasa - ukweli mchungu - JamiiForums

Mkuu au ndiyo kuwasili tokea sayari nyingine?
 
Sasa tufanyeje? Dereva wa fuso kazuiliwa mtukura ana corona unadhani tajiri yake atamlipa? Huoni keshafukuzwa kazi tayari? Tajiri atapeleka dereva mwingine huyo atajijua, semeni chakula hamna ndio kwanza mmeanza kununua mahindi sumbawanga
 
Hii ni petition
Ungeiandika na kuattach majina na sahihi zako pia ukatuomba na sisi kuongeza sahihi kesho ifowadiwe kwa Rais kupitia account yake ya twiter na email ya ikulu

Mkuu maboresho ruksa lakini hiyo ndiyo habari yenyewe. Hakuna woga wala nini. Baba askofu kaonyesha njia.

Beleshi kwa jina lake. Huu ni mwanzo tu. Mabadiliko ya sera na mtizamo kwa ugonjwa huu ni sasa.

Ulokole na ucha Mungu ni suala zuri tu. Lakini hilo ni suala binafsi haliwezi kuwa agenda ya nchi.
 

Mnasoma mkaelewa au yaleyale ya kudandia treni kwa mbele?

Marekani kama ilivyokuwa Spain, Italy, Germany, china nk ugonjwa wamesha udhibiti. Wanaopona in a given time ni wengi kuliko wanaoambukizwa. Kwa maana nyingine idadi ya wagonjwa mahospitalini inapungua.

Ikifikia hapo kwa uangalifu na logically hatua kali zinaanza kupunguzwa kurudi kwenye normal life. Kumbe wewe unadhani imewashinda?

Mnakwenda shule kuhitimu umburula? Kwa nini hawawapokonyi hizo PhD. Usomi wenu mbona ni aibu kwa jamii?

Hata videbe unavyosema huenda ninavyo, sina Ila hata kwa uji tu najua siwezi kufa njaa katika siku 21.

Mbona jela na rumande mnawalisha watu mlo mmoja bado hawafi?

Msitake kuwaweka watu wote hatarini kwa tamaa tamaa zenu za kula kula kilafi. Kula ni muhimu lakini si kuwa ndicho pekee ambacho inabidi kuwa akilini na hata kama unahakikishiwa kuwa hakuna atakaye kufa njaa.

Halafu rejea hizi za kuangalia marekani na ulaya ni kwa ajili ya kulikuza mno suala hili ili kuonekana kuwa haiwezekani?

Hapo Kenya, Uganda au Rwanda hohehahe kama sisi hakufai kupigiwa mfano wala kuwepo katika rejea zenu?

Ama kweli mburula ni mburula tu hata liende shule vipi na hata likazamia kabisa ni mburula tu na litabakia pale pale.
 
Naona unataka kucopy Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unataka kucopy Rwanda

Sent using Jamii Forums mobile app

Sidhani kama ni hivyo. Tufanye kivyetu lakini tuna nafasi ya kujifunza kwa wengine. Tukijiridhisha hata ikibidi kucopy na ku paste ni sawa tu. Muda unayoyoma sana.

Hivi hawa mabalozi wetu huko nje wanafanya nini? Kada hii nyingine nayo ni ya kuangaziwa. Inafanya nini? Hata kutushauri tu, kuweza kupenya hapa salama hakuna?

Au yaleyale woga kwa kwenda mbele? Si mjiuzuru basi tujue kuwa angalau hamkukubaliana?
 
Duh! Mkuu labda wewe tu hujanielewa, mara nyingi watu wamekuwa wakitaja Marekani Italy na Spain kuwa zilifanya uzembe na kututaka sie tujifunze kupitia makosa waliyofanya hizo nchi ili kudhibiti huo ugonjwa. Lakini wakati sie tunataja hizo nchi kuwa zilifanya uzembe kiuhalisia huko ulaya ni nchi nyingi tu zilizoathirika na corona na ndiyo hoja yangu kwamba tatizo sio uzembe na kudharau bali hili ni janga la wote na ndiyo maana hata wale wasiosemwa kufanya uzembe nao hawako salama wanakufa kama wenzao. Urusi alichukua hatua mapema kufunga mipaka ila mpaka sasa ana idadi kubwa ya vifo kuliko sisi huku. Sasa kung'ang'ania kwamba sijui tulisema mapema hivyo ni uzembe sioni cha maana katika hizo lawama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…