Uchumi unaendana na wakati mkuu , labda kukuelewesha katika kipindi cha Kikwete wahitimu walikuwa wachache sana na waliendana na spidi yetu ya ukuaji wa uchumi... mfano mzuri tu ni kwamba shule zilikuwa zikijengwa kwa wingi na Zahanati na vutuo vya Afya ambako kulihitajika wafanyakazi ....Pili kikwete alikuwa akisaini mikataba mingi ya Kisela ambayo ilitengeneza Money influx ya kuweza kuajiri watu wengi huku akiwa hana Miradi mikubwa alioanzisha inayohitaji hela nyingi ... Upande wa Magufuli alihitaji hela nyingi kwenye miradi ambayo mingine ilifanikiwa na mingine ikafeli kitu kilichopelekea kukosekana kwa balansi.Ni staili tu za uongozi lakini haimaanishi kulikuwa na maendeleo.
Alichokosea Magufuli ni kuchukua kodi kinguvu huku akitaja malimbikizo ya Kodi yalipwe kwa wakati mmoja na hili lilipelekea biashara nyingi kufungwa , Lakini swali nani alitengeneza tatizo hili la biashara kukimbikiza kodi , utagundua ni Kikwete.
Nchi haiwezi kuendelea ikiwa misamaha ya kodi ni kila mahala huku ni kudidimiza uchumi.