Kwanini Afrika tunashadadia Mapinduzi ya Kijeshi?

Watu wanataka wezi wapya sio kila siku wezi hao hao tu na watoto wao. Mwizi mpya anaweza kuja na mbinu mpya za wizi zinazoweza kuwa na unafuu hata mtoto wa masikini akaambulia makombo.
Aaahaaaa,naunga mkono h
Sawa mkuu
 
Shida zimezidi na mifumo ya serikali nyingi za kiafrica zinawapa ulaji jamii ya watu wachache walio kwenye mfumo hivo kupelekea wananchi kutowapenda viongozi wao na pale inapotokea mabaidiliko ya kiuongozi wananchi hufurai wakiwa na matumaini ya huenda hali itabadilika.
 
Pia viongozi wengi wa kiafrica sio machaguo ya wananchi.
 

Tafta taarifa sahihi za Siasa za US.
Hiki ulichokiandika hapa ni kanjanja.
 
Hamna uchaguzi huru na wa haki.
 
Ndio njia pekee iliyobaki ya kuwaondoa madarakani wasiotaka kutoka kwa hiari kwa kuheshimu kura za wananchi.
 
MKUU NI KWAMBA HUJUI AMA?

Hivi ni kweli wewe huwa ufuatilii mambo yanayotokea humu AFRICA wakati WA uchaguzi,ufuatilii hatua zinazo chukuliwa na viongozi wa Africa wanapokosolewa kistaarabu kabisa kuwa hapa Mheshiwa Raisi umepuyanga.

NB: kukaa madarakani muda mrefu sio shida,shida unafanya Nini?
 
Yapinduliwe tu TUMECHOKA. Mleta uzi upo hapa hapa Africa. Na chaguzi zake unazijua. Rejea uchaguzi wa Tanzania 2020. Ukiona jeshi linapindua na wananchi wanashangilia, tambua kwamba walishachoka, na kwenye sanduku la kura wamefanyiwa u-JECHA mara kadhaa.
 
Kuna mwingine uganda....yeye Alisha sema wazi wazi......yeye ni kotapini Ile ya kwenye baiskeli...kotapini Huwa inaingia Kwa kugongelewa na nyundo...pia utokaji wake ni Kwa kuigonga....Huwa kotapini haitokagi kirahisi rahisi....
Mzee Museveni juzi amesema ya kwamba yeye HANA uchu wa madaraka SEMA tu Waganda ndio wanataka aendelee kuwa Rais wao na ndio maana wanamchagua Kila uchaguzi! Ahahahahaha!!!
 
Mzee Museveni juzi amesema ya kwamba yeye HANA uchu wa madaraka SEMA tu Waganda ndio wanataka aendelee kuwa Rais wao na ndio maana wanamchagua Kila uchaguzi! Ahahahahaha!!!
Alaf akasema ni marufuku Kwa Uganda kuuzwa nguo za mitumba..........

Akaziita Nguo za MAREHEMU WA ULAYA 😊😊....Nimarufuku kuuzwa miguo ya mitumba Uganda
 
Alaf akasema ni marufuku Kwa Uganda kuuzwa nguo za mitumba..........

Akaziita Nguo za MAREHEMU WA ULAYA 😊😊....Nimarufuku kuuzwa miguo ya mitumba Uganda
Ni kweli kasema hivyo, lakini Rais Magufuli alijaribu hilo la kuzuia mitumba nchini Mkataba wa AGOA ukambana. Labda Museveni atafanikiwa.
 
Watu wanataka mabadiliko makubwa. Hapa Africa usulutani hauwezi kuwepo kwa namna moja au nyingine.

Kwamba wewe mtoto wako na wajukuu wako mfaidi rasilimali za taifa kisa tu mlipewa dhamana za kuwa viongozi? Mbaya zaidi mnafaidi kwa ufisadi na uhuni wa kuwaona mnaowatawala wajinga na wapumbavu.

Mapinduzi ya kifikra na ya kuondoa viongozi mafisadi wasiofaa yameenea Africa nzima.
 
Kinachoendela Afrika ni sawa na kile kilichotokea Ulaya mwaka 1848. Mapinduzi yalitokea Ufaransa, Ujerumani, Austria, Ukraine, Poland nk na kulikumba bara zima. Watu walikuwa wakijisikia tu, wanaenda kupindua mfalme.
Kama ilivyotokea ile Arab spring iliyoanzia Tunisia na kuendelea nchi zingine za kiarabu baada ya yule kijana wa Tunisia kujichoma moto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…