Kwanini Afrika tunashadadia Mapinduzi ya Kijeshi?

Kwanza nipende kusema mleta mada umeandika uongo huenda ulikua unajua au hujui chochote, nipende tu kukwambia mgabe hakupinduliwa kama unavyozania wew, ndio maana unapaswa kujiuliza baada ya hayo mapinduzi feki ni kwanini marekani na umoja wa ulaya hawakuondoa vikwazo vya kiuchumi kwa zimbabwe.

Kingine demokrasia ni jini ambalo linatafuna haki ya waafrika katika kufikia maendeleo yaliyo bora sababu inamapungufu mengi hata kwa waliyoileta huko ulaya na marekani mfano ni chaguzi za marekani hilary clintoni alimzidi kura Trump mwisho wa siku Trump akawa raisi, ukija kwa biden nae alimzidi Trump na tukaona Trump followers wa republican walivamia bunge kufanya vurugu kwa kupinga matokeo.

Hapa ndio utajua kuna watu nyuma ya pazia wameishikiria marekani na wanaamua nani awe raisi kwa wakati upi na nani asiwe raisi, jambo hili hata hapa nyumbani Tanzania tumeliona mwaka 2020. Ndio maana nasema ni upumbavu kupanga mstari kwenda kupiga kura wakati kiongozi alishajulikana ni yupi.

Tukija kwenye mada yako, mie naona ni ulimbukeni kwa wanaoshabikia (coup d'etat) mapinduzi ya kijeshi zidi ya viongozi wa kiafrika waliokuwa si waadilifu kwa nchi zao.

Sababu haitaweza kuondoa matatizo mengi yanayozikumba nchi za afrika hasa tatizo la umaskini. Nimalizie tu kwa kusema time will tell.
 
Upo sahihi.
Libya walimng'oa Ghadafi wapate Rais mzuri zaidi ya Ghadafi.sasa hivi hata yule Ghadafi mbaya wanamtamani arudi lakini awampati.
 

Hizi point hakuna hata moja ambayo hai apply Tz
 

Umeonyesha mapungufu ya democrasi ila hujaonyesha ni mfumo upi bora wa kisiasa,mimi naamini democrasia ndio mfumo bora wa kisiasa shida ni kwamba democracia ni rahisi sana kuingiliwa na wenye nguvu.
 
Kuna chama nchi fulani kinajifanya hakioni yanayoendelea hizo nchi nyingine...kiko madarakani miaka yote...viongozi wanabadirishana tu vitengo..mzunguko ni uleule..familia ni zilezile...matatizo ni yaleyale

Hivi hawa watu wa mabakamabaka hawashtuki na hawaoni..wakaondoa hii kadhia??
 
Watu wanataka wezi wapya sio kila siku wezi hao hao tu na watoto wao. Mwizi mpya anaweza kuja na mbinu mpya za wizi zinazoweza kuwa na unafuu hata mtoto wa masikini akaambulia makombo.
 
Ni Kwa sababu kura hazijawahi kuwa njia Bora ya kupata uongozi mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…