Kwako Rais Samia, sisi Askari tunaomba utuongezee maslahi

Kudai 15,000 kwa siku kama posho ya kula ni hela nyingi. Elfu 10 inawatosha, hiyo ni hela ya kuongezea kwenye bajeti yako sio ya kukulisha moja kwa moja. Otherwise hoja nyingine ni za msingi msikilizwe
Kakwambia maisha yamekua ghali sana na akatoa moja ya sababu ni mipaka kuwa wazi,hivyo kupelekea ughali wa maisha,hiyo elfu kumi huoni ni ndogo au unamfikiria yeye tu hufikirii familia yake na wategemezi wake wengine ambao wapo nyumbani kwake?
Umewahi kufikiria kwanini wanachuo wameongezewa boom na JW hawalipwi elfu kumi kama wizara ya mambo ya ndani wanavyowafanyia askari waliopo kwenye hiyo wizara?
Hizo hoja zinatakiwa zifanyiwe kazi,zote ni za msingi.
Wasaidizi wa IGP na Rais,wanatakiwa wawafikishie wahusika,kwenye majeshi inasemekana kuna ulaji mwingi sana wa pesa,unafanywa na wakubwa wao,matokeo yake,JW wanaonekana maslahi yao ni makubwa,kumbe wao pesa zinawafikia moja kwa moja,kwenye mishahara yao.
 
Asante kwa kuumia na wanaoumia mungu akubariki
 
Hongera Afande. umeongea Kwa Hisia na Nina Imani. Kwa Upendo wa mama Samia. Atasikia ulichoomba.
Mkiongezewa mtukumbuke na sisi tuliopenda Kuwa Askari lakini tunazeekea Tu uraiani.
 
➕ RUSHWA na KUBAMBIKIA WATU KESI! Nyinyi jamaa si mtakuwa matajiri sana. Bora hata wangeongezewa askari magereza. Ila siyo nyinyi polisi.
 
Kwahiyo mnataka itoke Posho ya laki 300,000 Kwa mwezi iende 450,000 Kwa mwezi!?? Halafu ulipiwe maji na umeme!??aiseee!!! Hatari!! Hivi Ina maana huwezi kujilipia umeme Kwa mwezi shiling 20000!? Aisee !! Hatari!!
 
Kwanini mnapenda kufanana kimaslahi na JWTZ wakati nyie mna majukumu tofauti na wao basi ombeni mshirikiane kwenye majukumu yao mpelekwe Msumbiji mkawatoe magaidi
 
Mimi nilikuwa nauliza, hivi hiyo hela ya ngome huwa mnapewa au hampewi ndio mnataka mpewe?
 
Labda ni "mshikaji" wake. Ndiyo nasema nidhamu ya Kijeshi kwenye Jeshi la Polisi imeshuka sana. Sheria na taratibu nyingi sana za kuendesha Jeshi la Polisi hazifuatwi kama ilivyokuwa zamani.

Nidhamu ya kijeshi sio siasa na blah blah.

Afisa wa ngazi za juu akiwa na wenzake anasepa na 4.5 bilion igp amesimama hajui afanyaje halafu unahubiria askari nidhamu ya kijeshi[emoji2][emoji2].

Maana yake askari atamuona igp ni kama mshale wa sekunde tu ktk saa hana kazi,achia mbali huyo inspector,hakutakuwa na nidhamu hapo.
 

Mungu awabariki viongozi wa JWTZ,hata kama wanaiba basi wanaiba wakiwa na hofu ya Mungu.

Hizi kampuni nyingine hizi kuna matapeli walivaa khaki wakijifanya walinzi wa usalama.manyota kibao fix tupu.
 
Kwahiyo mnataka itoke Posho ya laki 300,000 Kwa mwezi iende 450,000 Kwa mwezi!?? Halafu ulipiwe maji na umeme!??aiseee!!! Hatari!! Hivi Ina maana huwezi kujilipia umeme Kwa mwezi shiling 20000!? Aisee !! Hatari!!

Anaweza kujilipa ila kimsingi pesa hiyo ataichukua kwako raia,halafu utakuja ulie lie hapa polisi wana njaa mpaka buku 2 wanabeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…