Kwanini Afrika tunashadadia Mapinduzi ya Kijeshi?

Hakuna mfumo wa uchaguzi wa kumuondoa mtawala na chama kongwe au kilichotawala kwa muda mref ndani ya bara la Africa!! Wameona hiyo ndio solutions cha kushangaza wananchi wanasapoti jeshi kuchukua Nchi........... Think bout it!!
 
Dikteta Jjiwe nae angeondolewa na jeshi,alishaonyesha nia ovu
 
Kwasababu kuna wajinga wanajimilikisha nchi
 
Wewe huoni ni jinsi gani utawala wa kiraia kupitia vyama vya siasa vinavyojimilikisha madaraka na kuiba chaguzi. Kwa chaguzi kama za 2020 hapa Bongo unategemea nini!? Hivi kweli kwa sanduku la kura unategemea nchi kama Tanzania, Uganda, Rwanda au Burundi kufanikiwa.

Sasa hivi tayari wameshakuja na Mikakati kuwa kwanza wanatoa elimu ya katiba kwa miaka 3. Baada ya hiyo elimu ndiyo waanze mchakato. Wanatuona wananchi ni mazuzu.

Next coup ni Equatorial Guinea au Cameron kabla ya kutelemka to East Africa.
 
Uko sahihi sana kiongozi,

Mathalani Niger,
ufaransa iliamuru Rais Bazum kumtimua kazi mkuu wa majeshi Gen.Tchiani ambae sasa ndie kiongozi wa Mapinduzi, kwa mtazamo wake tofauti na Rais Bazum kuhusu uwepo wa makambi ya Jeshi la ufaransa na Marekani ktk ardhi ya Niger. Sasa b4 hajafutwa kazi akafanya yake na kazi ikawa imekamilika.

Hizi ni miongoni mwa baadhi ya sababu nyingine zilizopelekea Mapinduzi na zitakazoendelea kuwaondoa mamlakani viongozi wengi barani Africa.

Usaliti miongoni mwa viongozi.
Kuzorota kwa uchumi kupindukia,
Kuzorota kwa hali ya kiusalama,
Umaskini wa kutupwa,
Rushwa kupindukia na iliyokithiri kitaasisi.

Ukosefu wa ajira kwa vijana.
Nguvu ya mataifa ya nje kiuchumi na ushawishi ndani ya serikali za Africa.
Kuzorota kwa hali za maisha ya watu na makazi yao.
Njaa na ukosefu huduma muhimu za afya, maji, umeme, Elimu n.k.

Kutofautiana falsafa ya kuongoza. nchi miongoni mwa viongozi.
Uchu na ulafi wa Madaraka.
Kupuuzwa kwa Katiba, utawala wa Sheria na utawala bora.
Kubinywa na kukandamizwa kwa haki na uhuru wa habari na kujieleza.

Kupuuzwa kwa Demokrasia.
Kung'ang'ana Madarakani kwa nguvu au kwa wizi wa kura.
Kukandamizwa haki za binadamu na usawa.
Mabadiliko ya Katiba na Sheria mbalimbali za kuwabakiza viongozi mamlakani.

Haya ni baadhi tu ya mambo machache yanaweza kuchochea Mapinduzi.
 
Kwa sababu ya viongozi ovyo ambao Watu wachache wajinga kama wewe mnawasapoti.
 
Ni vigumu sana kiongozi aliyeingia kijeshi kutolewa kwa sanduku la kura! Mkianza kupinduana, mtaendelea tu!
 
Moja ya sababu ni hizi,sio kwamba wengine wanafanya Kwa kupenda.
Gabon's former President Omar Bongo had 70 bank accounts, 39 apartments, 2 Ferraris, 6 Mercedes Benz cars, 3 Porsches and a Bugatti in France.

He ruled for 42 years (from 1967 to 2009).

His son, Ali Bongo has been President since 2009.

He has just been overthrown in a coup
 
Kwa kweli Afrika sijui niseme nini, sasa hata kule Niger ECOWAS itazidi kupata kigugumizi cha kuwaondoa wale wanajeshi waliopindua serikali halali. Na hakuna ushahidi wanajeshi wataleta neema wananchi wanayodhani wataipata. Ni sawa tu na nchi nyingine kama Kenya, Tanzania nk. ambazo wananchi wanakuwa na mzuka kwa raisi fulani anapogombea kisha akikaaa kidogo madarkani wakibaini hawezi kutimiza zile shauku zao wanaanza kumchukia ghafla.

Mfano HAPO KENYA Ruto alidhaniwa ataleta neema ya kiuchumi lakini ilivyoonekana neema haipo kirahisi walewale waliomchagua wanaanza tena kuandamana. Sudani ni hivyohivyo walimtoa Albashiri nini sasa wamepata?

Ni bora wananchi wenyewe wangeandamana jeshi likawasapoti lakini siyo kujifanya linachukua madaraka huku haijulikani ni lini watayakabidhi kwa raia, wanajeshi ni binadamu kama walivyo hao maraisi kwahiyo tusishadidie sana jeshi kushika madaraka.

Nadhani kuna mkono wa Urusi hata kama siyo moja kwa moja lakini Putin na New Order yake ana agenda fulani ya siri na Afrika tusipoangalia tutageuka vibaraka wa Urusi sawa tu na tulivyokuwa vibaraka wa nchi za Magharibi. Tunapigana Vita vya Ukraine bila kujijua
 
Jibu ni simple sana...raia wanashadadia jeshi lifanye hivyo kwasababu Hilo jeshi ndio linalofanya hai viongozi wasitoke Kwa kura halali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…